Indu ,unamzungumzia prince baina kamukuru ilikua raha sana,mm nafikir RFA waliish mbele ya muda maana kwa vipind vile na watangazaj wale hakuna redio ya sasa inayowafikia kila kipind kilikua vzur na watangazaj mahir kwel kwel ,mpaka maripota wao walikua vzur ikaenda ad kwa watuma salamu wakawa maarufuAcha kabisa mkuu. Enzi hizo nilikuwa nachelewa hata kwenda shule sababu ya mpangilio wa vipindi. Kuna muda ilinilazimu kukwepa masomo ili nisikilize redio. Ukija wikend ndio ilikuwa balaa lenyewe. Kuna kipindi kiliitwa Hindu style kama sikosei, ilikuwa inaelezewa movie ya kihindi na unaimagine kama unaona live kabisa. Zilikuwa zikipigwa nach za kutosha usiku wa kipindi. Rest in peace RFA ya enzi hizo. Sound engineers walikuwa makini na sauti ilikuwa haiumizi masikio. Siku hizi sijui wameajiri watu gani, sauti haivutii na kuna muda inakuwa kama inaparaza speaker.