CIF ya gari vs calculator ya TRA

CIF ya gari vs calculator ya TRA

Joyce wohwoh

Member
Joined
Sep 17, 2021
Posts
80
Reaction score
185
Naomba kuuliza nko kwenye process za mwisho kuagiza gari yangu japan. SWALI.

CIF ya gari ni kubwa kuliko estimation kodi ya TRA.mfano.CIF ya gari MIL 7.KODI TRA MIL 4.5.JE TRA watatumia hiyohiyo 4.5mil au itsongezeka?

Ipi I atakuwa iwe kubwa?

Cif ya gari au TRA culculator?
 
Mfano: CIF ya TRA ni $1800, na ushuru ni 4.2mil.

CIF ya gari ulilonunua ni $2500.

TRA wataaacha CIF yao, watatumia hiyo uliyonunulia gari ambayo ni kubwa kukokotoa ushuru ambao utakuwa mkubwa kuliko huo unaoonekana kwenye kikokotozi chao.
Umezidi kunichanganya kabisa,what I know kutoka kwa wadau humu,kuna bei ya gari ambayo unaipata kutoka kwa kampuni unayotaka kununua,then unaingia kwenye Web ya TRA kwenye culculator kuangalia kodi elekezi ya hiyo gari.

Uliponichanga mtu pori ni hapa kwenye mfano wako,CIF ya TRA ni 1800,na ushuru ni 4.2mil.halafu tena CIF ya gari ulonunua ni $2500.
 
Sawa, twende taratibu. Utaelewa tu. Iko hivi, TRA wana bei elekezi kwa kila gari. Ukiangalia kwenye kikokotozi chao utaona imeandikwa 'custom value CIF'.

Kwenye ununuzi wa gari huwa kuna gharama tofauti kama vile gari pekee (FOB), inspection, insurance, na freight. Mfano gari x, price (FOB) yake ni $1500, inspection $300, insurance $50, na freight $1800.

Ukijumlisha vyote hivi unapata $2650. Hii sasa ndio inaitwa CIF kwa upande wa hayo makampuni yanayouza magari kama Beforward. Ukiangalia kwenye website zao utaona wamekuwekea pale CIF ya gari X ni $3000 (mfano).

Kwa ufupi ni kuwa TRA wana bei elekezi yao kwa kila gari, na makampuni yanayouza magari nayo yana CIF zao kwa kila gari wanalouza.

Kila gari hupungua thamani kadiri miaka inavyoenda mbele. Kwa hiyo, TRA wana bei elekezi yao kwa kila gari. Mfano, gari X ya mwaka Y yenye sifa ABC, thamani yake ni $2600 (mfano), ushuru wake ni 4.2mil.

Endapo wewe utanunua gari kama hilo kwa thamani ya juu (mfano $4000) kuliko bei ekekezi ya TRA (ambayo ni $2600), basi hiyo thamani ya juu ya gari ulilonunua ndio itakayotumika kukokotoa upya huo ushuru ambao sasa utakuwa zaidi ya 4.2mil.

Endapo CIF ya gari huko Japan itakuwa na sawa na ya TRA (mfano $2600) au chini ya bei elekezi ya TRA (mfano $1900), basi utalipa ushuru huo unaoonekana kwenye kikokotozi chao.

Hadi hapo ninadhani utakuwa umeelewa.

Mimi ni mwalimu, sasa ninakupa zoezi. Ingia kwenye website ya Beforward, tafuta gari unalotaka kisha angalia CIF yake. Kisha ingia kwenye kikokotoo cha TRA na uingize sifa za hiyo gari (I assume you know how to enter the car's details) na baada ya kubofya 'calculate', angalia custom value CIF ni dollar ngapi. Kisha linganisha CIF ya TRA na CIF ya Beforward.

Ipi kubwa?
 
Nashukuru sana hapa sasa nimeelewa haswaa.hatimaye somo limeeleweka ubarikiwe sana.
 
Mimi ni mwalimu, sasa ninakupa zoezi. Ingia kwenye website ya Beforward, tafuta gari unalotaka kisha angalia CIF yake. Kisha ingia kwenye kikokotoo cha TRA na uingize sifa za hiyo gari (I assume you know how to enter the car's details) na baada ya kubofya 'calculate', angalia custom value CIF ni dollar ngapi.

Kisha linganisha CIF ya TRA na CIF ya Beforward.

Nimeingia mwalimu wangu nimepata CIF ya TRA kubwa zaidi ya CIF ya Beforward.

Hakuna maujanja wanafanyaga,ama niwaambie Beforward waniandikie CIF nnayotaka.maana budget imebana balaa.
 
Sawa, twende taratibu. Utaelewa tu. Iko hivi, TRA wana bei elekezi kwa kila gari. Ukiangalia kwenye kikokotozi chao utaona imeandikwa 'custom value CIF'.

Kwenye ununuzi wa gari huwa kuna gharama tofauti kama vile gari pekee (FOB), inspection, insurance, na freight. Mfano gari x, price (FOB) yake ni $1500, inspection $300, insurance $50, na freight $1800.

Ukijumlisha vyote hivi unapata $2650. Hii sasa ndio inaitwa CIF kwa upande wa hayo makampuni yanayouza magari kama Beforward. Ukiangalia kwenye website zao utaona wamekuwekea pale CIF ya gari X ni $3000 (mfano).

Kwa ufupi ni kuwa TRA wana bei elekezi yao kwa kila gari, na makampuni yanayouza magari nayo yana CIF zao kwa kila gari wanalouza.

Kila gari hupungua thamani kadiri miaka inavyoenda mbele. Kwa hiyo, TRA wana bei elekezi yao kwa kila gari. Mfano, gari X ya mwaka Y yenye sifa ABC, thamani yake ni $2600 (mfano), ushuru wake ni 4.2mil.

Endapo wewe utanunua gari kama hilo kwa thamani ya juu (mfano $4000) kuliko bei ekekezi ya TRA (ambayo ni $2600), basi hiyo thamani ya juu ya gari ulilonunua ndio itakayotumika kukokotoa upya huo ushuru ambao sasa utakuwa zaidi ya 4.2mil.

Endapo CIF ya gari huko Japan itakuwa na sawa na ya TRA (mfano $2600) au chini ya bei elekezi ya TRA (mfano $1900), basi utalipa ushuru huo unaoonekana kwenye kikokotozi chao.

Hadi hapo ninadhani utakuwa umeelewa.

Mimi ni mwalimu, sasa ninakupa zoezi. Ingia kwenye website ya Beforward, tafuta gari unalotaka kisha angalia CIF yake. Kisha ingia kwenye kikokotoo cha TRA na uingize sifa za hiyo gari (I assume you know how to enter the car's details) na baada ya kubofya 'calculate', angalia custom value CIF ni dollar ngapi. Kisha linganisha CIF ya TRA na CIF ya Beforward.

Ipi kubwa?

Saafi sana umeeleza kila kitu

Kuna gari moja inaitwa mazda Atenza 2013

What’s wrong with TRA calculator mbona ushuru uko chini sana around 6.2mls mpk huwa napata mashaka
 
Pia huwa kuna Nissan Teanna. Hizi ushuru huwa uko juu kuliko CIF ya gari. 😆😆
 
Saafi sana umeeleza kila kitu

Kuna gari moja inaitwa mazda Atenza 2013

What’s wrong with TRA calculator mbona ushuru uko chini sana around 6.2mls mpk huwa napata mashaka
Cheki ushuru wa Nissan Xtrail 2018 NT32 Vs Mercedes Benz C Class 2011, C200: zote Cc 1,500 - 2,000: Utaona maajabu
 
Mfano: CIF ya TRA ni $1800, na ushuru ni 4.2mil.

CIF ya gari ulilonunua ni $2500.

TRA wataaacha CIF yao, watatumia hiyo uliyonunulia gari ambayo ni kubwa kukokotoa ushuru ambao utakuwa mkubwa kuliko huo unaoonekana kwenye kikokotozi chao.
TRA Wana CIF,au import tax?
 
TRA Wana CIF,au import tax?
Import taxes hupatikana mwishoni baada ya gharama nyingine kuwa zimejumuishwa.

Customs value CIF huonesha thamani ya mzigo wako ili pamoja na mambo mengine, waweze kukadirisha kodi utakayolipa.

TRA ndio wanayo ambayo huwa ni kama reference point (huwa ninaiita bei elekezi) inayoonesha thamani ya gari fulani kwa wakati huo. Mfano, gari X yenye sifa ABC, thamani yake ni hii na total import taxes ni kiasi hiki.

Endapo thamani ya gari utakaloagiza itakuwa juu zaidi ya tathmini yao (TRA), utatozwa total import taxes zaidi ya ile inayoonekana kwenye calculator.
 
Safi sana,sasa kama CIF ya gari ni Tsh. 4,500,000 hapo TRA wataacha hiyo 4,500,00 na kuchukua hiyo TOTAL TAXES TSH.7,742,827+7,742,827. Badala ya TSH.7,742,827+4,500,00.
Kama nimekosea naomba kurekebishwa[emoji120][emoji120]

Asee naona bado hujaelewa kabisa

CIF hulipi TRA,unalipa ulikoagizia gari

TRA wanatumia CIF ku-calculate kodi utakayolipa

Sasa wana wana CIF elekezi kwa kila gari ambayo itatumika kupata iyo kodi

Ndo hyo hapo unayoina.

Sasa CIF uliyoagiza japan ikiwa kubwa kuliko yao elekezi waliotumia ku-calculate kodi,then watatumia CIF yako wew na kuacha ile yao elekezi ku-calculate kodi

Hivo kodi zitapishana kidogo na iliyopo kene calculator ambayo ile waliipata kutokana na ile CIF elekezi
 
Back
Top Bottom