Cocochanel live interview on DJ sepetu show!!

Hapana mimi ni Cocochanel tu.
Nimetoka kuangalia siku za kujiunga naona zina utofauti mkubwa na haziendeani na shutuma yako pia.
Okay dear sio kama nakushutumu..la!! Nilitaka tu kujua maana naye alikua machachari kama wewe...[emoji5] [emoji6]
 
Kumbe ndio maana unaipenda serikali......
 
....Huyu ndo anauliza maswali wengine wote wanaongozwa na emotions tu!
 
Kwako DJ Sepetunga, nimependa idea yako ya kuendesha interview kwa wanajamii forums. Lakini kwa mtazamo wangu naona huna huwezo wa kuendesha interview, una maswali mengi yasiyo na msingi. Unauliza watu maswali ya hovyo, una dominate interview sana . Yaani mpaka interview inaisha mtu makini hawezi kuona hasa malengo ya interview. Hebu kaka uwe unauliza maswali makini, na si haya ya hivyo.

Kindikwili from Ntwara
 

Najivunia mengi kwa sababu ya kujitahidi kujiongeza na mapya yake yanayojiri. Ndio nimeshawahi na pia kupelekea kufanyika project kubwa na zingine.

2: Jina lako cocochanel kama sijakosea ni la yule mwanamitindo (fashion designer) wa ufaransa kipindi hicho.. Je ni role model wako?? Nini kilikuvutia hadi ukatumia jina lake kumuenzi??

Napenda perfume za CocoChanel zaidi. nilitaka niandike nizipendazo mfano za Lancome n.k nikapenda hilo jina zaidi.

3: Hapa JF hasa kwenye jukwaa la siasa huwa nakuona kule unalumbana na watu kuhusu Mh. Paul Makonda anapochafuliwa, ni kwa nini? Je una uhusiano wowote na Lumumba? kwa maana watu wanakuita Kada wa Lumumba..

Sina uhusiano wowote na Lumumba na sifanyi kazi za hicho chama. Mimi ni mtu napenda awamu hii ya Mh. Magufuli na pia Mh. Makonda. Nimekuwemo humu miaka 10, na ni awamu hii nimevutiwa sana kuingia kwenye jukwaa la siasa.

Na naamini ana mengi sana anaweza kuongeza kwenye lori lake ili awamu zake ziwe moto moto zaidi na kuacha historia nzuri na kufurahisha wananchi na kusukuma amendeleo nchini. Speed yake ni super

Nilieleza kwenye majibu mengine.. nikiwa mahala lazima ninotiwe kivyovyote vile ni nyota tu niliyojaliwa. Hivyo sishangai kuitwa kada kwa ninayosimamia kwa kuandika humu.. ila vizuri wajue mimi sio kada kwa sasa ila nina kadi tulipewa shuleni sekondari za chama tawala.

Makonda nilianza kumsoma humu tangu habari zake akiwa chuoni na juu ya vyeo vya chuoni.. nikaona ana kitu fulani kwasababu ya yale mashambulizi.. sikushangaa baada akiwa anahusishwa na mengi ya ajabu kusingiziwa kama ilivyo sasa.

4: MIPANGO YAKO KWA MIAKA MITANO IPOJE?

......Nimejitahidi nisijibu kama vile swali la interview ya kazi bali nimejibu kama napiga story nawe kidogo... mengine nimebania shaaa

na swali la mwisho, hobbies na interest zako ni zipi??

Ha ha haaaaaa
Mimi mtu wa kutanua sana kwa kweli napenda kujipa raha.. napenda kusoma habari mbali mbali za duniani zikiwemo za uchunguzi na kujifunza mengi nisiyoyajua ya culture au makabila mengine. Nacheza sana games kwenye devices zangu na muda na wanangu ni muhimu sana kwangu na kuwafundisha mengi hata kuongelea jambo fulani na kuwapa raha tukiwa pamoja nyumbani sana na nje.

........lingine labda kuja kukuongoza siku moja eeeh sema ni kutafuta muda kwa kweli kufanya hayo. Labda ningeshavutiwa kabla kuingia na hadi sasa sijavutiwa kujisukuma.. na labda sitajisukuma. JPM akizidi kunyoosha na kusafisha itavutia wengi wazalendo na wanaoipenda nchi yetu kusukuma usukani.
 

Shukrani sana Cocochanel kwa kunijibu maswali yangu nashukuru sana... Nimeridhika na ulivyojibu, Pamoja sana, endelea kujibu maswali ya wengine..

Uwe na wakti mwema, Asante.
 
JF wote wasanii kula kulala nae unakuta anajifanya ana mbwembwe balaa
 
DJ nilikuwa bussy kufuatilia hii interview ila honestly kabsa mtu wako Leo alikuwa akiulizwa swali anajibu essay yenye content zero
Jitahidi siku nyingne usihoji mtu kama huyu maana amezingu kinoma.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…