Clouds FM kuwatema watangazaji PJ, Gerald Hando na Abel Onesmo wa Power Breakfast

Clouds FM kuwatema watangazaji PJ, Gerald Hando na Abel Onesmo wa Power Breakfast

Kutumbua majipu imekuwa lugha maarufu tangu kuingia madarakani kwa Rais, Dkt John Magufuli. Watumishi wa Umma wanaoshindwa kutimiza vyema majukumu yao wanafukuzwa au kusimamishwa kazi mara moja, huko ndio kutumbua majipu.

Kutumbua majipu kumeanza kutumika katika sekta binafsi ambapo wafanyakazi maarufu wa Clouds Fm, wametumbuliwa.

Habari zinasema kwamba PJ, Abel Onesmo na Gerald Hando watapigwa chini kuanzia mwezi April mwaka huu. Kwa kawaida, Clouds wana utaratibu wa kutoa mikataba mipya kila ifikapo April 1.

Katika zoezi hilo kuna wafanyakazi wapya wanaopewa mikataba na wale wa zamani ambao kituo kinawahitaji "hurenew" mikataba yao.

Imefahamika kwamba PJ , Abel Onesmo na Gerald Hando ambao wote wanatoka kipindi cha Power Breakfast (PB) watapigwa chini mwezi huu au kwa kauli ya mjini ni kwamba "Watatumbuliwa".

Sababu kubwa inayotajwa ya wakongwe hao kupigwa chini ni kushindwa kuendana na taratibu za kampuni hiyo kongwe na kinara katika sekta ya Burudani nchini kwani wanajiona wao wako juu ya watu wote.

Pia inasemekana suala la Rais Magufuli kupiga simu kwenye kipindi cha Clouds 360 limewauma sana kwani walikuwa wanaamini wao ndio kipindi bora zaidi cha asubuhi hivyo Suala la Magufuli kupiga simu 360 limeprove "otherwise".

Inadaiwa kuwa msuguano mkubwa ulianza wakati wa kipindi cha uchaguzi kutokana na kutumika kisiasa na kulipwa na baadhi ya wanasiasa ili watumie Power Breakfast kama jukwaa la kuwasafisha kinyume na maadili ya kazi yao yanayosisitiza "neutrality" katika kutoa habari.

Vilevile habari za kuaminika kutoka ndani ya Clouds zinasema kwamba tayari Clouds Media Group imeajiri vichwa vipya ambavyo kuanzia tarehe 1 vitaanza kupiga kazi.

Clouds nao wametumbua!

Mbona umewahi sana, April fool bado.
 
Duh huwa wanachangamsha sana kipindi kusema ukweli
 
Nasubiria kwa hamu kuona kama chapombe Hando atatumbuliwa.
vyapombe


hando sijui sijawahi kumuona...


Pj hata juzi J3 USIKU nilimuona kunduchi anakula, bia kibonde hata sijui niseme nini maana ni mlevi kupindukia kuna siku nilimuona pale chuo cha uhasibu kalewa anayumbayumba na suti yake mchana wa saa7 hahahah
 
waache mbwembwe, kwanza hao wanaofukuzwa wote wanavipaji na hawabahatishi, ko sidhani kama watakosa kazi sehem nyingne. Mungu awasimamie, all in all nataka nkaombe kazi pale cloudz ya utangazaji cjui wanataka vigezo gan wakuu?
Mkuu wakitoka tu m naingia ....umeshachelewa
 
Kiukweli clouds wakitaka wapoteze direction kwenye PB ya clouds wawatoe hao jamaa mm nitakuwa wa kwanza kuacha kusikiliza maana nawapenda sana hao jamaa asubuhi huwa aipiti Bila kusiliza PB. Apo awali nilikuwa napenda kusiliza sana JAHAZI kipindi hicho akiwepo CPT G.HABASHI baada ya kuhama jahazi imepooza maana kibonde ni siasa tu Kiukweli clouds walikuwa na watangazaji wazuri sana nasikitika kuona wanaishia wapi
 
vyapombe


hando sijui


pj hata juzi nilimuona kunduchi anakula bia kibonde hata sijui niseme nini maana ni mlevi kupindukia kuna siku nilimuona pale chuo cha uhasibu kalewa anayumbayumba na suti yake mchana wa saa7 hahahah
Kama ni mlevi na kazi yake anafanya vizuri.. Sioni tatizo..... Pj na Hando kiukweli wapo vizuri...
 
kama alivyopwaya fredwa leo sidhani kama kitasikilizwa tena aisee. ngojea tuone maana wote wawili hawakuwepo leo pengine utekelezaji ushaanza.
 
Kama ni mlevi na kazi yake anafanya vizuri.. Sioni tatizo..... Pj na Hando kiukweli wapo vizuri...
mhhhhhhhhhhhhhhh kuna muda ukimskiliza kibonde unajua kabisa huyu jamaa kalewa ...


mi naskiliza clouds tangu asubuhi mpaka saa 7 mchana kisha milad ayo


diva hata akitumbuliwa saa hii atumbuliwe tu kile kipindi maadili yake ni0.....................
 
Clouds wanawaweza sana. Hii taarifa imetolewa ili wapate attention ya Watu. Matarajio ni kuwa kwa mjadala kama huu PB na clouds kwa ujumla itaongeza wasikilizaji iliyowapoteza au ambao walikuwa wamepunguza "mahaba". Rejeeni stori za kuondoka Kibonde na "ugomvi" studio!!

Ni mikakati ya marketing.
Bravo Clouds
 
Back
Top Bottom