DOKEZO Clinic ya Marie Stopes Mwanza inatoa huduma za utoaji mimba (abortion)

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Siwaungi mkono ila partly aliyeamua kuitoa humzuio kwa kufunga kituo. Mungu aingilie kati tu. Inaanzia kwenye uzinzi. Hayo ndo matokeo ya uzinzi.
 
Ila nyie wanaume pia ndo visababishi sana kwenye utoaji mimba, na mara nyingi nyie ndo mnatoa hela ya ku cover gharama ya hiyo dhambi.
Usilaumu mwanaume. Wanaume kukwepa ujauzito ni jambo la kawaida na halijaanza leo. Tatizo linapoanza ni namna mabinti wanachangua wanaume wa kuwapa ujauzito.

Binti anajua kabisa huyu jamaa hana ramani, mume wa mtu, au chakaramu tu ambae hana mbele wala nyuma mwisho wa siku analala nae na kumuachia amkamulie tui la nazi ndani akishashika mimba tayari anaanza kuhaha.

Jamii inawalea watoto wa kike with Zero accountability kwa kisingizio kuwa ni viumbe dhaifu na wanatakiwa kuonewa huruma. Nenda familia za kiarabu na kihindi kama utasikia huu ujinga wa kuzalishana bila utaratibu wa ndoa sababu wana mifumo ya accountability.

Binti wa kiarabu akizaa bila Ndoa baba au kaka anaweza kumuua na hakuna mtu ataingilia. Huwezi kuta binti wa kiarabu anachezewa. Sisi sasa hawa wetu, wanazaa na yoyote wanaejisikia kumpa gemu with zero accountability ya maamuzi na matendo yao.

Kwasababu wanajua hakuna wa kuhoji maamuzi yao. Nenda huko vichochoroni utakuta vibinti vinakunjwa. Nenda bar n pubs, Lodges utavikuta vinaingia na mababa umri wa wajomba na baba zao wadogo.

Ukimfuata huyu binti umchane makavu anaweza kukujibu maneno ambayo yatakupa msongo wa mawazo mwaka mzima. Ila binti huyu huyu akishika ujauzito au akiharibika kizazi au kupata maradhi ya zinaa kama ukimwi ndio hawa hawa utasikia Ummy Mwalimu, Flaviana Matata, na wanaharakati wengine wanapigia chapuo zitengewe fedha za wizara au serikali ikaombe misaada au mikopo kuwasaidia na majanga kama kipindi kile cha magufuri alipopiga marufuku binti akizhika ujauzito kurejea shule na wenzake kama hakuna lililotokea na jamii nzima tukasema magufuri ana roho mbaya.

Sasa hapa mwanaume anahusikaje. Mabinti wangapi wanajitambua na wanafikia maisha mazuri na kuishi kama wengine. Ni swala la kuwa accountable tu hapa ndio naliona.
 
unapinga wewe kama nani kwani hii kazi ya kujaji mwachie Mungu atawachoma mwisho wa dunia. acha watu wapate huduma za uzazi salama
Napinga kwa sababu ni kinyume sha sheria ya nchi. Wala sijam judge mtu. In fact wewe ndo umeni judge kwa kuniita SHETANI. Mimi nimeripoti wavunjaji sheria za nchi yetu.
 
Reactions: Cyb
unajichosha kujipa kazi ya Mungu mtu ebu pumzika. unahesabu dhambi za watu kama vile wewe ni mtakatifu huna dhambi ata moja
Sijahesabu dhambi ya mtu, wewe ndo umeniita SHETANI.
Mimi naripoti wanaovunja sheria za nchi.
 
Wewe unajua Leo hiyo Kaka,hiyo taasisi ndio kazi yake lakini kingine vitendo vya kutoa mimba Ni kawaida at least hapo wanatoa very professional kuliko kwenda kutoa mtaani
Basi ishawishini Wizara ya Afya na wizara ya sheria wabadili sheria na kuruhusi abortion. Sio kutetea watu wanaofanya mambo kinyume cha sheria ya nchi
 
Haujakose kuleta hii taarifa hapa. Hawa wanaokupinga wanataka kukutibua tu. Ila upo sahihi kabisa.
 
Siwaungi mkono ila partly aliyeamua kuitoa humzuio kwa kufunga kituo. Mungu aingilie kati tu. Inaanzia kwenye uzinzi. Hayo ndo matokeo ya uzinzi.
Suluhisho sasa ni nini?Tuache, tunyamaze waendelee tu kuvunja sheria ya nchi?
 
njaa tu zinakusumbua mbona huachi kazi kama unajua unavunja sheria na ni dhambi
 
Uko sahihi pia kwa upande mwingine nakubaliana na wewe.
 
njaa tu zinakusumbua mbona huachi kazi kama unajua unavunja sheria na ni dhambi
Ni kweli njaa ninayo, hilo nimelisema tangu awali.
Lakini hiyo haiwezi kuwa justification ya kufumbia macho uvunjaji wa sheria.
 
Reactions: Cyb
Iyo ni tabia ya kike mzee.. kuzaa ni uhamuzi wa mtu na mimba inaweza kutolewa kwa usalama na muhusika akaendelea na mishe zake za kila siku.. hivi wewe ulipo hauna kosa hata moja kisheria unasema ulikua unahusika kuzitoa izo mimba kama kweli unajutia hicho kitendo kwanini usiende kusema polisi ili na wewe ukamatwe badala yake unawachongea wenzako kwa identity fake. Kazi hauiwezi achana nayo kimya kimya
 
we ni mtu wa ajabu mbona unahusika kwenye uvunjaji sasa
Si umesema kabisa wewe mwenyewe kuwa ni njaa?
Ni kweli nina njaa. Ila nimeamua kutoendelea kuwa sehemu ya hilo tena. Potelea mbali.
Unaniona mimi wa ajabu, ila wewe unaetetea utoaji wa mimba unajiona wa kawaida?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…