Clement Mzize usiwe mjinga, pigania maslahi yako!

Lakini Yanga nao wauze wachezaji na siyo kuwakomoa kwa mikataba migumu,mwisho wa siku Wydad wakiona wanamkosa watajaza hiyo nafasi na asisajiliwe tena,pia kuna kushuka kiwango au kocha akibadilishwa unaweza kukaa benchi hadi ukasahaulika.
 
Yanga watamuuza kwa kuangalia mahitaji yao ya kipindi icho na sio kupangiwa na mtu yoyote yule,,unapouza lazima uangalie pia na replacement yake atakuwa nani sio unauza tu ilimradi umeuza,,dirisha hili kupata mchezaji mzuri ni vigumu na yanga Iko CCL ikipigania nafasi nyie mnakuja na habari zenu za ajabu ajabu,,kama ni ofa wasubili dirisha kubwa mwisho wa msimu ndio waisikilize sio sasa!
 
Muite Meneja na Wakala wako, muite mezani Hersi mwambie ukweli kwamba unashukuru hapo alipokufikisha ila hii fursa hautaki kuiacha. Akikataa kukusikiliza utakuwa umejua rangi halisi ya bosi wako ila usikae kifalafala.
Hii dunia imejaa unafiki sana. Nyie ndio mliongoza kumponda na kumsema vibaya. Leo mnajikuta kuonesha upendo. Acheni huo unafiki bakini kwenye rangi zenu halisi
 
Nioneshe wapi na lini mimi binafsi nilimponda. Wakati mashabiki wa Yanga wanawakataa Mzize na Musonda, na hii ni juzi juzi tu hapa kuonesha mlivyo vigeugeu, mimi nilikuwa mmoja wa watu wachache niliosema wakiachwa Simba wachukue.

Suala la umri bado lina utata labda ndilo linawapa kigugumizi Yanga na huyo Mzize mwenyewe.
 
Mzize anamiaka 21 ,
swali ni
  • je ataweza kupambania namba hapo wydad..?
  • Unakumbuka samatta wakati anatoka TP Mazembe alikuwa ameachive nini kwenye ligi ya mabingwa
Hilo si jukumu la Yanga kuzingatia. Hakuna sehemu yoyote duniani eti klabu inakataa kumuuza mchezaji kisa huko anakoenda anaweza asipate namba! Hayo ni mambo ambayo mchezaji mwenyewe na management yake binafsi inazingatia.
 
We jamaa pamoja na kwamba unachezea utopolo nimekupigania sana ili timu yako isilalie fursa zinazokujia. Niliwahi kusema ukipunguza wenge wewe ndiyo unaenda kuchukua mikoba ya kina Samatta na kuibeba Taifa Stars kwa miaka 5 ijayo. Utulivu wako wa sasa unaonyesha kile nilichokiona.

Wydad wameonyesha nia ya dhati ya kukutaka ila klabu yako inakubania. Usidhani wanafanya hivyo kwa faida yako. Watakupa mifano ya kina Miquisonne, Msuva na Chama ila hawakupi mifano ya kina Percy Tau, Himid Mao, Mayele na wengine ambao wamefanikiwa huko huko Uarabuni. Hii nchi tuna historia ya kubania watu fursa za nje, kamuulize Sunday Manara kama sikosei tena hiyo Yanga ndiyo kabisa ina historia mbaya. Kina Nonda Shabani walitoroka na klabu haikupata hata sumni maana angesema afuate utaratibu asingeruhusiwa.

Wakikwambia eti unaenda kufunga magoli 2 fainali ya CAFCL na thamani yako itapanda, waambie waweke nyumba zao za urithi mechi ya Jumamosi na Al Hilal kama kweli wanaamini hivyo. Usikubali wakupumbaze na vikiki vya kuvamia dukani kwako kununua mashati, siku zote adui ya binadamu ni mtu wake wa karibu.

Wydad miezi michache ijayo anaenda kucheza Club World Cup. Anakutana hatua ya makundi na Juventus na Man City. Imagine ufunge goli kama lile ulilowapiga Mazembe, unadhani fursa kiasi gani zitafunguka?

Hata kama unadhani hao kina Hersi wamekulea na kukukuza kiasi gani au unadhani wazee wa Yanga ndiyo wamekutengeneza (labda kama hili lina ukweli), ifike wakati ujisimamie kama mwanaume. Kuna wachezaji wengi wameviendekeza hivi vilabu wakaishia kustaafu kwa fedheha.

Muite Meneja na Wakala wako, muite mezani Hersi mwambie ukweli kwamba unashukuru hapo alipokufikisha ila hii fursa hautaki kuiacha. Akikataa kukusikiliza utakuwa umejua rangi halisi ya bosi wako ila usikae kifalafala.

Yangu ni hayo tu.
Kolo mshauri na kibu
 
Upo sahihi mkuu mimi natamani sana tupate kina samatta wengi kwani West Africa wamewezaje kujaa Europe, ni muda sasa mchezaji akiimarika akatafute changamoto sehemu nyingine
 
GUSA ACHIA TWENDE KWAO imeibua mambo mengi kutoka kwa MAKOLO. Na bado na mtasema timu nzima ipiganie haki. GUSA ACHIA TWENDE KWAO ndo kwanzaaa kabisa nchini ila malalamiko ni mengi.
 
Siku zote utopolo wana roho mbaya sana. Hawawez kumkubalia jamaa watamfanyia roho mbaya tu asipate rizki yake.
Percy tau saiv anaenda qatar kule anaenda kupokea bilioni 2 kama mshahara kila mwezi...
 
Anzisheni chama cha kutetea wachezaji wa Yanga maana mna uchungu nao sana
 
Simba akili zenu mnazijua wenyewe Mzize anaweza kuuzwa hata zaidi ya hiyo pesa unayosema akiwa bora zaidi na akaenda kucheza mpira Ulaya sio swala la kukurupuka tu ukiambiwa 1 B hii unauza harafu Timu yako unayoijenga inakufa kwa 1b uliyomuuza mchezaji jifunzeni ninyi Simba mmeuza wachezaji harafu mkawarudisha mkitegemea kiwango kitakua kile kile huku Timu ikipotea harafu ndio upo busy kumshauri Mzize..
 
We jamaa pamoja na kwamba unachezea utopolo nimekupigania sana ili timu yako isilalie fursa zinazokujia. Niliwahi kusema ukipunguza wenge wewe ndiyo unaenda kuchukua mikoba ya kina Samatta na kuibeba Taifa Stars kwa miaka 5 ijayo. Utulivu wako wa sasa unaonyesha kile nilichokiona.

Wydad wameonyesha nia ya dhati ya kukutaka ila klabu yako inakubania. Usidhani wanafanya hivyo kwa faida yako. Watakupa mifano ya kina Miquisonne, Msuva na Chama ila hawakupi mifano ya kina Percy Tau, Himid Mao, Mayele na wengine ambao wamefanikiwa huko huko Uarabuni. Hii nchi tuna historia ya kubania watu fursa za nje, kamuulize Sunday Manara kama sikosei tena hiyo Yanga ndiyo kabisa ina historia mbaya. Kina Nonda Shabani walitoroka na klabu haikupata hata sumni maana angesema afuate utaratibu asingeruhusiwa.

Wakikwambia eti unaenda kufunga magoli 2 fainali ya CAFCL na thamani yako itapanda, waambie waweke nyumba zao za urithi mechi ya Jumamosi na Al Hilal kama kweli wanaamini hivyo. Usikubali wakupumbaze na vikiki vya kuvamia dukani kwako kununua mashati, siku zote adui ya binadamu ni mtu wake wa karibu.

Wydad miezi michache ijayo anaenda kucheza Club World Cup. Anakutana hatua ya makundi na Juventus na Man City. Imagine ufunge goli kama lile ulilowapiga Mazembe, unadhani fursa kiasi gani zitafunguka?

Hata kama unadhani hao kina Hersi wamekulea na kukukuza kiasi gani au unadhani wazee wa Yanga ndiyo wamekutengeneza (labda kama hili lina ukweli), ifike wakati ujisimamie kama mwanaume. Kuna wachezaji wengi wameviendekeza hivi vilabu wakaishia kustaafu kwa fedheha.

Muite Meneja na Wakala wako, muite mezani Hersi mwambie ukweli kwamba unashukuru hapo alipokufikisha ila hii fursa hautaki kuiacha. Akikataa kukusikiliza utakuwa umejua rangi halisi ya bosi wako ila usikae kifalafala.

Yangu ni hayo tu.
Salama Ngare AKA Nifah hebu njoo na uchambuzi wako juu ya hili.
 
Back
Top Bottom