Clip ya RC Chalamila imenikumbusha mara ya kwanza nilipohudhuria mazishi ya kiislamu. Yale mafundisho nlopata pale huwa yananirudia akilini

Clip ya RC Chalamila imenikumbusha mara ya kwanza nilipohudhuria mazishi ya kiislamu. Yale mafundisho nlopata pale huwa yananirudia akilini

Funzo lisilo na kikomo?
Imani zingine bana miyeyusho sana kiumbe hai chochote kufa ni lazima
Kwa sababu Dunia Sio milele ni sehemu ya kupita then unaenda sayari zingine zisizo na kifo
 
Nimekutana na huu Ujumbe wa RC Chalamila ila sijajua ilikuwa lini umenitafakarisha Sana katika Sabato ya leo

Kwamba Mazishi ya muislamu ni ibada kamilifu isiyo na mbwembwe zozote

Kwamba Ulikuja mtupu na unarudi mtupu hakuna mbwembwe za aina yoyote wala sababu za kumchelewesha marehemu ambaye Mungu amempenda zaidi

Nawatakia Sabato Njema!
 
Aache kusambaza UDINI
Sanyingine kuchagua kunyamaza hufaa sana
 
Nimekutana na huu Ujumbe wa RC Chalamila ila sijajua ilikuwa lini umenitafakarisha Sana katika Sabato ya leo

Kwamba Mazishi ya muislamu ni ibada kamilifu isiyo na mbwembwe zozote

Kwamba Ulikuja mtupu na unarudi mtupu hakuna mbwembwe za aina yoyote wala sababu za kumchelewesha marehemu ambaye Mungu amempenda zaidi

Nawatakia Sabato Njema!
Dini ni imani, nashauri usiwe mjadala kujua nani yuko sahihi kwenye muda wa kuzika. Hii itatuletea mjadala usio na afya kama ule wa nani ana haki ya kuchinja.

RC Chalamila anafanya utani tu na ukiwa mjinga utamuamini. Kama angekuwa serious si angeondoka kwenye madhehebu yake ya KIKRISTU na kuhamia UISLAMU fasta? Na hakuna dini nyepesi kujiunga kama UISLAMU.

HAMIENI tu na wewe mtoa mada johnthebaptist na RC wako
 
Ukitaka urudi kama ulivyozaliwa basi hata marehemu alitakiwa arudi akiwa mtoto
 
Hao jamaa wako njema kwenye mambo ya ndoa na mazishi

Kuna muda huwa nataman kuwa upande huo maana huku wizi umezidi,eti tuna wageni wiki hii tunataka michango

Serikali imesema itagharamia uharibifu kanisa la geita lakin wajuaji wamesema tuchange,kwahyo wanataka wapige pote za serikali na za waumini,
 
Kuna Clip ya RC Chalamila anasifia mazishi ya waislamu. Pale RC kiukweli kasema ukweli mtupu.

Nakumbuka siku moja nilihudhuria mazishi ya muislamu mmoja mtaani kwetu, huyo marehemu alikua ni mtu mkubwa kdg na anafahamika hvyo kwenye mazishi alikuwepo Shehe mkuu wa msikiti wa pale mtaani, Shehe mkuu wa wilaya nadhan na shehe mkuu wa mkoa.

Baada ya kufanya ibada zao, Shehe wa wilaya alifanya tafsiri kdg ya swala ilofanywa pale, sababu pale kabla kuna mzee mmoja alichuchumaa pembeni ya kaburi akaanza kutamka maneno ambayo ni kama swala hv lkn kwa kiarabu. Kumbe ile nadhan huwa ni sura kwenye Quran.

Yule shehe alisema kwamba siku ukifa, Mungu atamtuma malaika wake na utaulizwa hapa duniani uliabudu nini?

Je uliabudu tamaa zako na kuzisikiliza kila zinachokusukuma unafanya?

Au uliabudu pesa zako, ukafanya zikusahaurishe kila kitu?

Au uliabudu wadhifa wako?

Au ulimuabudu Muumba wako?

Yule shehe alienda mbalu akasema pia hawa watu wanaotetea mambo ya ushoga kwa kisingizio cha haki za kibinadamu wakumbuke pia kuna haki za Mungu, kama haki ya binadamu inaenda kinyume na haki ya Mungu basi huo ni ubatili.

Mwisho nilitoka pale nimenywea sana, mwezi mzima nilinyooka kwa mafundisho nilopata pale
Haya maisha tuombe mwisho mwema Tu mauti ni ukumbusho tosha hatutakiwi kuipaparukia sanaa hii dunia
 
Attachments

  • 60ba2cf4d6cc1d09f746d60ba9c92b81.mp4
    15.3 MB
Back
Top Bottom