CNN: 'Don't use birth control,' Tanzania's President tells women in the country

Hao wanawakimbia watoto wao ndio wafanye birth control maana hawana uwezo wa kuwatunza.
Halafu nimegundua unachangia tuuu hata wala hukumsikiliza Magufuli alicho ongea... una dandia tuu
 
List of countries by future population (United Nations, medium fertility variant)
From Wikipedia, the free encyclopedia

Jump to navigationJump to search
This is a list of countries by future population using the medium variant (which is the recommended one), ranging from 2020 to 2100 in decades or ten-year periods, as estimated by the 2017 revision of the World Population Prospects database by the United Nations Population Division. All figures are rounded and given in thousands.

List of countries by future population (United Nations, medium fertility variant) - Wikipedia
 
This a shame to our nation, yoyote angesema lkn asingekua Raisi wetu, inaonyesha Raisi kwamba hana international exposure.
International exposure ya kitu gani ? Uzazi wa mpango? Ana national exposure ya ukweli kwamba watanzania tunazaana sana ! Na hizo contraceptive methods baadhi zimeonekana kuwa na side effects nyingi kwa akina mama kiafya na hata uzazi wao. Ni heri anaesema ukweli kuliko anayejidanganya ! Na huko Marekani kwenyewe kuna maeneo ya conservatives wanazaa mpaka watoto kumi ! CNN haitangazi hayo mara nyingine.

Mtu mwenye nguvu na uwezo wa kufanya kazi na kutunza familia kwa nini asizae? Hao wachina wenyewe sasa hivi wanaachana na one child policy japo wako wengi. Sio kila sera inayotungwa na wazungu ni relevant kwetu wakati mwingine tunalazimika kuzikumbatia ili tupewe misaada! Hivyo ni lazima sana tupambane na umaskini ili kuepuka utegemezi wa mataifa ya nje kwa njia ya kuomba omba unaotulazimu kukubali kila sera na programu kwa wananchi wetu hata kama zinaenda kinyume na mila zetu.
 
Hao ndio vyombo vya habari za kimataifa kukiwa shwari wanakaa kimya.

Wanasubri wakati muafaka wanashambulia.

Aibu ingine baadhi ya watanzania tunajivika zile sanamu na mbele ya vyombo hivi tukishirikiana navyo kushehereka.

Likipta hili baadhi ya watanzania hao wanavua hizo sanamu na wanarudi kuwa wa kawaida na wanasubiri tena.
 
Hao wanawakimbia watoto wao ndio wafanye birth control maana hawana uwezo wa kuwatunza.
Halafu nimegundua unachangia tuuu hata wala hukumsikiliza Magufuli alicho ongea... una dandia tuu
Siyo mimi sikumsikiliza yeye bali yeye ndiyo hajataka kusikiliza kampeni ya uzazi wa mpango inataka nini. Uzazi wa mpango nia yake ni kila mtu azae watoto anaoweza kuwatunza kama una uwezo wa kutunza watoto 20 vizuri zaa tu. Sasa yeye anasema chapeni kazi na mfyatue watoto tu huu ni upuuzi, utazaaje bila kujipima na kujua uwezo wako wa kulea upoje? Na kwa mfano ukajua unauwezo wa watoto saba utazaaje saba bila usaidizi wa uzazi wa mpango je ukizidisha?

Tatizo hamjaelewa hata kampeni ya uzazi wa mpango ni nini, hatuwezi kuishi kwa kubahatisha tuenende kama mang'ombe sisi ni binadamu. Mungu ametupa utashi na Mungu wetu ni Mungu wa utaratibu lazima tuwe na mpango mkakati katika kila jambo. We have to plan everything maisha yetu lazima yaende kwa mpangilio mimi nilishakataa watoto wa bahati mbaya na wa kushitukizwa najua lini napata mtoto na nani. Siyo umekutana na mwanamke huko hata haeleweki mimba tayari.
 
Umewahi ishi au tembelea kijijini na ukaona maisha ya watu wanaozaa bila mpango .watoto sita chumba kimoja mlo nusu kwa siku na mzazi anawaficha wasiguse shule? Zaeni kama simbilisi Jiwe atawasomesha na kuwanunulia mpaka pedi
 
Kwanini uvilaumu vyombo vya habari kwa kuandika habari, kwa nini usilaumu source yenyewe ambaye ni Magufuli kama asingesema CNN wangeandika nini.

Labda kama ni kuvilaumu tuvilaumu iwapo vitaandika habari ya uongo.
 
Alisema mkazaliane hakusema lazima kila mtu azae na wala hakusema uzae kumi, hata ukizaa mmoja au wawili umezaliana, usipozaa pia upo sahihi. Ndiyo maana Mtume Paulo alishauri Kama hutaki kuingia kwenye ndoa ruksa hii inamaana kutokuzaa pia siyo dhambi maana uzinzi ni dhambi.
 
kama anaweza japo kwa kuthubutu. mwambieni awafukuze wale UNFPA pale mikocheni ndo mjue kama nyie ni nchi yenye eneo kubwa la kiutawala au kajinchi kanakoongozwa na vichaa vichaa hivi
 
apart of loosing MANPOWER, what about other Negativities of using artificial birth control tech's?...
tujiandae kuongeza idadi ya wagonjwa wa mifumo ya uzazi.. endapo TUTAEGAMIA katika ARTIFICIAL BIRTH CONTROL TECH'S
 
Umewahi ishi au tembelea kijijini na ukaona maisha ya watu wanaozaa bila mpango .watoto sita chumba kimoja mlo nusu kwa siku na mzazi anawaficha wasiguse shule? Zaeni kama simbilisi Jiwe atawasomesha na kuwanunulia mpaka pedi
Mkuu waache wazae tutawaanzishia tuzo ya uzaaji bora.

Huwa najiuliza mtu mmoja watoto kumi ili iweje? Kwani ni sifa? Ukiuliza utaambiwa ooh wazazi wangu wasingezaa wengi nisingekuwepo so what? Usingekuwepo ungepungukiwa nini? Ushajiuliza wasiokuwepo wanashida ipi?

Tuacheni fujo zaa mtoto mmoja wawili au watatu wahudumie vizuri, enjoy maisha yako.
 
Tatizo lenu mnafikiri chochote anachosema rais ni sahihi, hata akikosea mtajitahidi kumtafutia tu maneno twa kumpamba ili aonekane hajakosea, sidhani kuwa hiyo ni njia sahihi ya kumsaidia,

Tanzania ina kampeni ya uzazi wa mpango nchi nzima na inasimamiwa na wizara ya afya kwa niaba ya serikali inayoongozwa na Magufuli mwenyewe na rais anaidhinisha bajeti ya kampeni hiyo, nina imani siku ile angesema anaunga mkono uzazi wa mpango sidhani kama leo ungempinga.
 
Hakuna baya lolote alilosema JPM maana hamna MTU atakayepangiwa azae watoto wangapi ila JPM alitoa tu maoni yake tatizo lenu nyie wakosoaji mligeuza Ile hotuba ajenda yenu ya kisiasa badala ya kuangalia uhalisia wa hotuba yenyewe.
 
Umewahi ishi au tembelea kijijini na ukaona maisha ya watu wanaozaa bila mpango .watoto sita chumba kimoja mlo nusu kwa siku na mzazi anawaficha wasiguse shule? Zaeni kama simbilisi Jiwe atawasomesha na kuwanunulia mpaka pedi
Sio tu kutembelea! Nimekaa kijijini miaka mingi tuu na usemayo sio mageni kwangu ! Suluhisho sio kuwafunga vizazi hao wa mama au kuwalazimisha matumizi ya njia za uzazi wa mpango! Suluhisho ni kuboresha kipato na maisha yao na kuwapa elimu. The question of family planning linakuja automatically when you improve people's lives and educate them. Kwa hiyo ni wajibu wa serikali kuhakikisha inapanga na kutekeleza programu mbalimbali zenye lengo la kunyanyua kipato cha watu (kutoka hicho cha 2$ a day) ili kukidhi mahitaji yao ya chakula na elimu. Vile vile kuboresha Huduma za afya hasa maeneo ya vijijini kwa kujenga zahanati na hospitali ili kupunguza vifo hasa vya akina mama wazazi na watoto wadogo wa chini ya miaka mitano.

Impact ya change in population ni generational ! Tunaweza farijika leo kwa kupunguza uzazi wa kina mama kwa kutumia contraceptives matokeo yanakuja baadaye sana wakati sisi hatupo tena kama vile uhaba wa nguvu kazi. Population inatabia ya kujicheck yenyewe, baadhi ya wanazuoni kama Thomas Malthus aliwahi andika ya kwamba hata vita na magonjwa ya mlipuko kama kipindupindu ambayo huua watu wengi sio laana bali mpango wa mungu wa kudhibiti ongezeko la watu alivyoona yeye. Hata ukame na njaa yeye alisema ni natural check ya population, kwa hiyo ni suala la mtazamo tu na kuchukua njia sahihi ambayo haina madhara mbeleni karne zijazo.
 
This a shame to our nation, yoyote angesema lkn asingekua Raisi wetu, inaonyesha Raisi kwamba hana international exposure.
Nonsense. Unafahamu kwamba sera ya chama tawala nchini marekani The Republicans inakataza uzazi wa mpango? Au kwa vile Rais mweusi wa nchi ya kiafrika kasema mawazo yake kuhusu birth control ndo imekuwa "shame on your country"? Shame on you.
 
Umewahi ishi au tembelea kijijini na ukaona maisha ya watu wanaozaa bila mpango .watoto sita chumba kimoja mlo nusu kwa siku na mzazi anawaficha wasiguse shule? Zaeni kama simbilisi Jiwe atawasomesha na kuwanunulia mpaka pedi
Sio tu kutembelea! Nimekaa kijijini miaka mingi tuu na usemayo sio mageni kwangu ! Suluhisho sio kuwafunga vizazi hao wa mama au kuwalazimisha matumizi ya njia za uzazi wa mpango! Suluhisho ni kuboresha kipato na maisha yao na kuwapa elimu. The question of family planning linakuja automatically when you improve people's lives and educate them. Kwa hiyo ni wajibu wa serikali kuhakikisha inapanga na kutekeleza programu mbalimbali zenye lengo la kunyanyua kipato cha watu (kutoka hicho cha 2$ a day) ili kukidhi mahitaji yao ya chakula na elimu. Vile vile kuboresha Huduma za afya hasa maeneo ya vijijini kwa kujenga zahanati na hospitali ili kupunguza vifo hasa vya akina mama wazazi na watoto wadogo wa chini ya miaka mitano.

Impact ya change in population ni generational ! Tunaweza farijika leo kwa kupunguza uzazi wa kina mama kwa kutumia contraceptives matokeo yanakuja baadaye sana wakati sisi hatupo tena kama vile uhaba wa nguvu kazi. Population inatabia ya kujicheck yenyewe, baadhi ya wanazuoni kama Thomas Malthus aliwahi andika ya kwamba hata vita na magonjwa ya mlipuko kama kipindupindu ambayo huua watu wengi sio laana bali mpango wa mungu wa kudhibiti ongezeko la watu alivyoona yeye. Hata ukame na njaa yeye alisema ni natural check ya population, kwa hiyo ni suala la mtazamo tu na kuchukua njia sahihi ambayo haina madhara mbeleni karne zijazo.
 
Kwa hiyo unamini Mungu anaruhusu Kipindupindu+vita kwa watu wake sio?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…