Cocochanel live interview on DJ sepetu show!!

Cocochanel live interview on DJ sepetu show!!

Hapana mimi ni Cocochanel tu.
Nimetoka kuangalia siku za kujiunga naona zina utofauti mkubwa na haziendeani na shutuma yako pia.
Okay dear sio kama nakushutumu..la!! Nilitaka tu kujua maana naye alikua machachari kama wewe...[emoji5] [emoji6]
 
Mimi kuna kipindi wazazi walikuwa nje ya nchi nasi kwa miaka michache. na hivyo ilikuwa ngumu sana walipotaka tusome shule za Tanzania.. nikaenda kusoma boarding school niliona kama nitashindwa kumudu na pia kwa kuishi nao mbali.. ila kwa kweli nilipokua niliwaelewa sana pamoja na kuwa na pesa za kutusomesha nje huko au nje ya ulaya n.k. hii kitu siijutii leo hii hasa baada ya kuja kusoma nchi za ulaya baadae.
Ilinifundisha mengi ya maisha na hivyo tangu sekondari hadi leo nikiwa nyumbani kwa wazazi ni kuwatembelea tu tangu warudi nchini miaka sasa.
Unajua ile ya kuwa independent woman basi hiyo najiona nimo
Kumbe ndio maana unaipenda serikali......
 
Cocochanel mimi nina maswali kadhaa...(kama yameshajibiwa utanitaarifu)

1: Umesema wewe unafanya kazi/ fani ya mambo ya teknolojia, Je ni kwa kiasi gani umefaidika na teknolojia na unajivunia nini kuhusu teknolojia..Je ulishawahi kuwaza kuvumbua jambo jipya kuhusu teknolojia mahala unapofanyia kazi au nje ya hapo??

2: Jina lako cocochanel kama sijakosea ni la yule mwanamitindo (fashion designer) wa ufaransa kipindi hicho.. Je ni role model wako?? Nini kilikuvutia hadi ukatumia jina lake kumuenzi??

3: Hapa JF hasa kwenye jukwaa la siasa huwa nakuona kule unalumbana na watu kuhusu Mh. Paul Makonda anapochafuliwa, ni kwa nini? Je una uhusiano wowote na Lumumba? kwa maana watu wanakuita Kada wa Lumumba..

4: MIPANGO YAKO KWA MIAKA MITANO IPOJE??

na swali la mwisho, hobbies na interest zako ni zipi??

Asante
....Huyu ndo anauliza maswali wengine wote wanaongozwa na emotions tu!
 
Kwako DJ Sepetunga, nimependa idea yako ya kuendesha interview kwa wanajamii forums. Lakini kwa mtazamo wangu naona huna huwezo wa kuendesha interview, una maswali mengi yasiyo na msingi. Unauliza watu maswali ya hovyo, una dominate interview sana . Yaani mpaka interview inaisha mtu makini hawezi kuona hasa malengo ya interview. Hebu kaka uwe unauliza maswali makini, na si haya ya hivyo.

Kindikwili from Ntwara
 
Cocochanel mimi nina maswali kadhaa...(kama yameshajibiwa utanitaarifu)

1: Umesema wewe unafanya kazi/ fani ya mambo ya teknolojia, Je ni kwa kiasi gani umefaidika na teknolojia na unajivunia nini kuhusu teknolojia..Je ulishawahi kuwaza kuvumbua jambo jipya kuhusu teknolojia mahala unapofanyia kazi au nje ya hapo??

Najivunia mengi kwa sababu ya kujitahidi kujiongeza na mapya yake yanayojiri. Ndio nimeshawahi na pia kupelekea kufanyika project kubwa na zingine.

2: Jina lako cocochanel kama sijakosea ni la yule mwanamitindo (fashion designer) wa ufaransa kipindi hicho.. Je ni role model wako?? Nini kilikuvutia hadi ukatumia jina lake kumuenzi??

Napenda perfume za CocoChanel zaidi. nilitaka niandike nizipendazo mfano za Lancome n.k nikapenda hilo jina zaidi.

3: Hapa JF hasa kwenye jukwaa la siasa huwa nakuona kule unalumbana na watu kuhusu Mh. Paul Makonda anapochafuliwa, ni kwa nini? Je una uhusiano wowote na Lumumba? kwa maana watu wanakuita Kada wa Lumumba..

Sina uhusiano wowote na Lumumba na sifanyi kazi za hicho chama. Mimi ni mtu napenda awamu hii ya Mh. Magufuli na pia Mh. Makonda. Nimekuwemo humu miaka 10, na ni awamu hii nimevutiwa sana kuingia kwenye jukwaa la siasa.

Na naamini ana mengi sana anaweza kuongeza kwenye lori lake ili awamu zake ziwe moto moto zaidi na kuacha historia nzuri na kufurahisha wananchi na kusukuma amendeleo nchini. Speed yake ni super

Nilieleza kwenye majibu mengine.. nikiwa mahala lazima ninotiwe kivyovyote vile ni nyota tu niliyojaliwa. Hivyo sishangai kuitwa kada kwa ninayosimamia kwa kuandika humu.. ila vizuri wajue mimi sio kada kwa sasa ila nina kadi tulipewa shuleni sekondari za chama tawala.

Makonda nilianza kumsoma humu tangu habari zake akiwa chuoni na juu ya vyeo vya chuoni.. nikaona ana kitu fulani kwasababu ya yale mashambulizi.. sikushangaa baada akiwa anahusishwa na mengi ya ajabu kusingiziwa kama ilivyo sasa.

4: MIPANGO YAKO KWA MIAKA MITANO IPOJE?

......Nimejitahidi nisijibu kama vile swali la interview ya kazi bali nimejibu kama napiga story nawe kidogo... mengine nimebania shaaa

na swali la mwisho, hobbies na interest zako ni zipi??

Ha ha haaaaaa
Mimi mtu wa kutanua sana kwa kweli napenda kujipa raha.. napenda kusoma habari mbali mbali za duniani zikiwemo za uchunguzi na kujifunza mengi nisiyoyajua ya culture au makabila mengine. Nacheza sana games kwenye devices zangu na muda na wanangu ni muhimu sana kwangu na kuwafundisha mengi hata kuongelea jambo fulani na kuwapa raha tukiwa pamoja nyumbani sana na nje.

........lingine labda kuja kukuongoza siku moja eeeh sema ni kutafuta muda kwa kweli kufanya hayo. Labda ningeshavutiwa kabla kuingia na hadi sasa sijavutiwa kujisukuma.. na labda sitajisukuma. JPM akizidi kunyoosha na kusafisha itavutia wengi wazalendo na wanaoipenda nchi yetu kusukuma usukani.
 
Najivunia mengi kwa sababu ya kujitahidi kujiongeza na mapya yake yanayojiri. Ndio nimeshawahi na pia kupelekea kufanyika project kubwa na zingine.

Napenda perfume za CocoChanel zaidi. nilitaka niandike nizipendazo mfano za Lancome n.k nikapenda hilo jina zaidi.

Sina uhusiano wowote na Lumumba na sifanyi kazi za hicho chama. Mimi ni mtu napenda awamu hii ya Mh. Magufuli na pia Mh. Makonda. Nimekuwemo humu miaka 10, na ni awamu hii nimevutiwa sana kuingia kwenye jukwaa la siasa.

JPM nilianza kupenda yake nilipooona kideo kikimuonyesha ameenda sehemu ya kazi na mtu kumdanganya n.k nikaanza kumfatilia. Alipochaguliwa kugombania uraisi nilifurahi sana kama vile ni ndugu yangu kumbe mimi fan wake wa mitandaoni. Na naamini ana mengi sana anaweza kuongeza kwenye lori lake ili awamu zake ziwe moto moto zaidi na kuacha historia nzuri na kufurahisha wananchi na kusukuma amendeleo nchini. Speed yake ni super

Nilieleza kwenye majibu mengine.. nikiwa mahala lazima ninotiwe kivyovyote vile ni nyota tu niliyojaliwa. Hivyo sishangai kuitwa kada kwa ninayosimamia kwa kuandika humu.. ila vizuri wajue mimi sio kada kwa sasa ila nina kadi tulipewa shuleni sekondari za chama tawala.

Makonda nilianza kumsoma humu tangu habari zake akiwa chuoni na juu ya vyeo vya chuoni.. nikaona ana kitu fulani kwasababu ya yale mashambulizi.. sikushangaa baada akiwa anahusishwa na mengi ya ajabu kusingiziwa kama ilivyo sasa.

Kwa kweli nitapenda sana niwe kwenye wimbi la kuona teknolojia imepiga hatua sana nchini hapa. Na kwa sasa ni muda wa kupata nafasi kuingia kwenye mashimo kuyajaza.. nchini hapa kuna mengi sana.. na kujitengenezea pesa pia.. naendelea kusaka muda muafaka niweze kujidumbukiza kizaidi kwenye hayo. Mengine naamini nitakuwa bado happy na maisha yangu kama sasa. Nimejitahidi nisijibu kama vile swali la interview ya kazi bali nimejibu kama napiga story nawe kidogo... mengine nimebania shaaa

Ha ha haaaaaa
Mimi mtu wa kutanua sana kwa kweli napenda kujipa raha.. napenda kusoma habari mbali mbali za duniani zikiwemo za uchunguzi na kujifunza mengi nisiyoyajua ya culture au makabila mengine. Nacheza sana games kwenye devices zangu na muda na wanangu ni muhimu sana kwangu na kuwafundisha mengi hata kuongelea jambo fulani na kuwapa raha tukiwa pamoja nyumbani sana na nje.

Napenda sana kusoma na kujiendeleza kwenye teknolojia niwezavyo hata kujifunza maeneo mengine yanayohusika na business, management ili nijiongeze na kujinyakulia certs nijisikie raha. Mengine naona aibu namezea... lingine labda kuja kukuongoza siku moja eeeh sema ni kutafuta muda kwa kweli kufanya hayo. Labda ningeshavutiwa kabla kuingia na hadi sasa sijavutiwa kujisukuma.. na labda sitajisukuma. JPM akizidi kunyoosha na kusafisha itavutia wengi wazalendo na wanaoipenda nchi yetu kusukuma usukani.

Shukrani sana Cocochanel kwa kunijibu maswali yangu nashukuru sana... Nimeridhika na ulivyojibu, Pamoja sana, endelea kujibu maswali ya wengine..

Uwe na wakti mwema, Asante.
 
c861714d47c73bafbed36682dad10c52.jpg
355424799eab49d173ecd111886ceb39.jpg
Huyu Mzee toka niskie anatoa mtandao pendwa daah
 
JF wote wasanii kula kulala nae unakuta anajifanya ana mbwembwe balaa
 
Back
Top Bottom