Wamezaa kumi ndiyo hawa watoto wao wanakimbilia mjini kuwa mahouse girl na mahouse boy, wengine ndiyo hawa ombaomba. Sasa mtu kama huyu anayeombaomba na watoto watano alikuwa na ulazima gani wa kuzaa? Angefunga kizazi akatulia zake angeonekana hajakamilika? Kama mtu huna uwezo wa kutunza na kuhudumia its better ufe bila mtoto kuzaa its not mandatory. Hata biblia inaposema enendeni duniani mkazaliane haimaanishi kila mtu lazima azae, ndiyo maana kuna manabii na mitume wengi tu walikufa bila watoto.
Huu ni mjadala wa ajabu, maanake unaweza ukajikuta unaunga mkono pande zote za mjadala.
Sasa ngoja nikupe pendekezo. Mimi sipendi kuwa ombaomba, na sipendezwi kamwe kama nchi tuwe ombaomba kwa kila kitu tusaidiwe. Ni lazima kabisa tufike mahali tuseme, sasa basi, tujitegemee kwa yale yaliyo ndani ya uwezo wetu.
Lakini angalia pesa inayoingia nchini kwa madhumuni ya mpango huo wa kupunguza kizazi, ukiwa ni msaada tunaopewa.. Je hiyo hela inaweza kupelekwa kusaidia hao watoto wa mitaani kuliko kuielekeza kwa hawa ambao hawajazaliwa?
Na kwa vile sipendezwi nchi yangu kuwa ombaomba. Je, serikali inaweza kulazimishwa ili iweke mipango ya kuhakikisha kwamba wananchi wake wanaozaa watoto wanaowataka wao watakiwe pia na kuwezeshwa inapobidi, kuwa na uwezo wa kuwahudumia wakisaidiana na serikali? Maana yangu ni kuwa pawe na sera za wazi zinazotutaka kama taifa kulisimamia hili jambo.
Complex social problems that call for solutions through national development strategies.
Tanzania ni nchi kubwa ya kutosha na inao utajiri tosha kuhimili zaidi ya watu million mia moja na zaidi. Bado tupo nusu tu hadi sasa. Ukikataa kuijaza kwa kuzaana sisi kwa sisi, tutasaidiwa kuijaza, tukitaka, tusitake na wahamiaji, haramu au halali, huo ndio ukweli wenyewe.