Toka zako hapa. Unajua maana ya critical thinker wewe au umekariri tu?
Wewe mbona mgumu kuelewa wewe? Watanzania mnapenda sana kutumia visivyo phrases za watu.
Huja-declare interest bali 'in the interest of full disclosure' umeweka hadharani unazi wako kwa CHADEMA.
Natumai baada ya kukusahihisha mara mbili hutarudia tena kosa. Sawa ndugu?
Kwanza, unakosea unaposema natetea kila kitu kuhusu Clouds. Hiyo siyo kweli.
Pili, mimi sina maslahi yoyote mahsusi.
Tatu, sitokwi na mapovu.
Nne, mimi siyo bandwagoner. Sirukii tu bandwagon kisa ni kitu ambacho ni popular kukifanya. Sijawahi hata kidogo kuwa mfuata mkumbo.
Kuna wengine humu wamefikia hatua ya kuabudu watu hadi kufikia wakimuona mtu huyo kachukua msimamo fulani basi na wao wanachukua msimamo huo huo. Hawawezi kuchukua misimamo yao kabla ya mungu wao hajachukua msimamo. Na hawawezi kabisa kupingana na hao watu wanaowaabudu.
Mimi siko hivyo. Mimi napima na kutafakari mambo kwa kadri ya uwezo wangu bila ushawishi wa yeyote kabla sijachukua msimamo na huwa siyumbishwi yumbishwi hovyo kama watu wengine.
Hivyo, kutetea kwangu Clouds kuhusiana na hili sakata la sasa hakujatokea tu hivi hivi. Nilisoma ule waraka wa kwanza wa huyo mwanamke na sikuona madai yoyote yale yaliyo mahsusi. Nilichoona ni madai ya jumla jumla mno tena ambayo mengine yalikuwa si sahihi.
Kwa jinsi nilivyo, hata wewe siku ikitokea nimeona unashambuliwa tu pasi na sababu, nitakuwa upande wako, yaani kwa maneno yako - nitatoa povu kukutetea. Hivyo ndivyo nilivyo.