Umezidi kunichanganya kabisa,what I know kutoka kwa wadau humu,kuna bei ya gari ambayo unaipata kutoka kwa kampuni unayotaka kununua,then unaingia kwenye Web ya TRA kwenye culculator kuangalia kodi elekezi ya hiyo gari.
Uliponichanga mtu pori ni hapa kwenye mfano wako,CIF ya TRA ni 1800,na ushuru ni 4.2mil.halafu tena CIF ya gari ulonunua ni $2500.
Sawa, twende taratibu. Utaelewa tu. Iko hivi, TRA wana bei elekezi kwa kila gari. Ukiangalia kwenye kikokotozi chao utaona imeandikwa 'custom value CIF'.
Kwenye ununuzi wa gari huwa kuna gharama tofauti kama vile gari pekee (FOB), inspection, insurance, na freight. Mfano gari x, price (FOB) yake ni $1500, inspection $300, insurance $50, na freight $1800.
Ukijumlisha vyote hivi unapata $2650. Hii sasa ndio inaitwa CIF kwa upande wa hayo makampuni yanayouza magari kama Beforward. Ukiangalia kwenye website zao utaona wamekuwekea pale CIF ya gari X ni $3000 (mfano).
Kwa ufupi ni kuwa TRA wana bei elekezi yao kwa kila gari, na makampuni yanayouza magari nayo yana CIF zao kwa kila gari wanalouza.
Kila gari hupungua thamani kadiri miaka inavyoenda mbele. Kwa hiyo, TRA wana bei elekezi yao kwa kila gari. Mfano, gari X ya mwaka Y yenye sifa ABC, thamani yake ni $2600 (mfano), ushuru wake ni 4.2mil.
Endapo wewe utanunua gari kama hilo kwa thamani ya juu (mfano $4000) kuliko bei ekekezi ya TRA (ambayo ni $2600), basi hiyo thamani ya juu ya gari ulilonunua ndio itakayotumika kukokotoa upya huo ushuru ambao sasa utakuwa zaidi ya 4.2mil.
Endapo CIF ya gari huko Japan itakuwa na sawa na ya TRA (mfano $2600) au chini ya bei elekezi ya TRA (mfano $1900), basi utalipa ushuru huo unaoonekana kwenye kikokotozi chao.
Hadi hapo ninadhani utakuwa umeelewa.
Mimi ni mwalimu, sasa ninakupa zoezi. Ingia kwenye website ya Beforward, tafuta gari unalotaka kisha angalia CIF yake. Kisha ingia kwenye kikokotoo cha TRA na uingize sifa za hiyo gari (I assume you know how to enter the car's details) na baada ya kubofya 'calculate', angalia custom value CIF ni dollar ngapi. Kisha linganisha CIF ya TRA na CIF ya Beforward.
Ipi kubwa?