Clement Mzize usiwe mjinga, pigania maslahi yako!

Biashara ya mpira siyo ya utumwa. Mchezaji ulimpata bure unakataa vipi hata kukaa mezani kumsikiliza mtu anayetaka kumnunua kwa zaidi ya milioni 500?

Kuna nini nyuma ya pazia mnachotaka kisijulikane?
Nenda kausome huo Mkataba wao
 
We jamaa pamoja na kwamba unachezea utopolo nimekupigania sana ili timu yako isilalie fursa zinazokujia. Niliwahi kusema ukipunguza wenge wewe ndiyo unaenda kuchukua mikoba ya kina Samatta na kuibeba Taifa Stars kwa miaka 5 ijayo. Utulivu wako wa sasa unaonyesha kile nilichokiona.

Wydad wameonyesha nia ya dhati ya kukutaka ila klabu yako inakubania. Usidhani wanafanya hivyo kwa faida yako. Watakupa mifano ya kina Miquisonne, Msuva na Chama ila hawakupi mifano ya kina Percy Tau, Himid Mao, Mayele na wengine ambao wamefanikiwa huko huko Uarabuni. Hii nchi tuna historia ya kubania watu fursa za nje, kamuulize Sunday Manara kama sikosei tena hiyo Yanga ndiyo kabisa ina historia mbaya. Kina Nonda Shabani walitoroka na klabu haikupata hata sumni maana angesema afuate utaratibu asingeruhusiwa.

Wakikwambia eti unaenda kufunga magoli 2 fainali ya CAFCL na thamani yako itapanda, waambie waweke nyumba zao za urithi mechi ya Jumamosi na Al Hilal kama kweli wanaamini hivyo. Usikubali wakupumbaze na vikiki vya kuvamia dukani kwako kununua mashati, siku zote adui ya binadamu ni mtu wake wa karibu.

Wydad miezi michache ijayo anaenda kucheza Club World Cup. Anakutana hatua ya makundi na Juventus na Man City. Imagine ufunge goli kama lile ulilowapiga Mazembe, unadhani fursa kiasi gani zitafunguka?

Hata kama unadhani hao kina Hersi wamekulea na kukukuza kiasi gani au unadhani wazee wa Yanga ndiyo wamekutengeneza (labda kama hili lina ukweli), ifike wakati ujisimamie kama mwanaume. Kuna wachezaji wengi wameviendekeza hivi vilabu wakaishia kustaafu kwa fedheha.

Muite Meneja na Wakala wako, muite mezani Hersi mwambie ukweli kwamba unashukuru hapo alipokufikisha ila hii fursa hautaki kuiacha. Akikataa kukusikiliza utakuwa umejua rangi halisi ya bosi wako ila usikae kifalafala.

Yangu ni hayo tu.
Kwaiyo unataka auzwe sasa hivi na timu Iko kwenye harakati za kufuzu robo fainali? Utawatafutia replacement yake kwa muda huu kwenye hili dirisha? Unadhani vilabu vinauza tu wachezaji kiholela bila kuangalia mazingira yaliyopo,,kauzeni na nyie wa kwenu kina mutale mmeshindwa nini!
 
Narudia tena feisali analipwa 16m mzinze analipwa 7m, feitoto analipwa pesa mara 2 ya mzize akiwa na kipengele kinachosema akifikisha magoli 10 anapewa 10m.

Huna unachokijua
Huna unachokijua
Huna unachokijua utopolo mkubwa ww
Acha porojo weka mkataba hapa
 
Mzize anamiaka 21 ,
swali ni
  • je ataweza kupambania namba hapo wydad..?
  • Unakumbuka samatta wakati anatoka TP Mazembe alikuwa ameachive nini kwenye ligi ya mabingwa
 
Feisali analipwa hela mara 2 ya hela anayolipwa mzinze hapo yanga, feisal kachukua signing on fee zaidi ya m400, feisal kapewa nyumba ya gorofa moja na range rover mpya ya kutembelea.
Acha Kujiachia Kiasi Hiki Utafedheheka
 
We jamaa pamoja na kwamba unachezea utopolo nimekupigania sana ili timu yako isilalie fursa zinazokujia. Niliwahi kusema ukipunguza wenge wewe ndiyo unaenda kuchukua mikoba ya kina Samatta na kuibeba Taifa Stars kwa miaka 5 ijayo. Utulivu wako wa sasa unaonyesha kile nilichokiona.

Wydad wameonyesha nia ya dhati ya kukutaka ila klabu yako inakubania. Usidhani wanafanya hivyo kwa faida yako. Watakupa mifano ya kina Miquisonne, Msuva na Chama ila hawakupi mifano ya kina Percy Tau, Himid Mao, Mayele na wengine ambao wamefanikiwa huko huko Uarabuni. Hii nchi tuna historia ya kubania watu fursa za nje, kamuulize Sunday Manara kama sikosei tena hiyo Yanga ndiyo kabisa ina historia mbaya. Kina Nonda Shabani walitoroka na klabu haikupata hata sumni maana angesema afuate utaratibu asingeruhusiwa.

Wakikwambia eti unaenda kufunga magoli 2 fainali ya CAFCL na thamani yako itapanda, waambie waweke nyumba zao za urithi mechi ya Jumamosi na Al Hilal kama kweli wanaamini hivyo. Usikubali wakupumbaze na vikiki vya kuvamia dukani kwako kununua mashati, siku zote adui ya binadamu ni mtu wake wa karibu.

Wydad miezi michache ijayo anaenda kucheza Club World Cup. Anakutana hatua ya makundi na Juventus na Man City. Imagine ufunge goli kama lile ulilowapiga Mazembe, unadhani fursa kiasi gani zitafunguka?

Hata kama unadhani hao kina Hersi wamekulea na kukukuza kiasi gani au unadhani wazee wa Yanga ndiyo wamekutengeneza (labda kama hili lina ukweli), ifike wakati ujisimamie kama mwanaume. Kuna wachezaji wengi wameviendekeza hivi vilabu wakaishia kustaafu kwa fedheha.

Muite Meneja na Wakala wako, muite mezani Hersi mwambie ukweli kwamba unashukuru hapo alipokufikisha ila hii fursa hautaki kuiacha. Akikataa kukusikiliza utakuwa umejua rangi halisi ya bosi wako ila usikae kifalafala.

Yangu ni hayo tu.
Acha pumba wewe; unaingiaje kwenye maisha yake? Unajua plani zake? Ulikuwa wapi kumshauri hadi amefanikiwa ndipo unaleta kimbelemebele? Ungeaza kumshauri wakati bado ni dereva wa boda boda.

Utakuwa ni kati ya wanaoparamia embe lolote linaloning'inia kwenya tawi la chini hata kabla embe hilo hailjaiva.
 
Back
Top Bottom