solowisonzo
Member
- Feb 1, 2014
- 32
- 24
Wadau mi nimechaguliwa st. Joseph- civil engineering. Wakati nafanya application kulikuwa na contradiction miongon mwa walionishauri. Wengine wanasema sio pazuri na wengine wanasema ni pazuri. Wengine wakaniambia civil haina ajira bora nichague education bt civil ndo ilikuwa ndoto zangu. Naomba kwa anaekifahamu vizuri hiki chuo na hyo kozi ya civil ni pazuri?
karibu bwana mdogo,maelezo yangu ni mengi mno lakini tafadhali yasome yote hii ni kwaajili ya kufukia mashimo ya wanaopotosha kuwa st.joseph ni chuo cha fm6 failures yatakusaidia sana kuclear doubts zako nyingi
mimi nipo pale tangu mwaka 2012,ni kweli wanafunzi wengi wanaosoma pale wana ufaulu wa pts 14,15,16 na 17(hiz n points za zamani)
hakuna chuo chochote kinachojipangia marks kwa ajili ya kudahili wanafunzi wa degree bila kuwa approved na TCU,kwaiyo kulingana na mashariti ya tcu minimum requirements zinazotakiwa kwa mwanafunzi kusoma degree ni principal(E) mbili,ambapo kwa hesabu ya haraka ni kitu ambacho hakiwezekani kwa mtu mwenye dvsn four ya pts 18 kuwa na izo principal pass mbili kwaiyo ni upotoshaji tena udhalilishaji kwa taasisi ya Tcu kuisingizia kuwa inadahili wanafunzi wenye dvsn 4 na kuwapeleka st.joseph,sababu wanafunzi wa st.joseph hudahiliwa na tcu yenyewe
Tcu ndio walioanzisha utaratibu wa pre entry na kuviruhusu vyuo vyote vinavyotaka kuendesha programu hiyo vidahali wanafunzi wenye ufaulu usio na principal mbili lakini angalau wawe na principal moja na subsiduary moja na program iendeshwe kwa kipindi cha miezi mitatu kisha chuo kitume majina tcu kwa ajili ya wanafunzi hao kuwa approved na kuruhusiwa kusoma degree,kwaiyo aliyedai kuwa st.joseph kuna wanafunzi wenye S flat fm6 amelipotosha jukwaa na tena ameidhalilisha tcu
Mwaka 2012 tcu iliufuta utaratibu wa pre entry ya miezi mitatu na kuanzisha utaratibu wa post fm 6 certificate ambapo badala ya wanafunzi wasio na principal 2 kusoma miezi mitatu,ilitakiwa wasome mwaka mzima na kisha baada ya hapo wanapewa cheti then wanaopt kuendelea kusoma degree palepale st.joseph ama wanajiunga na vyuo vingine kupitia central admission,na kuthibitisha hilo wanafunzi wa batch ya 1 kupitia program walidahiliwa ktk vyuo vya MZUMBE,NIT,MUST,SAUT na pia kuna wanafunzi waliosoma hiyo program mwaka huu wamedahiliwa UDSM,DIT,ARDHI na SUA kwaiyo wale mnaodai eti st.joseph ni chuo cha kichochoroni naomben kuanzia sasa mtambue kuwa udsm,dit,ardhi,sua,mist na mzumbe navyo ni vyuo vya kata kwa sababu wamekubali kudahili makapi na matakataka toka st.joseph ambao walifeli fm6
kuhusu ada kulinganisha st.joseph na saut siyo haki,sababu saut ina ada ndogo kuliko vyuo vyote vya serikali ukiondoa udom,hii ni sababu ni chuo cha muda mrefu na kina ruzuku kubwa toka serikalini,naomba tulinganishe ada ya st.joseph na ada ya st.john pamoja na tumaini ambavyo navyo ni vyuo vya private,ada ya education st.john ni 1.6 mil,ada ya education tumain 1.6 mil,ada ya education kampala n 2.2 mil,ada ya education st.joseph ni 1.75 mil,sasa unapata wapi ujasiri wa kuwaita wahindi matapeli wakati wana ada sawa na vyuo vingine vya private ambavyo ni vya wazawa???
Sawa ada ya st.joseph kwa engineering ni 2.75 mil,hii ni kwa sababu engineering n kozi zinazodemand practical na facilities zenye gharama kubwa na hata walimu pia wanademand mishahara mikubwa na ikumbukwe kuwa st.joseph ni chuo pekee cha private kwa engineering tz,saut wameanzisha civil na electrical mwaka jana na wanachukua wanafunzi wachache wasiozid 40,ili kukwepa gharama za kuendesha koz,maana yake ata tumaini leo wakianzisha engineering ada yao itakuwa kati ya 2.5-3.0 mil
All in all dogo karibu,nimeongea mengi lakin changamoto apa zipo,sheria ni kali,kwa muhindi no discipline no academic perfomance,ni pindi kuanzia asubuh mpaka saa tisa,na ole wako attendance yako darasan ikiwa chin ya 85% hufanyi mtihan wa semester,kila mwezi kuna CAT,assignments na mitihan ni mingi mno,hurusiwi kuvaa sendoz maeneo ya chuo,kama wewe ni sharobaro apa utapata taabu ni mwiko kuvaa kihuni ukiwa chuoni,then nakushauri ufungue akaunti exim bank lasivyo bumu utalisikia kwenye bomba