Tusiamishe mjadala kutoka pale tulipokuwa tunajadilana. Hoja sio IFFHS hoja nimekuuliza juu nitajie vigezo vya kushiriki michuano ya FIFA club world cup 2025 ni zipi? Maana mkibanwa tu hoja mnahama nje ya mada. Mada iliyopo hapa sio IFFHS bali FIFA club world cup 2025
Kwani hili nalo ni swali la msingi?
Ngoja sasa nikujibu kwa upana na kama ulikuwa unauliza kwa lengo la wewe kutaka kujua basi sio shida.
Kulingana na FIFA ku expand hii michuano kwa kuongeza timu 32 zishiriki Club World Cup
FIFA ikaamua itumie kigezo cha points zilizokusanywa kwa misimu minne ambapo points huhesabiwa kuanzia level ya group stage na kuendelea.
FIFA ilitaka kupata radha kamili ya hii michuano na ndio maana ikatumia kigezo cha consistency yani muendelezo wa kuwa na rekodi nzuri kwa misimu minne.
Walifahamu kuwa wakiweka kigezo cha last tournament na achievement uliyopata kuna timu zisizo bora zinaweza kupata nafasi ya kushiriki ilihali zilipata hayo mafanikio kwa bahati tu.
Sasa maana yake timu ambayo imekusanya pointi nyingi katika misimu minne ipo miguu yote mbele kushiriki mashindano hayo kuliko timu nyingine.
Timu hiyo haitohitaji ichukue ubingwa wa CAF ili ishiriki kwasababu tayari ishafuzu kwa vigezo vilivyowekwa.
Ila kwakua awali FIFA walikuwa wanatoa nafasi kwa timu inayochukua ubingwa basi nafasi hiyo pia ipo hata kwa ile timu ambayo haikuweza kukusanya pointi kwa misimu minne iliyopita.
So ifahamike kuwa awali kushiriki Club World Cup ilikuwa mpaka uchukue ubingwa wa CAF champion league. Lakini kwa sheria mpya za kuingiza timu 4 zinampa fursa hata yule ambaye hajachukua ubingwa kuweza kushiriki iwapo atafikia idadi ya points kubwa
Kumbuka Europe itatoa timu 12, S. America itatoa timu 6, lakini mabara yaliyobaki yatatoa timu 4 yani kuanzia N. America, Africa na Asia hizo zote zitatoa timu 4
Kwa Afrika katika zile nafasi 4 sisi tayari tuna timu 2 ambazo zishafuzu ambazo ni Al Ahly na Wydad. Hizi timu hazihitaji kupata pointi kujazia ili zi qualify.
Nafasi mbili zilizobaki ndio zinashindaniwa na timu eidha iongeze points au ichukue ubingwa wa CAF
Kwa hiyo FIFA wakatoa list ya timu ambazo zipo kwenye marathon ya kuweza kupambania hizo nafasi mbili. Timu ambazo zimepewa probability kubwa kutokana na points zao.