Thumbs up Mkuu. Kuna watu humu JF huwa wanachangia mada wakiwa hawajaelewa au hata kujisumbua kupata full story behind mada iliyoanzishwa. Kama mtu una akili timamu na umemsikiliza Mheshimiwa alichokisema mwanzo mwisho sidhani kama mtu anaweza kuwa na mawazo mgando kama yanayojionyesha hapa.
Kwa jinsi watu wanavyowahusudu wazungu miaka ijayo ukoloni unaweza kurudi tena tena Africa, maana ni kama kila kitu anachokisema mtu mweupe bila hata kukipima mtu anaruka nacho kama ndio standard of life. Wachina kwa sasa wana mpango wa kuachana na one child policy, mbona hatuwasikii wazungu wakiwakosoa! Ila kwa kua wanajua akili za kiafrika zilivyo jambo lolote likitoka kwetu wanaaamini wakiweka neno tu lazima wenyewe kwa wenyewe tugeukane bila hata kulitafakari.
Na haya maneno aliyoyasema Mh. Rais, kama yangesemwa na kiongozi mwingine wa taifa la ulaya au marekani hawa wanaosema tumeabishwa yamkini ndio wangekua wapiga debe wakuu kisa tu ngozi nyeupe imesema.
"kama unajimudu, na una uwezo wa kutunza na kuihudumia familia yako zaa kadiri uwezavyo" In Mr. President voice.