Coach Ramovic nitakukupopoa hadi utakapobadilika.
Mimi kama mtaalam wa football na mwanachama wa Yanga bado Ramovic hajanishawishi Kwa mbinu zake
Leo ameanza na mabeki 5 nyuma Bacca, Job, Boka, Kibwana na Israh,
Hii mbinu imenishangaza, kocha aliamua kujilinda sana dhidi ya Kagera sugar?
Hakuna kama Kagera sugar ingekuja kama second team kujilinda? Kagera sugar ilibaki nyuma ya mpira na wewe uwe na walinzi wengi utawafungaje?
Alifanya mechi iwe ngumu first half bila sababu yoyote.
Mudathir ametumika sana unaona kabisa maamzi yake na pasi nyingi zinapotea kwanini asingempumzisha?
Bench una Chama, Pacome, Max, Ikangalombo Bado unaanza na mabeki 6 dhidi ya Kagera sugar?
Eng Hersi Kwa huyu Ramovic ulijichanganya?
Timu inacheza kama haina coach yaani kama timu ya mtaani, hatuoni mbinu za Mwalimu ni vipaji vya wachezaji vinaamua mechi
Eng Hersi ingia sokoni mlete Coach mwenye CV iliyoshiba
Yanga bingwa