CIA haimtambui Kikwete kama ni DR? Inatambua DRs watatu tuu katika Serikali ya JK!

Hao ni doctor of medicine and vertenary doctor ndio maana wanawatambua!! Hivi unajua kuwa hata barack obama ni phd holder but ulishasikia wanamuita dr obama????

Safi sana, ukituondoa sisi M.D na wale Vet. Doctors, wanasiasa watz wanafikiri kuitwa Dr kutawaongezea 'ujiko'. Hivyo ujikomba wapewe ' vi Ph.D vya heshima' Wakati wengiwao utendaji wao wa kazi ni 'impontent'.
SHAME ON THEM.
 
Mbona hushangai Mwenyewe Obama ni holder wa Doctorate lakini mbona hujauliza kwanini hawaanzi na kiimbo cha Dr.? Au ndio kunya anye kuku akinya bata kaharisha?
 
Kikwete pia ni Luteni Kanali mstaafu, mbona hujaandika kwamba hilo nalo hawalitambui?
Afadhali umeweka alama ya kuuliza maana, wanajeshi(makamanda) walikataa kumpa kamisheni (yaani uafisa) kwa sababu hakukidhi masharti ya uafisa na hafai kuwa ofisa wa jeshi kwa sababu za fitina na unafiki kwa wenzie (kama mwanamke vile?).
 
Mbona hushangai Mwenyewe Obama ni holder wa Doctorate lakini mbona hujauliza kwanini hawaanzi na kiimbo cha Dr.? Au ndio kunya anye kuku akinya bata kaharisha?

Ni kweli Obama na mkewe wana doctorates (JD) za sheria kutoka Harvard Law school. Lakini hawajikwezi nazo. Huku bongo mtu akiwa na Advanced diploma kutoka Mbeya Referral Hospital usipomuita "dokta" anaweza kukununia kutwa nzima! Kuna mmoja nilikosea nikamtaja kama "Mr" mahali tulipokuwa naye kwenye kikao cha harusi, alitumia karibu dakika 10 kunisahihisha!
 
Ni kweli Obama na mkewe wana doctorates (LLD) za sheria kutoka Yale Law school. Lakini hawajikwezi nazo. Huku bongo mtu akiwa na Advanced diploma kutoka Mbeya Referral Hospital usipomuita "dokta" anaweza kukununia kutwa nzima! Kuna mmoja nilikosea nikamtaja kama "Mr" mahali tulipokuwa naye kwenye kikao cha harusi, alitumia karibu dakika 10 kunisahihisha!
Hata hivyo mkuu ulikuwa na bahati, wapenda sifa wa kibongo wanaweza kukununia hata mwaka mzima.
 
Ni kweli Obama na mkewe wana doctorates (LLD) za sheria kutoka Yale Law school. Lakini hawajikwezi nazo. Huku bongo mtu akiwa na Advanced diploma kutoka Mbeya Referral Hospital usipomuita "dokta" anaweza kukununia kutwa nzima! Kuna mmoja nilikosea nikamtaja kama "Mr" mahali tulipokuwa naye kwenye kikao cha harusi, alitumia karibu dakika 10 kunisahihisha!

Obama na mkewe wana LLD kutoka Yale? Una uhakika?
 
Afadhali umeweka alama ya kuuliza maana, wanajeshi(makamanda) walikataa kumpa kamisheni (yaani uafisa) kwa sababu hakukidhi masharti ya uafisa na hafai kuwa ofisa wa jeshi kwa sababu za fitina na unafiki kwa wenzie (kama mwanamke vile?).

That is beside the question. Which remains unanswered.

Halafu hujawatendea haki wanawake kwa kuleta habari ya kusadikisha watu kwamba fitina na unafiki ni mambo ya kike.
 
Una maanisha hata wakati wa Mtukufu mwenyeheri uchakachuaji ulikuwepo? Imebaki kuhoji jina kama kweli huyu tunaemuona na kumjua ndio mtoto hasa wa Chifu wa W.ak.were chif mrisho kikwete?

hii la kuwa kanali bila vigezo ni moja ya miujiza ya jk
 
Obama na mkewe wana LLD kutoka Yale? Una uhakika?

Obama na mkewe wana JD (Juris Doctor) kutoka Harvard Law School. Ni sawa na LLD, au vipi kuna tofauti? Poa mkuu, siyo Yale ni Harvard. Lakini point yangu ilikuwa kwamba wana doctorates lakini wako poa tu, hawashinikizi wala kushadidia kuitwa "Dr Obama". Jaribu kwa madokta wetu hapa uone watakavyokushushua kuwa "nipe heshima yangu! mie dokta bana!"
 
Nani kasema JK amewahi kuwa mwanafunzi Monduli?

Waulize wakuu wa majeshi amepata fast tracking kwa faida ya nani. Waulize CCM mfumo mzima wa "chama kushika hatamu" ulikuwa kwa faida ya nani.

Watanzania wamemchagua JK kwa wingi, kwa sababu wengi wetu hatuna utaratibu wa kuhoji, na si tu wengi hatujahoji kupandishana vyeo bila merit, mimi sijawahi kusikia a convinving case for Kikwetes achievements prior to becoming a candidate.

Hivi Kikwete alikuwa na merit gani ya kusema anaweza kuwa rais wa nchi maskini kama Tanzania?

Badala ya kuhoji kwa nini sisi kama jamii hatujahoji JK kukosa merit kabla, na kwa nini tumemchagua licha ya kukosa merit, na kuhoji mfumo mzima wa watu kupanda ngazi bila merit (rais wa pili Ally Hassan Mwinyi alishawahi kujiuzulu Uwaziri wa Mambo ya ndani kwa uzembe kimsingi, akaweza kurudi na kuwa rais hatujaliona hili kama tatizo)

Matatizo yetu hayajaanza na wala hayaishi kwa JK.

Kama tunatafuta suluhisho, tuulize maswali yenye kina cha zaidi ya JK.

Kama vile, ilikuwaje mtu aliyejiuzulu kwa uzembe kama Ally Hassan Mwinyi aweze kupewa nafasi ya kugombea urais? Tena chini ya uangalizi wa kipanga wenu JK Nyerere?

Ukiangalia maswali kama haya utaona huu upuuzi wa kupandishana tu kwa sababu "huyu mwenzetu", hata kama mtu kajiuzulu kwa uzembe, ulianza kabla Kikwete hata hajaingia serikalini.

Kwa hiyo ku focus kwa Kikwete kunaweza kuwa sawa kwa sababu yeye ni rais na yuko visible sana, lakini kuna matatizo yaliyo katika jamii nzima yaliyoanza kabla ya Kikwete na yenye kina kirefu kumshinda Kikwete.

Kikwete si sababu ya matatizo yetu.

Kikwete ni matokeo ya matatizo yetu.

Ukitaka kutatua tatizo kuangalia matokeo ni muhimu, lakini kuangalia sababu ni muhimu zaidi.

You have exhausted everything no more questions or opinions, thanks for your little time.
 
Udaktar wa falsafa kwa wenzetu ni kitu cha kawaida sana, wala hutasikia wakiji-boast kujiita Dr. Fulani. Kwa mfano, waziri wa zamani wa mambo ya nje Marekani Condolezza Rice ni dokta, lakini hata siku moja hutasikia hiyo kitu. Ni mtazamo tu
 
Hivi mnajua kuwa karibu maaskofu wote wa kanisa katoliki wana doctorates km JCD (Juris Canonici Doctor kama ile ya Slaa), DD (Doctor of Divinity), STD (Sacrae Theologiae Doctor), PhD na nyinginezo. Lakini hata siku moja hawatajwi kama madokta. Ni suala la unyenyekevu tu. Na hata Dr Slaa aliukumbuka "udokta" wake baada ya kuacha upadri, lakini sasa sina uhakika kama ataridhika tukimtaja tu kama "Bwana Slaa". Kumbe, nadhani, waswahili tunapenda kukwezwa. Natazama jinsi wahandisi wa bongo wanavyolazimisha majina yao yatanguliwe na neno Eng. Sijaona mahali pengine. Kwa hiyo hili la honorary doctorates za JK ni reflection ya jinsi sisi wabongo tulivyo, linawakilisha vizuri tabia ya wabongo.
 
Wengine utawasikia "My name is Dr. ..."

No, your name is not Dr., Sir. If anything your title or profession may be doctor.

Unless your parents named you "Doctor" or you have gone through the process of having doctor as your name, your name cannot be doctor.

I can understand someone saying "I'm doctor so and so". But the minute one says "My name is Dr. ..." I start to question the doctorate.
 
Hivi mnajua kuwa karibu maaskofu wote wa kanisa katoliki wana doctorates km JCD (Juris Canonici Doctor kama ile ya Slaa), DD (Doctor of Divinity), STD (Sacrae Theologiae Doctor), PhD na nyinginezo. Lakini hata siku moja hawatajwi kama madokta. Ni suala la unyenyekevu tu. Na hata Dr Slaa aliukumbuka "udokta" wake baada ya kuacha upadri, lakini sasa sina uhakika kama ataridhika tukimtaja tu kama "Bwana Slaa". Kumbe, nadhani, waswahili tunapenda kukwezwa. Natazama jinsi wahandisi wa bongo wanavyolazimisha majina yao yatanguliwe na neno Eng. Sijaona mahali pengine. Kwa hiyo hili la honorary doctorates za JK ni reflection ya jinsi sisi wabongo tulivyo, linawakilisha vizuri tabia ya wabongo.

Sasa hivi ashakua mwanasi- hasa ukimuita hivyo mtagombana.
 
Nakuelewa sana ndugu.
Nilifanya kazi na profesa mmoja kwa miaka miwili (sikujua kwamba ni profesa). Kuna siku nikawa nasoma presentation yake online ndipo nilipojua kuwa ni prof. Nilishangaa sana (kibongobongo) kwa sababu alikuwa 'humble' mno, wala huwezi kumdhania kabisa, wala hajisikii wala kujisifia. Penye shida anaomba kueleweshwa kama ilivyo kwa wengine. Sasa sisi wabongo, kama unavyosema, hata civil au mechanical technician (mafundi mchundo) lazima ajiite engineer, kama akina Eng. Gerson Lwenge, Eng. Stella Manyanya n.k. Tunahitaji kubadilika.
 
Mbona hushangai Mwenyewe Obama ni holder wa Doctorate lakini mbona hujauliza kwanini hawaanzi na kiimbo cha Dr.? Au ndio kunya anye kuku akinya bata kaharisha?

na ndio mana yule anaitwa Obama na huyu ni Kikwete,means hawafanani hawa kwa tabia.kichwa chetu kinapenda sifa hata kma ni za kijinga.
 
Hapa kwetu Tanzania,mtu asipokuwa addressed kama Prof au Dr. lazima 'amaind' wkt watu wengine ni Dr. na hawalifanyi hilo kama Jina mfano mtu anaitwa Carlos Junior (Dr) ila sisi inakuwa Dr. Carlos Junior
 
Back
Top Bottom