Yoyo Zhou
Senior Member
- Jun 16, 2020
- 126
- 215
Maonyesho ya 7 ya Kimataifa ya Uagizaji Bidhaa ya China (CIIE) yatafanyika hivi karibuni mjini Shanghai. Ili kutekeleza kihalisi hatua za ushirikiano zilizofikiwa kwenye Mkutano wa Kilele wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC) wa mwaka 2024, eneo maalum la kuonesha bidhaa za kilimo za Afrika katika awamu hii ya CIIE litaongezwa.
Katika miaka ya hivi karibuni, maonyesho haya yametoa mchango muhimu kwa bidhaa za kilimo za Afrika mbazo zimepata umaarufu katika soko la China.Mwezi Septemba mwaka huu, nyama ya kondoo kutoka Madagascar ilianza kuuzwa katika soko la China, ikiwa ni mara ya kwanza kwa China kuagiza bidhaa za kondoo kutoka Afrika.
Nyama ya kondoo ya Madagascar ilifanikiwa kuingia kwenye soko la China kutokana na CIIE, kwani kwenye maonesho ya mwaka jana, China na Madagascar zilisaini makubaliano ya kuruhusu nyama ya kondoo kutoka Madagascar kuuzwa kwenye soko la China.
Licha ya nyama ya kondoo ya Madagascar, bidhaa nyingi za kilimo za nchi za Afrika zimekuwa na umaarufu nchini China kupitia CIIE katika miaka ya hivi karibuni.
Bidhaa mbalimbali za kilimo za Afrika zikiwemo matunda kutoka Afrika Kusini, kahawa ya Ethiopia, pilipili ya Rwanda, korosho za Tanzania, asali ya Zambia, ambazo awali zilioneshwa kwenye CIIE, sasa ni maarufu sana katika soko la China. Tangu awamu ya kwanza ya CIIE, mauzo ya bidhaa za kilimo za Afrika nchini China yameongezeka kwa miaka saba mfululizo.
Takwimu zinaonesha kuwa katika miezi saba ya kwanza ya mwaka huu, China iliagiza bidhaa za kilimo kutoka Afrika zenye thamani ya dola bilioni 3.6 za Kimarekani, ambalo ni ongezeko la asilimia 7.2 ikilinganishwa na mwaka jana kipindi kama hiki.
Wakati Mkutano wa Kilele wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika wa mwaka 2024 ulipofanyika Beijing Septemba mwaka huu, Rais Xi Jinping wa China alitangaza kwamba China imeamua kusamehe ushuru wa fordha kwa bidhaa za nchi zote zilizokuwa nyuma zaidi kimaendeleo ambazo zina uhusiano wa kibalozi na China, zikiwemo nchi 33 za Afrika. Pia kwenye mkutano huo, China ilisaini makubaliano mengi na nchi za Afrika kuhusu mauzo ya bidhaa za kilimo nchini China:
yakiwemo makubaliano na Zimbabwe kuhusu mauzo ya parachichi nchini China, makubaliano na Zambia kuhusu mauzo ya soya, na makubaliano na Msumbiji kuhusu mauzo ya mbaazi, macadamia na korosho.
Bidhaa hizi za kilimo za Afrika zinatarajiwa kuonekana kwenye CIIE ya mwaka huu na kuwa nyota ya kesho katika soko la China.
Katika miaka ya hivi karibuni, kutokana na China kufungua mlango zaidi kwa Afrika, bidhaa nyingi zaidi za kilimo za Afrika zimefanikiwa kuingia kwenye soko la China.
Hadi mwishoni mwa Agosti mwaka huu, China imesaini Makubaliano 22 na nchi 14 za Afrika kuhusu kuuza bidhaa za kilimo katika soko la China. Licha ya hayo, majukwaa ya kuhimiza biashara yaliyoanzishwa na China ikiwemo CIIE yamesaidia bidhaa za kilimo za Afrika kuunganishwa moja kwa moja na soko la China, na kupata umaarufu kwa haraka nchini China.