Clouds FM kwanini mnasema wazi kuwa Yanga na Singida BS ni ndugu?

Clouds FM kwanini mnasema wazi kuwa Yanga na Singida BS ni ndugu?

ngara23

JF-Expert Member
Joined
Aug 31, 2019
Posts
9,091
Reaction score
21,087
Nimesikitishwa na kituo cha clouds FM kusema ati Yanga na SBS ni ndugu na wana jambo lao Moja

Clouds FM ni media ambayo imejijengea heshima Kwa muda mrefu, kwanini Sasa inataka kujiondelea hiyo heshima

Mmejiajiri media personnel wasio kuwa na waledi

Yaani undugu wa Yanga na Singida BS unatoka wapi

Singida Black Stars ni team inafanya biashara na timu zote
Imefanya biashara na Simba wakichukua wachezaji akina Aishi Manula, Kennedy, Yusuph Kagoma na wengine
Kwanini biashara ikifanyika dhidi ya Yanga ionyeshe hujuma

Hoja ya udhamini wa GSM
GSM sio mmiliki wa Yanga,GSM ni mfanyabiashara, Yeye anatangaza biashara zake kupitia timu za mpira,
Wala udhamini wake hauathuri chochote

Clouds FM jitathimini haraka na mbadilike
 

Attachments

  • markup_1000103295.png
    markup_1000103295.png
    1.4 MB · Views: 1

Hiki kitabu nimekisoma Vizuri mno.
Kinaelezea Uhusika wa Michezo katika Kusaidia harakati za Kupambania Uhuru.

Kwa kifupi kinasema
1. Mashabiki na Viongozi wa yanga hawakuwa ni Watu wenye elimu kabisa.
(Walikuwa wajinga).

2. Yanga ilikuwa ni timu ya walala hoi Hoehae Timu ya watu wasio na ukwasi.
( Masikini wakubwa.).

3. "Mashabiki wa Yanga ni wala Mihogo wameshiba mihogo huko wanakuja kuisema zena yanga"
Yanga vs club African 0-0
Rais wa yanga 2022

4 .Nadhani bado kuna Muendelezo wa hii historia hadi leo baada ya Miaka 60 ya Uhuru na Miaka 90 ya kuanzishwa yanga.

UTOPOLO
 
Hiki kitabu nimekisoma Vizuri mno.
Kinaelezea Uhusika wa Michezo katika Kusaidia harakati za Kupambania Uhuru.

Kwa kifupi kinasema
1. Mashabiki na Viongozi wa yanga hawakuwa ni Watu wenye elimu kabisa.
(Walikuwa wajinga).

2. Yanga ilikuwa ni timu ya walala hoi Hoehae Timu ya watu wasio na ukwasi.
( Masikini wakubwa.).

3.Nadhani bado kuna Muendelezo wa hii historia hadi leo baada ya Miaka 60 ya Uhuru na Miaka 90 ya kuanzishwa yanga.
Kishushe hapa mkuu ili tuwajue vizuri tuanze kuwakaanga.
 
Vituo vingi vya redio vina watangazaji Makanjanja, Ukweli ni kuwa Mechi ya kwanza ya Singida Big Star vs Yanga iliyochezwa Aman Stadium Zanzibar

Ndio Mechi pekee iliyokua na ushindani kuanzia kwa Makocha mpaka wachezaji uwanjani.

Ni moja ya Mechi iliyochezwa kwa daraja la juu kabisa la Ushindani uwanjani uku marefa wakichezesha fair kabisa.

Awa wachambuzi njaa wanaolipwa 10,000/= wengi hawana uwezo wa kuchanganua soka.
 
Hapo kwenye gsm kutangaza biashara zake kwenye timu zote hizo ndipo tatizo lilipo kwani hujui kwamba timu ikifanya vizuri ndani na kimataifa ndivyo biashara zake zinavyozidi kukuwa, na katika timu zote anazodhamini yanga ndio yenye uwezo wa kufanya vizuri sehemu zote mbili kwahiyo ni lazima afanye juu chini ili ahakikishe yanga ambayo pia ndio timu anayoshabikia inapata ushindi, na njia mojawapo anayotumia ni pamoja na kushawishi zile timu ndogo anazozidhamini ziiachie yanga ipate ushindi dhidi yao ili yanga izidi kufanya vizuri kwenye ligi
 
Back
Top Bottom