Clouds FM kuwatema watangazaji PJ, Gerald Hando na Abel Onesmo wa Power Breakfast

Clouds FM kuwatema watangazaji PJ, Gerald Hando na Abel Onesmo wa Power Breakfast

Ngumu kumesa.

Ngoja tusikilizie kwanza.

Yule mpayukaji Kibonde amemuacha?? au kwa kuwa ni swahibaaaaa
 
Mimi sioni jipya hapo,Ajira ni kama basi unapanda na kushuka wengine wapande pia.
 
Kama binadamu.. Wanaweza kukosea... Lkn kuwatoa Hando na PJ ....mmmmmh!!!! Watakua hawajui watendalo. Hivi Yale magazet yatasomeka kweli!?! Fredwaa na mizaa atasikilizwa na nani?! Mfano uchambuzi wa leo ..
Leo uchambuzi ulipwaya sana kama ni kweli nitawamiss sana PJ na Gerald Hando nilikuwa navutiwa na uchambuzi wao wa magazeti.
 
Kutumbua majipu imekuwa lugha maarufu tangu kuingia madarakani kwa Rais, Dkt John Magufuli. Watumishi wa Umma wanaoshindwa kutimiza vyema majukumu yao wanafukuzwa au kusimamishwa kazi mara moja, huko ndio kutumbua majipu.

Kutumbua majipu kumeanza kutumika katika sekta binafsi ambapo wafanyakazi maarufu wa Clouds Fm, wametumbuliwa.

Habari zinasema kwamba PJ, Abel Onesmo na Gerald Hando watapigwa chini kuanzia mwezi April mwaka huu. Kwa kawaida, Clouds wana utaratibu wa kutoa mikataba mipya kila ifikapo April 1.

Katika zoezi hilo kuna wafanyakazi wapya wanaopewa mikataba na wale wa zamani ambao kituo kinawahitaji "hurenew" mikataba yao.

Imefahamika kwamba PJ , Abel Onesmo na Gerald Hando ambao wote wanatoka kipindi cha Power Breakfast (PB) watapigwa chini mwezi huu au kwa kauli ya mjini ni kwamba "Watatumbuliwa".

Sababu kubwa inayotajwa ya wakongwe hao kupigwa chini ni kushindwa kuendana na taratibu za kampuni hiyo kongwe na kinara katika sekta ya Burudani nchini kwani wanajiona wao wako juu ya watu wote.

Pia inasemekana suala la Rais Magufuli kupiga simu kwenye kipindi cha Clouds 360 limewauma sana kwani walikuwa wanaamini wao ndio kipindi bora zaidi cha asubuhi hivyo Suala la Magufuli kupiga simu 360 limeprove "otherwise".

Inadaiwa kuwa msuguano mkubwa ulianza wakati wa kipindi cha uchaguzi kutokana na kutumika kisiasa na kulipwa na baadhi ya wanasiasa ili watumie Power Breakfast kama jukwaa la kuwasafisha kinyume na maadili ya kazi yao yanayosisitiza "neutrality" katika kutoa habari.

Vilevile habari za kuaminika kutoka ndani ya Clouds zinasema kwamba tayari Clouds Media Group imeajiri vichwa vipya ambavyo kuanzia tarehe 1 vitaanza kupiga kazi.

Clouds nao wametumbua!

==============
Mwingine
=============
Leo ni 30.03.2016, kesho ni 31.03.2016 na kesho kutwa ni 01.04.2016 siku ya hatari duniani kote
 
Mhh! Hivi ni kweli au ndo tunakaribisha April 1, 2016

TAARIFA Nilizonazo Ni Kwamba Kuna CHEMBE CHEMBE Zote Za UKWELI ULIOTUKUKA Kwamba Jamaa Wametemwa. Mleta UZI Hongera Sana Na Mno Kwa Kuja Na TAARIFA Hii MUHIMU. Hauko Mbali Na USAHIHI Wake. Jamaa Ndiyo Bye Bye Labda Huruma Za Members Humu Ziwaingie WAAJIRI Wao Wawasamehe Wabadilishe Mawazo.
 
Taarifa za kukatisha tamaa sana... Ivi kwani hao waajiri hawaoni umuhimu wao... Kuwandaa watangazaji wapya mpaka wakubalike ni lini!?! Ila yetu macho... Liwalo na liwe....
 
TAARIFA Nilizonazo Ni Kwamba Kuna CHEMBE CHEMBE Zote Za UKWELI ULIOTUKUKA Kwamba Jamaa Wametemwa. Mleta UZI Hongera Sana Na Mno Kwa Kuja Na TAARIFA Hii MUHIMU. Hauko Mbali Na USAHIHI Wake. Jamaa Ndiyo Bye Bye Labda Huruma Za Members Humu Ziwaingie WAAJIRI Wao Wawasamehe Wabadilishe Mawazo.
.....E fm,
 
Back
Top Bottom