Jaji Mfawidhi
JF-Expert Member
- Feb 20, 2016
- 15,835
- 23,776
Mwanamuzi, muimbaji na mtunzi wa nyimbo za injili Israel Mboni ametua Tanzania kufanya tamasha Mlimani City na Leaders Club.
Katika interview pale Clouds muwe mnaweka, kama ni mtu wa injili basi wale watu wa gospel, wenye uelewa wa injili na kufuatilia na ikibidi wekeni mlokole.
Sasa Sudi Brown ni "mataifa' "kafiri"na hamjui Mungu alafu anawekwa kumuuliza mtu aliyeokoka, kajikuta anauliza maswali ya ngono ambayo ndio wamezoea kuuliza wasanii.
Clip ya mahojiano hayo nimeona aibu kuipost hapa maana hata waandishi wengine watajisikia vibaya.
Kwa ujumla, mwandishi huwezi kuwa mbobezi wa kila kitu, ni sawa ni kibatala leo u mlete afanye ishu za corporate, hatoweza.
Ajiri watu wenye profession zao hata kwa mkataba wa kazi maalum.
Sitoshangaa sku mnamuhoji raisi au makamu mkaanza kumuuliza maswali kama hayo.