CNN hires Larry Madowo as Nairobi based correspondent

Ukishagundua mtu ni pumba na kwamba hutamhoji chochote mbona umuite kwenye show in the first place? The aim of the media is to give out news to the general public for consumption. How you give out that news depends on your level of professionalism as a journalist. Hata hapa Kenya hao mapumba as you call them get interviewed and such interviews/shows still get audience. It all boils down to the journalist - knowing what to get from his interviewees and how
 
Those are your opinions. You can't defend them when asked to
 
Tatizo kubwa ninaloliona kwetu ni kuwa hatuna wawekezaji wakubwa kwenye Media..hakuna mtu aliyeserious hata kidogo..Ukiacha Azam ambaye yeye michezo na kuuza kisimbuzi chake ndo kipaumbele chake hawa wengine wapowapo tu siku zinaenda na ndo maana hatuwezi kupata Journalist wenye uwezo mkubwa maana haya makampuni yetu kwanza yanatafuta cheap journalists wasiojua mambo.

=====
IPP hamna kitu.

Sahara imekufa.

Clouds wanafanya mseto usioeleweka kwenye Tv.

Wasafi..tv ya umbea na muziki.

====

Huwezi kulinganisha na standard Media ya Kenya yenye dedicated channel kwa ajili ya habari tu i.e KTN News.. na bado kina Citizen Tv na wengine.
 
Asante [emoji122] [emoji122] [emoji122]
 
Kwa hiyo unanisuta ama? πŸ˜…πŸ˜…πŸ˜…

Leta hoja bro niondolee maumivu mimi 🀣🀣

Hoja zinakupiga ngwara unaleta hisia 😜
Hisia unaleta wewe tunaongelea mtu kupata chance katika CNN moja ya network kubwa kabisa duniani na wale hawaajiri vilaza wewe umeleta issue za siasa sijui Mbowe mara Gas sasa niambie umeni quote wapi nimeongelea siasa hapa. Umeanza kuchanganya mambo wala sio sehemu yake.
 
Na hii ndio hoja yangu wale watu wenye upeo wa kuuliza mambo ya msingi hawapati nafasi ni mara moja tu kwa mimi inawezekana wako wengine ila sijawahi kuona labda ni siku ile Mayala alimrushia maswali magumu JPM na sio uhumu tu maswali ya msingi japo nadhani alikuwa kama mwandishi huru labda angekuwa wa chombo fulani asingeweza na wengi walishtuka siku zile kusikia mtanzania kuuliza katika ile sababu hatujazoea lakini sote tunajuwa baada ya hapo Mayala akapotea. Lakini naamini wako watu wanaweza kusimama na kuuliza kwa nia njema tu lakini swali gumu wapo na uhakika. Ila kila kizuri kinahitaji matunzo. vyombo vya habari au wamiliki wana agenda zao ni kulinda maslahi yao sio habari. Bahati mbaya hatuna media yoyote kwetu wanaoweza kusema wako huru hata gazeti la mwananchi walikuwa kidogo nao kwisha labda huko Raia mwema wako kidogo.
 
Jamaa ni genius. Alianza kufanya kazi KTN akiwa na miaka ishirini. Mimi nikiwa na miaka ishirini nilikuwa nakimbizana na wasichana kwenye kijiji.

Aha haaa
Mzee wa timu mzee wa nyika.

Hiyo sishangai, kuna jamaa yangu mmoja yeye mradi wake ulikuwa kukimbizana na mwanamke kutoka kila kabila. Mwingine Ulaya alitaka kila rangi. Kweli ujana ni kichaa, uzee ni maradhi.
 
Wakenya wanabebwa na lugha. Nahisi hata kwetu ingepewa kipaumbele. Kujua lugha mbili kwa ufasaha si jambo baya.
Sio lugha tu, ongeza kisomo na experience ya mhusika! 🀣 Kazi hazipatikani kwa kujua lugha flani tu...
 
Imekuuma dadeq! 🀣 🀣 🀣
 

Faida ya kuwa na lugha moja kama taifa gani?
 
Duh, wewe ulitoholewa pahali kwa chuki hizi. Hivi kiswahili nikijue kwa undani ili iweje. Lugha sio moja duniani, soma akili ipanuke uache kubobokwa ovyo!
 
Faida ya kuwa na lugha moja kama taifa gani?
Ni utambulisho wa mtanzania, mkenya akiingia Tanzania the moment he she opens the mouth every one knows huyu sio mtanzania, the same to any national

Hiyo ni faida kubwa sana ya kuwa na lugha yetu ya swahili
 
Wakenya wanabebwa na lugha. Nahisi hata kwetu ingepewa kipaumbele. Kujua lugha mbili kwa ufasaha si jambo baya.

Acha kusema wakenya wanabebwa na lugha, ni connection na urafiki... ile kitu unahitaji ni urafiki, connection na masomo. Ukipata hizo najua utasaidika kiwewe.
 
Hamna kitu, wachambuzi hakuna points za muhimu mnaweza rusha, sababu ya kuogopa serikali yenyu, haha eti msifungiwe vituo vya habari. Vipi mkuu, ka mtu hafanyi kazi yake, ni aulizwe live si kutoleana meno hapo kwenye runinga.
 
Ni utambulisho wa mtanzania, mkenya akiingia Tanzania the moment he she opens the mouth every one knows huyu sio mtanzania, the same to any national

Hiyo ni faida kubwa sana ya kuwa na lugha yetu ya swahili
Hicho kiswahili ukiwa ughaibuni ukizungumza tu, unaulizwa vipi we mkenya... Haha alafu kama vipi hatukizimii sana vile, kaeni nacho tu! 🀣
 
Ni utambulisho wa mtanzania, mkenya akiingia Tanzania the moment he she opens the mouth every one knows huyu sio mtanzania, the same to any national

Hiyo ni faida kubwa sana ya kuwa na lugha yetu ya swahili
Sababu ya kuwa na lugha moja ni ju ya wakenya ama ni sifa gani munatafuta kwa hii dunia?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…