Clouds Media wafungiwa kwa siku 7, kwa kutangaza Takwimu za Uchaguzi ambazo hazijathibitishwa na Tume

Clouds Media wafungiwa kwa siku 7, kwa kutangaza Takwimu za Uchaguzi ambazo hazijathibitishwa na Tume

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760
Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imevifungia vituo vya habari vya Clouds TV na Radio kwa siku saba kuanzia kesho Agosti 28 na adhabu ya kuomba radhi siku nzima ya leo kwa kosa la kukiuka kanuni za utangazaji na kanuni ndogo za utangazaji za Uchaguzi.

TCRA imesema kosa walilolifanya ni kutangaza takwimu za Uchaguzi ambazo hazijathibitishwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC). Hii ni adhabu ya 2 ndani ya mwezi huu kwa Clouds baada ya kipindi chake cha Jahazi kufungiwa siku chache zilizopita.



=====

The Tanzania Communication Regulatory Authority has on Thursday August 27 banned Clouds TV and Clouds FM for Seven days with immediate effect.

The authority said in a press conference today that the station has been banned after it announced election statistics that had not been approved by the National Electoral Commission.

On Wednesday NEC said the station had aired results that showed that certain Members of Parliament aspirants had sailed through unopposed after other contestants failed to meet nomination criteria in certain constituencies.

Earlier this month TCRA banned a radio programme (Jahazi) from the same station for allegedly promoting immorality in the society.

Zaidi, soma;

Uchaguzi 2020 - Tanzania: The National Elections Regulations(2020) - Mambo muhimu ya kuzingatia
 
Tanzania Communication Regulatory Authority( TCRA) imeagiza Clouds TV na Redio kusitisha matangazo yao kwa muda wa siku saba kuanzia kesho 28 Agosti hadi 3 Septemba 2020 kwa kosa la kukiuka kanuni za utangazaji na kanuni ndogo za utangazaji za uchaguzi. Pia, wametakiwa kuomba radhi siku nzima leo.

TCRA Wameyasema hayo Wakati wakiongea na Wanahabari na kudai kwamba, Clouds Media Walitangaza Takwimu za Wagombea waliopita bila kupingwa kinyume na Sheria ya Uchaguzi inavyotaka na kwamba Tume ya Uchaguzi ilikuwa haijawatangaza.

Hivi karibuni Tume ya Uchaguzi ilalamikia baadhi ya vyombo vya habari kutangaza majina ya Waliopita bila kupingwa.
 
Muda huu Eng. Kilaba anazungumza na vyombo vya habari, anatangaza kuifungia Clouds Media TV na Radio kuanzia kesho tarehe 28 hadi tarehe 3 septemba, kuanzia dakika hii hadi jioni Clouds media isitishe matangazo yote na irushe tangazo la kuomba radhi hadi jioni, kosa ni kutangaza wagombea waliopita bila kupingwa
 
Back
Top Bottom