biabia
Senior Member
- Nov 18, 2023
- 192
- 242
Iko hivi, wathailand 12 wameachiwa pamoja na waisrael 12 ikiwa ni makubaliano yaliyofanyika Kati ya Israel na Hamas. Sasa tujadili hill jambo. Clemence Mtenga sasa ni marehemu, amefia Gaza. Mpaka sasa maelezo hayajanyooshwa kuwa kafa kwa kombora, au gunshot etc. Vyombo vya habari vinavyojulikana hapa nchini hawakutangaza kuhusu hawa Vijana waliotekwa hata katika tukio la bwana Clemence kufariki. Katika pita pita Zangu mtandaoni niliona kuwa serikali ya Thailand ilifanya makubaliano na Iran ili wananchi wao waachiwe. Lakini bongo kuna watu wengi hawana hata taarifa kuwa kuna Mtanzania kauwawa. Nina unpopular opinion, mimi nadhani ubaguzi wa rangi na udini umefanya hili jambo lisichukuliwe kwa uzito na kusababisha kifo. Inasemekana wapalestina waarabu ni wabaguzi wa rangi kwa black Palestinians....inawezekana Hamas wamemuua kwasababu his, au alishikiliwa na raia na katika missle akawa mhanga. Pili mimi naamini Jina lake lingekuwa Rashid Mtenga, tungekuwa nae....ila kwa kuwa anaonekana sio part ya Islam umma, wala hakuna alietilia maanani kwanzia viongozi wa dini waliotaka kuandamana mpaka serikalini.