Clouds FM uvumilivu umewashinda, waanzisha kipindi cha michezo asubuhi

Baba yangu sisi wabongo ni wajuaji kinyamaa alafu wabishi dunia nzima!

Nilitegemea kukuta ubishi wa hivyo yani mtu hata hajasikiliza Radio labda mara ya mwisho amesikiliza miezi minne nyuma lakini anabisha tu hahahahaha kudadaaadeki😂😂

Huyo unayemsema yuko sahihi kuliko kilicholetwa na mleta maada.

Bado siyo kipindi rasmi.
 
Kipindi Cha michezo cha asubuhi kumbukumbu zangu zinaniambia mwasisi Ni RFA. Kilikuwa kinaanza saa 1:30 asubuhi hadi saa 1:50 asubuhi.

EFM alochofanya ni kuwa na masaa mengi tofauti na RFA.
 
Clouds imeishiwa kitambo tu, hawana jipya hata kidogo. Wasafi nao ni wachovu sana kwa vipindi vya redio.
Hawajaishiwa mzee, issue ni kuwahabarisha wateja wao ..kuhakikisha msikilizaj abanduk redion
 
vipindi vya michezo asubuhi vilianzishwa na Radio free africa, walianza na kipindi chao mwaka 2006 kuanzia saa 1:20 asubuhi
Naaaam, RFA ndiyo waasisi wa vipindi vya michezo asubuhi.
 
Naaaam, RFA ndiyo waasisi wa vipindi vya michezo asubuhi.
Yes, baada ya matukio. Enzi hizo inabamba sana, kisha baada ya michezo yanafuatia matangazo hadi saa mbili kamili, muhtasari wa habari kisha anaingia Fredwaa na sindano tano za moto. Inafuata RFA bonanza hadi saa sita mchana kisha mapishi na salamu, taarifa ya habari saa 6 na nusu. Saa saba ni DW. Saa nane ni Showtime hadi saa 10 jioni. Kisha mambomambo na RFA hadi 12 kamili, DW kwa nusu saa inafuata BBC. Ilikuwa bandika bandua. Sijui kwnn wamepoa sana siku hizi.
 
Mkuu inaonekana ulikuwa mfuatiliaji mzuri sn wa RFA kipindi hicho.
Ukweli ni kuwa RFA ilikuwa redio bora sana siku za nyuma lkn nadhani Management imewaangusha mpaka watangazaji wote wazuri wakakimbia!
Ukifatilia vizuri utagundua karibu nusu ya watangazaji maarufu wa redio na tv nchini ni zao la RFA.
 
Acha kabisa mkuu. Enzi hizo nilikuwa nachelewa hata kwenda shule sababu ya mpangilio wa vipindi. Kuna muda ilinilazimu kukwepa masomo ili nisikilize redio. Ukija wikend ndio ilikuwa balaa lenyewe. Kuna kipindi kiliitwa Hindu style kama sikosei, ilikuwa inaelezewa movie ya kihindi na unaimagine kama unaona live kabisa. Zilikuwa zikipigwa nach za kutosha usiku wa kipindi. Rest in peace RFA ya enzi hizo. Sound engineers walikuwa makini na sauti ilikuwa haiumizi masikio. Siku hizi sijui wameajiri watu gani, sauti haivutii na kuna muda inakuwa kama inaparaza speaker.
 
Radio One ilikuwa nzuri kwa kipindi cha michezo enzi hizo. Key mtangazaji? Maulid Kitenge.

Ikaja EFM ikawasha moto. Key anchor? Maulid Kitenge.

Kwa sasa inavuma Wasafi na Sports Arena/ Sports Court. Key anchor? Kitenge once again.

In two or tree years kunaweza kutokea Radio nyingine. Sina shaka nahodha wa kipindi cha michezo atakuwa nani.
 
Maulidi Baraka Kitenge ni mmoja kati ya watangazaji waliokuwa wanasauti za kimichezo tangu zamani. Jezi nambari 9 mgongoni. Jamaa anajua sana aisee.
 
Upo Kama mimi Jumbe Brown
 
Issue ni kwamba binadamu tunapenda sana matunda ya mafanikio au kuwaona watu ni mashujaa kwa kuwa wanakuwa "nyuso" za firm husika.

Ila watubwanaokuwa ntuma ya pazia unakuwa ni magwiji kabisa wa tasnia husika.
 
ilikua lazima waweke asubuhi....wenzao sport hq na sport arena wako asubuhi na wamechukua deals zote za pesa..wadhamini wengi wanaona huo ndo muda mzr kuliko saa tatu usiku..
 
Baba yangu sisi wabongo ni wajuaji kinyamaa alafu wabishi dunia nzima!

Nilitegemea kukuta ubishi wa hivyo yani mtu hata hajasikiliza Radio labda mara ya mwisho amesikiliza miezi minne nyuma lakini anabisha tu hahahahaha kudadaaadeki😂😂
Huku kwetu Bara kuna Redio kabisa ya michezo ya Abdallah Majura kwa hiyo ni Redio nyingi tu zinaanza na Michezo asubuhi.
Kwa DSM redio shindani anaona ni Clouds na hao Wasafi na hawa jamaa kwangu ni kero kabisa bora hata vile vipindi vya Traffic Jam au umbeya wa clouds ni Live
kwa asubuhi pesa ni ngumu acheni tuwe wabishi Mkuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…