CMAG Yamfariji Rais Samia, Yapigia Debe Ushirikiano Tanzania

CMAG Yamfariji Rais Samia, Yapigia Debe Ushirikiano Tanzania

Zack Abdul

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2026
Posts
1,194
Reaction score
911
Jumuiya ya Madola kupitia Commonwealth Ministerial Action Group (CMAG) imetuma salamu za rambirambi kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, kufuatia kifo cha mume wake, Hafidh Amir Hassan.

Katika kikao chake cha 74 kilichofanyika New York, CMAG ilifanya dakika moja ya ukimya kwa heshima ya marehemu, ambaye alifariki dunia tarehe 7 Septemba 2026.

Katika kikao hicho, CMAG pia ilitambua ushirikiano wa Tanzania na Jumuiya ya Madola, ikiwemo ushirikiano na Mjumbe Maalum wa Katibu Mkuu wa Jumuiya hiyo pamoja na hatua za hivi karibuni za Tanzania katika kushirikisha vyama vya siasa na juhudi za maridhiano Zanzibar.

CMAG pia ilihimiza kuendelea kwa ushirikiano na Tanzania na ikataka Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Madola kuendelea kushirikiana na Rais Samia pamoja na wadau wengine, ikiwemo kupitia ziara nchini Tanzania. Tanzania itaendelea kuwa kwenye Formal Agenda ya CMAG kwa ajili ya mazungumzo na ushirikiano unaoendelea.

Hatua hizi zinaonyesha kuendelea kwa mashirikiano ya kidiplomasia kati ya Tanzania na Jumuiya ya Madola, huku Tanzania ikiendelea kushirikiana na jumuiya hiyo katika masuala ya maridhiano, mazungumzo na uimarishaji wa taasisi.
HSu76nfWcAAfH8_.jpg
HSu77hPXcAARt18.jpg
HSu78kNXsAAFO6N.jpg
 
Back
Top Bottom