SAYVILLE
JF-Expert Member
- Mar 25, 2010
- 7,895
- 12,975
We jamaa pamoja na kwamba unachezea utopolo nimekupigania sana ili timu yako isilalie fursa zinazokujia. Niliwahi kusema ukipunguza wenge wewe ndiyo unaenda kuchukua mikoba ya kina Samatta na kuibeba Taifa Stars kwa miaka 5 ijayo. Utulivu wako wa sasa unaonyesha kile nilichokiona.
Wydad wameonyesha nia ya dhati ya kukutaka ila klabu yako inakubania. Usidhani wanafanya hivyo kwa faida yako. Watakupa mifano ya kina Miquisonne, Msuva na Chama ila hawakupi mifano ya kina Percy Tau, Himid Mao, Mayele na wengine ambao wamefanikiwa huko huko Uarabuni. Hii nchi tuna historia ya kubania watu fursa za nje, kamuulize Sunday Manara kama sikosei tena hiyo Yanga ndiyo kabisa ina historia mbaya. Kina Nonda Shabani walitoroka na klabu haikupata hata sumni maana angesema afuate utaratibu asingeruhusiwa.
Wakikwambia eti unaenda kufunga magoli 2 fainali ya CAFCL na thamani yako itapanda, waambie waweke nyumba zao za urithi mechi ya Jumamosi na Al Hilal kama kweli wanaamini hivyo. Usikubali wakupumbaze na vikiki vya kuvamia dukani kwako kununua mashati, siku zote adui ya binadamu ni mtu wake wa karibu.
Wydad miezi michache ijayo anaenda kucheza Club World Cup. Anakutana hatua ya makundi na Juventus na Man City. Imagine ufunge goli kama lile ulilowapiga Mazembe, unadhani fursa kiasi gani zitafunguka?
Hata kama unadhani hao kina Hersi wamekulea na kukukuza kiasi gani au unadhani wazee wa Yanga ndiyo wamekutengeneza (labda kama hili lina ukweli), ifike wakati ujisimamie kama mwanaume. Kuna wachezaji wengi wameviendekeza hivi vilabu wakaishia kustaafu kwa fedheha.
Muite Meneja na Wakala wako, muite mezani Hersi mwambie ukweli kwamba unashukuru hapo alipokufikisha ila hii fursa hautaki kuiacha. Akikataa kukusikiliza utakuwa umejua rangi halisi ya bosi wako ila usikae kifalafala.
Yangu ni hayo tu.