#COVID19 CNN: After death of Covid-denying president, Tanzania sets roadmap to combat the virus

eti corona hiyo hiyo ilimuondoa.

acha ujinga kijana,vitu vingine muwe mnakaa kimya.wanaojua haya mambo wakiwasoma wanawasikitikia tu namna ujinga wenu unatumika vibaya.
 
wee jamaa wazazi wako ile pesa ya ada waliyokuwa wanakulipia bora wangekuwa wananunulia kitimoto kilo kadhaa na bia za kutosha ili wafurahishe nafsi zao.
 
Mabeberu huwa ni wana maslahi yao.

Nchi ambayo watu wanaenda kuangalia mpira viwanjani bila barakoa,
nchi ambayo mkutano wa CCM ulifanyika kumpa utezi madam SSH kuwa mwenyekiti nadhani waliovaa barakoa huenda walikuwa hawafiki 10%
Nchi ambayo watu wanajazana kwenye daladala nyomi na wengi hawana barakoa barakoa;
Nchi ambayo wanafunzi na walimu wa kutwa kwa shule za msingi na sekondari kila siku wanaenda shule na kurejea nyumbani,
Nchi ambayo masokoni kwa asilimia kubwa hawavai barakoa na maisha yanasonga;

Najua jaribio la lockdown phase 2 ya corona Tanzania lili-buma na kuvaa barakoa ni sawa mtu kujikinga na kuwakinga wengine ila tunalo jambo kubwa la kumshukuru Mungu kwa kutuponya Tanzania na Afrika kwa ujumla dhini ya athari hasi za kiafya za Corora.

Ilitabiriwa wakati wa pandemic ya kwanza kuwa Afrika watu watakufa kama kuku na tutaona maiti barabarani watu wakianguka, unabii wao ukabuma. Itoshe kusema, Tanzania kwa sasa wataka kuuza chanjo wapige "hela" ila kwa kuwa ndio mambo ya sanyansi na compliance ya EAC, SADC, AU & WHO wacha chanjo ije maadam sio lazima.

Ila kwa kuwa ni kile wanasayansi wanasema "clinical trail"; ahh acha tuone, maana ndio masuala ya kuwa compliance tusibaki "yatima" maana na wenzetu wanachanjwa.

Itoshe kusema, sio kila habari inayotoka kwa mzungu ni njema, kuna zingine pia huwa ni mbaya. Bila shaka NIMR watapata muda kupitia chanjo zinazokuja ili kujiridhisha juu ya content yake.
Suala la msingi, tuna bajeti na equipment za kuweza kujua "kunani" kwenye content ya chanjo?

Tukiweza ku-develop chanjo yetu wenyewe baada ya kujiridhisha ni nzuri, je tukiwauzia "mabeberu" watanunua na za kwetu maana sitakuwa zimekidhi sayansi?

JMT, kazi iendeleee.
 
Shujaa wa Africa leo anaitwa Covid denying President.....teh
Wazungu wat.henge covid ingekuwepo bongo wale jamaa ambao wanajazana kwenye mwendo kasi wandeanza kufa kama simbilisi!!!
sijui ile tume ya mama imekuja na majibu yepi!?
kuna vitu vingine ni reasoning tu
 
Pumba hizo
 
We umerogwa, si bure.
 
Hiyo chanjo ya ndani ikwapi? Tuzidishe maombi?
 
Kalifufueni. Limeshaoza Kule kwenye mabati
 
Mabeberu haya..eti"Covid denying president"

Sitazungumzia kuhusu wahusika lakini ni kweli - marehemu alikuwa ujumbe unaochanganya sana kuhusu corona. Hakusema corona haiko lakini alisema “Mungu katuepusha na corona”. Na ni chini ya uongozi wake tulibeza barakoa, takakataa kupima, tukakataa kutoa takwimu, tukaita ugonjwa fulani “changamoto ya upumuaji”, tukashutumu kuhusu chanjo!! Ni katika kipindi hicho tulikwenda kuchukua dawa Madagascar, tukahimizi nyungu, ikatokea dawa ya Nimcarf, covidol nk.

Tulifunga shule na vyuo! Tukana maji tiririka! Tukavaa barakoa! Tukashauri kutofanya safari zisizo za lazima. Tukawa na wagonjwa na taarifa zikitolewa WHO kila siku lakini tarehe 26/04/2020 ghafla kila kitu kikawa sawa na corona ikatoweka Tz!!

Sijui yote hayo yamefanywa na mabeberu?? Wakati mwingine chuzi zetu zinatupeleka kuwa watu wa hovyo sana!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…