CNN ni sehemu ya CIA: Mtazamo wao kuhusu Serikali yetu ni mtazamo wa Jumuiya ya Kimataifa. Tusiwapuuze!

Yaani yule profesa mchambuzi pale CNN kaongea kila kitu tena very clear kwa kila kinachotokea katika nchi yetu
 
Mkuu CNN ni kituo cha tv ambacho kipo kimaslahi zaidi na kilitumika kwa kiasi kikubwa katika kampeni za urais wa Marekani dhidi ya Donald Trump
Mkuu CNN wapo biased sana katika kuripoti mambo ya human rights ukichukulia masuala ya Palestine kwa hiyo haiaminiki sana. Kuhusu mahusiano ya serikali ya awamu ya sita na nchi za magharibi Chadema wasitegemee kupata support yeyote kwani mahusiano yameimarika sana hata leo tumeona serikali Marekani ikiikabidhii chanjo za covid 19 kwa Waziri wa Afya wa Tanzania masuala ya human rights serikali ya awamu ya 6 kwa kipindi kifupi imeonyesha mabadiliko makubwa mpaka Chadema wameshtuka kuona umaarufu wao unaanza kushuka kwa kasi mpaka wakaja kuanzisha vurugu za kudai katiba mpya.
Mbowe alifanya ziara Tanzania nzima lakini mapokezi aliyopata yalikuwa madogo sana. Sasa Tundu Lissu, Mbowe na Maria Sarungi kukimbilia hizi main stream media kama CNN haiwezi kuwasaidia wanatakiwa wawe nasubira kama Rais Samia Suluhu Hassan alivyoahidi atashughulikia masuala ya katiba baada ya kujenga uchumi baada ya taifa kuathirika kwa kiasi kikubwa kiuchumi kwa ajili ya janga la Covid19
 
Mama samia,, wewe ni Muisilamu wakweli, una imani, huluma, na rais wa wanyonge. Hebu tenda haki,pitisha hii katiba mpya.
 

Mkuu Mbona mnakuwa na mawazo ya ajabu mkuu?

Mikutano ya Kisiasa ni haki ya Kikatiba. Kwa nini inazuiliwa na wanaruhusiwa CCM tu?
Kusanyiko ni haki ya kikatiba pia.

Uhuru wa maoni na mijadala ya kisiasa ni haki pia ya kikatiba . Mbona zinavunjwa. Nani anavunja na haya ni Maagano kati ya watwaliwa na watawala?

Halihitaji Nani kuahidi ni au nini?. kwa nini aahidi wakati katiba imeruhusu haya Mambo?

Nchi inaongozwa na nini kama si katiba?. Kilichompa mama Uraisi ni nini kama siyo Katiba?. SASA kwa nini vifungu vingine vinaminywa, na kubiruhusu ionekane kama hisani?
 
Ku-calculate impact ya kitu unachotaka kukifanya, inahitajika uwe na akili. Hawa wa kwetu hawana huo uwezo.
 
Hawa jamaa
Hawa jamaa walichangia sana kumwangusha Trump,itakuwa huyu wa Unguja,Sirro na Mabeyo!
 
Kweli kuwa na mikutano ni haki zao za kikatiba lakini lazima serikali iangalie mikutano hiyo itakuwa na madhara gani kwa taifa letu kwani lugha za viongozi waandamizi wa Chadema akiwemo Mbowe zimeonekana ni tishio kwa usalama wa taifa mfano Mbowe kumuita Mkuu wa Wilaya ya Ilemela Mpumbavu ilikuwa sahihi ? Chadema wafanye siasa za kistaarabu watoke kwenye siasa za Radical Politics.
 
Yaani yule profesa mchambuzi pale CNN kaongea kila kitu tena very clear kwa kila kinachotokea katika nchi yetu
Nimemsikiliza mpaka nikakundua kuna watu wanaijui nchi yetu kuliko hata sisi watanzania wenyewe.
 
Hakuna mtu niliamini atatutoa jalalani kama huyu mama. Yaani ameamua kutupeleka tabata dampo kabisa. Ngoja nisimalize maneno yote.
 
Mkuu mpaka sasa serikali ya awamu ya sita ipo kwenye right track kwenye masuala ya uchumi ingawa kuna wahuni wachache wanajaribu ku tarnish ama kuchafua jina la serikali kwa manufaa zao kisiasa. Rais Samia Suluhu huu ni mwezi wa 4 toka achukue madaraka na unakumbuka jinsi serikali ya awamu ya 5 ilivyoharibu mahusiano yetu na jumuiya za kimataifa, kazi kubwa serikali ilichofanya ni kurudisha confidence kwa hawa jamaa na kwa kiasi kikubwa imefanikiwa leo wakulima wa Tanzania wanauza mazao kwa nchi jirani bila shida. Nilitegemea kipindi cha mwanzo wa utawala wa serikali ya awamu 6 vyama vyote vitaunga mkono juhudi lakini leo tunaona mambo ya kihuni yakifanyika na lugha za kibabe na dharau.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…