Mabeberu huwa ni wana maslahi yao.
Nchi ambayo watu wanaenda kuangalia mpira viwanjani bila barakoa,
nchi ambayo mkutano wa CCM ulifanyika kumpa utezi madam SSH kuwa mwenyekiti nadhani waliovaa barakoa huenda walikuwa hawafiki 10%
Nchi ambayo watu wanajazana kwenye daladala nyomi na wengi hawana barakoa barakoa;
Nchi ambayo wanafunzi na walimu wa kutwa kwa shule za msingi na sekondari kila siku wanaenda shule na kurejea nyumbani,
Nchi ambayo masokoni kwa asilimia kubwa hawavai barakoa na maisha yanasonga;
Najua jaribio la lockdown phase 2 ya corona Tanzania lili-buma na kuvaa barakoa ni sawa mtu kujikinga na kuwakinga wengine ila tunalo jambo kubwa la kumshukuru Mungu kwa kutuponya Tanzania na Afrika kwa ujumla dhini ya athari hasi za kiafya za Corora.
Ilitabiriwa wakati wa pandemic ya kwanza kuwa Afrika watu watakufa kama kuku na tutaona maiti barabarani watu wakianguka, unabii wao ukabuma. Itoshe kusema, Tanzania kwa sasa wataka kuuza chanjo wapige "hela" ila kwa kuwa ndio mambo ya sanyansi na compliance ya EAC, SADC, AU & WHO wacha chanjo ije maadam sio lazima.
Ila kwa kuwa ni kile wanasayansi wanasema "clinical trail"; ahh acha tuone, maana ndio masuala ya kuwa compliance tusibaki "yatima" maana na wenzetu wanachanjwa.
Itoshe kusema, sio kila habari inayotoka kwa mzungu ni njema, kuna zingine pia huwa ni mbaya. Bila shaka NIMR watapata muda kupitia chanjo zinazokuja ili kujiridhisha juu ya content yake.
Suala la msingi, tuna bajeti na equipment za kuweza kujua "kunani" kwenye content ya chanjo?
Tukiweza ku-develop chanjo yetu wenyewe baada ya kujiridhisha ni nzuri, je tukiwauzia "mabeberu" watanunua na za kwetu maana sitakuwa zimekidhi sayansi?
JMT, kazi iendeleee.