CNN, Sky news, Aljezeera, BBC, New York Times, Daily Mail, CBS, DW, Finacial Times vyaunga mkono hotuba ya Magufuli kuhusu Test kits

CNN, Sky news, Aljezeera, BBC, New York Times, Daily Mail, CBS, DW, Finacial Times vyaunga mkono hotuba ya Magufuli kuhusu Test kits

Huu usemi wa vya bure vina gharama inaweza kuwa na ukweli, hivi kwa nini hatukununua hizi kits toka mataifa yanayojielewa? au ndiyo tuliogopa kufanya kazi na MABEBERU?
 
Msimamo usioyumbishwa! Hiyo ndiyo picha aliyoitengeneza Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwenye vyombo vya habari vya kimataifa, baada ya kueleza waziwazi mashaka yake juu ya mashine zinazotumika kupima sampuli za wagonjwa wa Corona.

Akizungumza kutokea Chato, mkoani Geita wakati wa hafla fupi ya kumwapisha Waziri wa katiba na Sheria, Mwigulu Nchemba, Rais Magufuli alieleza wasiwasi wake juu ya mashine hizo huku akitolea mfano jinsi sampuli kutoka kwenye papai, mbuzi na ndege aina ya kware zilivyotoa majibu kuonesha kwamba wahusika wana maambukizi ya Corona.

Kauli yake hiyo, imeripotiwa na vyombo vikubwa vya habari duniani, kuanzia televisheni za BBC, DW, CBS, VOA, AL Jazeera, Sky News, CNN na kadhalika, huku magazeti ya New York Times, Financial Times, Daily Mail, The Guardian, Times of India yakiipa uzito habari kuhusu alichokizungumza.

Shirika la Habari la Reuters, nalo pia limeiripoti habari hiyo kwa ukubwa katika vyombo vyake mbalimbali, na kuzidi kuifanya hotuba ya Magufuli kuwa mjadala unaoumiza vichwa vya wanasayansi duniani kote kuhusu ubora na ufanisi wa vifaa vinavyotumika kupima Corona duniani kote.

Vyombo hivyo vya kimataifa, ambavyo mara kwa mara hushutumiwa kuandika habari mbaya pekee kutoka barani Afrika, safari hii vimejikuta vikiizungumzia habari ya hotuba ya Rais Magufuli kwa uzuri kwa sababu alichokibaini kuhusu ufanisi wa mashine hizo, kinahitaji mjadala mpana wa kitaalamu.

Katika hafla ya kumwapisha Mwigulu, Rais Magufuli alieleza jinsi sampuli kadhaa zilivyopelekwa kwenye Maabara Kuu ya Taifa, bila ya wataalamu wa maabara hiyo kujua kuwa si za binadamu, kisha majibu yakatoka kwamba sampuli hizo zilizokuwa zimepewa majina ya binadamu, zilikuwa na Corona wakati kiuhalisia zilikuwa ni sampuli za papai, ndege kwale pamoja na mbuzi.

“…Papai lile lipo halijafa linaiva tu. Mbuzi yule yupo tu hajafa, fenesi lile lipo tu labda lije kuoza… kwa hiyo natoa wito kwa Watanzania msiwe na hofu…mbona mafua yamekuwepo lakini haya ni makali, nayo yatapita…,” alisema Rais Magufuli katika hotuba yake aliyoitoa katika hafla hiyo.

Vyombo hivyo vimeendelea kumnukuu Rais Magufuli akisema: “…Lazima ugundue kuna mambo ya ajabu yanafanyika nchi hii. Ama wahusika wa maabara wamenunuliwa na mabeberu, ama hawana utaalamu jambo ambalo si kweli kwa kuwa maabara hii imetumika sana katika magonjwa mengine. Ama zile sampuli zinazoletwa maana vifaa vyote vinatoka nje, hivyo lazima kuna kitu fulani kinafanywa.”

Rais Magufuli, ambaye hadi sasa anatajwa kuwa rais kutoka nchi za Kiafrika anayeheshimika duniani kote kutokana na kuwa na misimamo isiyoyumbishwa, alisema kutokana na taarifa hizo anaamini kuna watu ambao walipewa majibu yasiyo sahihi kwamba wameambukizwa Corona wakati si kweli na kuongeza pengine kuna waliopoteza maisha kwa sababu ya hofu.

Rais Magufuli pia alivishutumu vyombo vya habari vya kimataifa kwa namna vinavyoripoti kuhusu janga hilo nchini Tanzania licha ya kuwa vyombo hivyo vipo katika maeneo ambayo yameathirika na ugonjwa huo kuliko hata Tanzania

Upo sawa maana una exercise haki yako ya free speech
 
Basi wambieni hao mabeberu wawape hela.
Yaani nchi zote zimeshepewa pesa ndefu na IMF na WB, hadi Togo Malawi mpaka Sudani. Somali watapewa pia. Ila nyie hampewi kwa sababu ya ukaidi wa magu.
Ni very secretive kama North Korea.. hakuna mwandishi anayereport kuhusu korona wala kuhusu hali ya Hospital. Its nonsense. Yaani JK hatutakuja kukusamehe kwa kutuletea hili likiazi
 
Hujielewi. Unajua equipments ngapi zimerudishwa China ziko FAULTY? Let be legitimate si kutukana tuu all the time. UK government waliacha kutumia Chinese testing kits, US nao walirudisha so Magufuli might be right.
Jamaa kaona Corona is out of control, mambo shaghalabagala kaamua kutupa zigo kwa wengine, kama ilivyokuwa issue ya Korosho ndivyo hii itakavyokuwa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ni jambo la heri,hata kama una nguvu ndogo za kiuchumi ,lakini unatakiwa ujiamini kwa kile unachokiamini na kujua kuwa hakiko sawa......
 
Jeshi kubwa la mbowe ni viwavi walionyuma yake huku wakijificha nyuma ya mgongo wa mabadiliko,hakika hawataweza chini ya jemedali mkuu mheshimiwa jpm na serikali yake

Hakika viwavi wenye uchu na raslimali zetu kama taifa wamekwama na watapata tabu sana,
Mungu ibariki Tanzania bariki viongozi wa serikali yetu dhidi ya viwavi wa raslimali za nchi yetu
Mtaji Mkubwa wa Magufuli ni Jeshi Kubwa la Wajinga lililopo nyuma yake!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Jeshi kubwa la mbowe ni viwavi walionyuma yake huku wakijificha nyuma ya mgongo wa mabadiliko,hakika hawataweza chini ya jemedali mkuu mheshimiwa jpm na serikali yake

Hakika viwavi wenye uchu na raslimali zetu kama taifa wamekwama na watapata tabu sana,
Mungu ibariki Tanzania bariki viongozi wa serikali yetu dhidi ya viwavi wa raslimali za nchi yetu

Sent using Jamii Forums mobile app
Mwingine huyu imempenya toboni....
 
Vyombo kama Uhuru kusifia kazi inayofanywa na mataifa ya Magharibi au kuwaaminisha wannchi kwamba mzungu kasema hivi mara kasema hivi ni kukinzana na msimamo wa Rais dhidi ya mabeberu.

Account za tweeter na mitandao ya kijamii yamejaa taarifa za kuwaaminisha Watanzania kuwa mabeberu wamesifia Tanza nia kitu ambacho ni kinyume kabisa na ukweli uliopo Duniani. Kwanini tusimame na hotuba ya Rais? Kwanini kama tunaiamini tusiisambaze? Hadi leo uone gazeti au media ya ndani iliyochambua hotuba yake ,wote tunaripoti wenzetu wanavyofanya Tena tukiwakosoa na kuwasifia ila kwetu hakuna anayekosoa.

Mfano mdogo, Marais wa Afrika walifanya vikao wiki iliyopita ambapo Tanzania hatukushiriki, katika mkutano ule moja ya Jambo lilokubaliwa ni kujaribu kutumia dawa ya Madagasca kukabiliana na korona, hii habari imetangazwa na media zote. Leo hii vyombo vyetu vinadai marais wa Africa waungana na Rais Magufuli kutumia dawa ya Madagasca, media hizo hizo zinasau ziliripoti Nini last week before hotuba ya Magu.

Jambo la pili lakusikitisha, Nchi zote zilizofunga mipaka zilieleza wazi kwamba zinafunga mipaka kwa siku kadhaa kuangalia ukubwa wa tatizo kabla yakufungua mipaka, zilieleza wazi watu watafungiwa kutembea kwa siku kadhaa na hii ipo wazi na mkakati wa mataifa mengi Dunian, baadhi ya nchi zimeanza kufungua mipaka na kuwaruhusu watu kutoka nje...media zetu zinaandika Mataifa mengi yaunga mkono msimamo wa Tanzania wa kutofunga mipaka. Kwa maslahi ya Nani?

Shule ufaransa zimeanza kufunguliwa ila kwa idadi ya wanafunzi wachache kufikia 6 hadi 15 kwa darasa, huku kwetu ambapo tuna darasa la wanafunzi mia napo usishangae tukafungua shule bila taadhari yoyote.

Haya yote yanafanywa na kuripotiwa na media zetu kinyume Cha uhalisia, media zetu zinaripoti zaidi kuhusu Magharibi na mataifa mengine kuliko zinavyoeleza Tanzania kimkakati.

Media houses kuweni waadilifu na siyo waoga
 
Hao mabeberu wametuibia sana ,

Tukiwadai wakichotuibia watabaki na mabarafu tu mali zote zitarudi Africa
 
Msimamo usioyumbishwa! Hiyo ndiyo picha aliyoitengeneza Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwenye vyombo vya habari vya kimataifa, baada ya kueleza waziwazi mashaka yake juu ya mashine zinazotumika kupima sampuli za wagonjwa wa Corona.

Akizungumza kutokea Chato, mkoani Geita wakati wa hafla fupi ya kumwapisha Waziri wa katiba na Sheria, Mwigulu Nchemba, Rais Magufuli alieleza wasiwasi wake juu ya mashine hizo huku akitolea mfano jinsi sampuli kutoka kwenye papai, mbuzi na ndege aina ya kware zilivyotoa majibu kuonesha kwamba wahusika wana maambukizi ya Corona.

Kauli yake hiyo, imeripotiwa na vyombo vikubwa vya habari duniani, kuanzia televisheni za BBC, DW, CBS, VOA, AL Jazeera, Sky News, CNN na kadhalika, huku magazeti ya New York Times, Financial Times, Daily Mail, The Guardian, Times of India yakiipa uzito habari kuhusu alichokizungumza.

Shirika la Habari la Reuters, nalo pia limeiripoti habari hiyo kwa ukubwa katika vyombo vyake mbalimbali, na kuzidi kuifanya hotuba ya Magufuli kuwa mjadala unaoumiza vichwa vya wanasayansi duniani kote kuhusu ubora na ufanisi wa vifaa vinavyotumika kupima Corona duniani kote.

Vyombo hivyo vya kimataifa, ambavyo mara kwa mara hushutumiwa kuandika habari mbaya pekee kutoka barani Afrika, safari hii vimejikuta vikiizungumzia habari ya hotuba ya Rais Magufuli kwa uzuri kwa sababu alichokibaini kuhusu ufanisi wa mashine hizo, kinahitaji mjadala mpana wa kitaalamu.

Katika hafla ya kumwapisha Mwigulu, Rais Magufuli alieleza jinsi sampuli kadhaa zilivyopelekwa kwenye Maabara Kuu ya Taifa, bila ya wataalamu wa maabara hiyo kujua kuwa si za binadamu, kisha majibu yakatoka kwamba sampuli hizo zilizokuwa zimepewa majina ya binadamu, zilikuwa na Corona wakati kiuhalisia zilikuwa ni sampuli za papai, ndege kwale pamoja na mbuzi.

“…Papai lile lipo halijafa linaiva tu. Mbuzi yule yupo tu hajafa, fenesi lile lipo tu labda lije kuoza… kwa hiyo natoa wito kwa Watanzania msiwe na hofu…mbona mafua yamekuwepo lakini haya ni makali, nayo yatapita...,” alisema Rais Magufuli katika hotuba yake aliyoitoa katika hafla hiyo.

Vyombo hivyo vimeendelea kumnukuu Rais Magufuli akisema: “…Lazima ugundue kuna mambo ya ajabu yanafanyika nchi hii. Ama wahusika wa maabara wamenunuliwa na mabeberu, ama hawana utaalamu jambo ambalo si kweli kwa kuwa maabara hii imetumika sana katika magonjwa mengine. Ama zile sampuli zinazoletwa maana vifaa vyote vinatoka nje, hivyo lazima kuna kitu fulani kinafanywa.”

Rais Magufuli, ambaye hadi sasa anatajwa kuwa rais kutoka nchi za Kiafrika anayeheshimika duniani kote kutokana na kuwa na misimamo isiyoyumbishwa, alisema kutokana na taarifa hizo anaamini kuna watu ambao walipewa majibu yasiyo sahihi kwamba wameambukizwa Corona wakati si kweli na kuongeza pengine kuna waliopoteza maisha kwa sababu ya hofu.

Rais Magufuli pia alivishutumu vyombo vya habari vya kimataifa kwa namna vinavyoripoti kuhusu janga hilo nchini Tanzania licha ya kuwa vyombo hivyo vipo katika maeneo ambayo yameathirika na ugonjwa huo kuliko hata Tanzania.

Hasta la victoria siempre
 
Hili nalo nijambo la kushangaza dunia lakini ngoja na wao wapime mapapai na mbuzi zao tuone watatoa majibu gani Positve au negative?
 
Haoo chini wameonyesha mtazamo wao kuhusu critisism and secretive iliyo nayo tanzania,eti rais wao amewaambia waiombee corona iondoke,na wao wamashangilia!! Its more than illiterate,more than ignorance,sheer stupidity we can call.
Ameona sisi hatujui lugha ya malkia eti anaweka mawazo yake kana kwamba ndo tafsiri ya kilichosemwa/andikwa. Kaniudhi sana
 
India iliwahi ku cancel order ya vifaa hafifu vya kupimia corona toka China. Kama vyetu ni msaada wa China basi tatizo linajulikana. Niliwahi kuona kuwa nchi ya Senegal ina njia rahisi na aminifu ya kutest corona, vile vile wanatengeneza ventilator za bei rahisi sana.

Ninachotaka kusema ni kuwa baada ya kushambulia hivyo vifaa dhaifu tunafanya nini? Ingependeza kama tungejivunia na kutembea kifua mblele kwa kutengeneza vya kwetu na kuachana na misaada hovyo. Bila hivyo hata tukitangazwa sana kwenye hivyo vyombo vya habari, matatizo yetu yatabaki pale pale.
 
Back
Top Bottom