Clouds Media wafungiwa kwa siku 7, kwa kutangaza Takwimu za Uchaguzi ambazo hazijathibitishwa na Tume

Clouds Media wafungiwa kwa siku 7, kwa kutangaza Takwimu za Uchaguzi ambazo hazijathibitishwa na Tume

Mh!
Kwahiyo kuanzia saa hii tutakuwa tunasikia hivi...


"... ndugu watanzania, tunaomba radhi kwa kuwatangaza Kassim, Nape, Aboud na wengine wote wa ccm kwamba wamepita bila kupingwa.... hiki kilichotokea ni kiherehere chetu tu kwani sisi sio tume ya uchaguzi ..."
😂😂
 
Watanzania tukatae udikteta. We want our country back.
HIVI wanasoma wapi uana habari?
Unatangaza waliopita kesho mtu amepigwa pingamizi anaondolewa,

wengine ni wakwepa kodi wewe unajuaje kama atatoboa?
Wafungiwe tu
 
Wakurungezi waliokuwa wanawatangaza wabunge wa CCM na kuwathibitisha kwa hati kuwa ni wabunge wamepita bila kupingwa wameachwa wanafungiwa wale waliotangaza kile kilichotangazwa na wakurugenzi ambao ndio tume yenyewe.
 
Mimi Kama Great Thinker naona mkosaji namba moja Ni Wasimamizi wa uchaguzi ambao walitoa taarifa za watu kupita bila kupingwa, otherwise hata huyo mwandishi asingeweza kujuwa kuwa Kuna mtu kapita bila kupingwa. Poor CCM and it's members
 
NEC wanaandaa mazingira ya vitisho kwa vyombo vyote vya habari ili visithubutu kutangaza matokeo ya uchaguzi as received kutoka majimboni.

Siku 7 zote kwa nini? Huu ni uzuzu. Kuna siku watakuja kuamuru JF isiwe accessed kwa mwezi mzima
 
Naomba pia TCRA imchukulie Babu Tale hatua kwa kosa la kujitangaza mbunge bila idhini ya tume. Ametumia kurasa za kijamii kujitangaza.
 
Wasiwafungie tu Bali wachukue na makatapila wakavunje na kusagasaga ofisi zao pale mikocheni karibu na mwai kibaki road.
 
Clouds Radio na Clouds Tv zafungiwa na TCRA baada ya kukiuka maadili ya utangazaji....

Stay Tuned kwa updates zaidi
 
Back
Top Bottom