Wako sahihi sana hao maana mpaka sasa haileti mantiki kwanini hatujafa milioni 10 Afrika, na hatuendelei kufa kwa laki tano kila siku.
Huu ugonjwa unawatesa mataifa yenye uwezo mara 1,000 zaidi yetu Afrika, na ukweli hamna kikubwa tunachokifanya kuzuia, Waafrika tupo tupo siku zinaenda, Corona yenyewe inatupapasa wala haijaonyesha makucha huku mpaka sasa.
Ukitembea mtaani uone tunavyoishi, hata kwa wale ambao wamechukua tahadhari ya hali ya juu Afrika, bado hawajafikia hata robo ya wanachokifanya wale wenye kufa Ulaya.
Hiki kitu jameni wazungu wagundue dawa mapema kabla hakijapata sababu za kutukondolea macho Afrika, maana sisi wenyewe hatuna uwezo hata wa kutengeneza dawa za aina ya panadol.