PostGE2025 Clemence Mwandambo akamatwa (tena) na Polisi kwa tuhuma za kijinai

PostGE2025 Clemence Mwandambo akamatwa (tena) na Polisi kwa tuhuma za kijinai

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections

Troll JF

Platinum Member
Joined
Feb 6, 2015
Posts
10,592
Reaction score
15,404
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linamshikilia Mwalimu wa Shule ya Awali ya "Saint Clemence" ndugu Clemence Kenani Mwandambo, mkazi wa Uzunguni "A" Jijini Mbeya kwa tuhuma za kuchapisha na kusambaza taarifa za uongo pamoja na kukashfu imani za dini zingine.

Mtuhumiwa alikamatwa mnamo Disemba 29, 2025 saa 4:00 asubuhi maeneo ya Uzunguni Jijini Mbeya akichapisha na kusambaza taarifa za uongo pamoja na kukashfu imani ya dini ya kiislamu na kikristu kupitia akaunti zake za mitandao ya kijamii.

Upelelezi unakamilishwa ili hatua nyingine za kisheria ziweze kuchukuliwa dhidi yake.

Soma Pia: Jeshi la Polisi Mbeya lakiri kumshikilia Clemence Mwandambo kwa tuhuma za Uchochezi
5fa0c094-f6c2-474d-9aca-4aa362a1838b.jpeg
 
...'Kusambaza taarifa za uongo'...
Siku hizi Polisi wamekuwa ndiyo mahakama ya kuhukumu watu sasa?!

Mtuhumiwa mtamthibitishaje kusambaza taarifa za uongo hata kabla hamjamfikisha mahakamani?

Wanaothibitisha kuwa hizo ni taarifa za uongo ama za kweli ni mahakama pekee!

Mandate yenu ni kukamata na kumshitaki mtuhumiwa na kumuombea kibali cha kesi kwa Dpp
Kwa taarifa yenu hii Mwandambo kawa mkosa tayari kabla hata hajafikishwa mahakanani!

What for?
 
Ni hatari ni zero brain
 
Katika hali kama hii hili jeshi unalisogeza vipi kwa wananchi?

Kwa hali hii Waziri Simbachawene ana mtihani mkubwa mno kwendana na hiyo dhamira ya kufanya mabadiliko ndani ya jeshi la polisi ili kulisogeza jeshi hilo karibu na wananchi kama chombo muhimu kwao.
Huyo Simbachaweni unamuamini?
 
Eti upelelezi unaendelea..

Ni wapumbavu pekee wanamkamata mtu upelelezi ukiwa haujakamilika.

Hawa ni vibaka ndani ya sare , watueleze upelelezi wa tukio la mzee Kibao, Mdude, Soka, Chaula, Polepole wamefikia wapi ndio nitawaamini.
 
Back
Top Bottom