Code zinaanza kufunguka

Upumbavu ulio nao ni kwamba unashikilia jmambo tofauti kabisa na unayo ambiwa.
Nani kakwambia hapendi ufanisi wa bandari? Ni wapi ulipo soma nikisema bandari ya Dar es Salaam haitakiwi kuwa na ufanisi?
Unapenda sana kusambaza roho ya chuki, umeikuta Tanzania imejaa wastaarabu na kila unachoanzisha kinakosa kuungwa mkono.
 
Muingereza anazo bandari mbili zinaendeshwa na DPW, sisi tumetawaliwa na muingereza.

Mhindii kaingia mkataba wa kuendesha bandari yake moja na huyo DPW, bado sijaongelea Belgium na kwingineko ambapo yupo huyo mwendeshaji.

Akili za kimasikini na hizi za kudhania mgeni anafaidika na mali yetu bila ya kutazama huyo mgeni analeta ufanisi mkubwa kiasi gani katika shughuli anayoifanya.

Hakuna kuneemeka bila ya nidhamu na kutoka jasho, ukiona wageni wananeemeka kuliko sisi ujue kwamba sisi ni wa hovyo tu katika suala zima la kuendesha taasisi na mashirika yetu.
 
Huijuwi historia yako wewe.

Wewe babu zako waliletwa kutumwa Mashariki ya Afrika, hii ardhi yote kabla ya kuja Mjerumani ilikuwa ni Zanzibar.
Wewe ni mjinga sana wewe, ukiwa kama mtu unayejinasibu kuijua vizuri historia, unawezaje kusema kwamba kabla ya ujio wa watu wa Germany hii ardhi yote ilikuwa ni Zanzibar.?

Hebu kasome kitabu kinaitwa "THE HISTORY OF AFRICA BEFORE 1948" kisha urudi hapa tena kucomment porojo zako.
 
Wewe kama ni mbantu, mashariki ya Afrika ni wakuja tu.

Kasome.
 
Wewe kama ni mbantu, mashariki ya Afrika ni wakuja tu.

Kasome.
Inaonekana najaribu kujadiliana na mtu asiyekuwa na uwezo wa kufanya reasoning zaidi ya kufanya ubishi tu.

Hebu linganisha idadi ya wabantu na ile ya wasio wabantu kwa hapa Afrika mashariki kisha useme akina nani ni wakuja.


Huyo Abed Amani Karume nwenyewe asili yake ni msumbuji hapo, uhuru wa Zanzibar wenyewe main strategists na waongoza harakati walikuwa Wabantu pure.


Utayajulia wapi ikiwa elimu pekee mmepewa ni ile ya kwenye mikeka?
 
Unafata hisia, hufati ukweli. Si kila mwenye rangi nyeusi ni mbantu.

Unaonesha hata ubantu huuelewi ni nini.

Soma kijana.
 
948 si juzi tu kijana? Soma kijana usiwe mvivu kusoma. Usinhgojee kila kusomea na kujazwa ujinga tu.
 
Unapenda sana kusambaza roho ya chuki, umeikuta Tanzania imejaa wastaarabu na kila unachoanzisha kinakosa kuungwa mkono.
Sasa hapa wewe unamsemea nani hasa! Unataka nisiwachukie mnao liangamiza taifa letu?

Ni nani mwenye roho ya chuki kama siyo nyinyi mnaotafuta kuwafanya waTanzania wawe watwana zenu. Hivi unazo akili za kufikiri sawasawa wewe?

Ndiyo, Tanzania imejaa wastaarabu na sifa hiyo ndiyo mnayo itumia nyinyi kuwadhalilisha. Kila siku mnaimba kwa hadaa na ulaghai mkubwa; "amani amani" wakati matendo yenu yakifanya kinyume kabisa na kujenga hiyo amani ambayo waTanzania wamekuwa nayo miaka yote.

Nyinyi ndio mnaoleta uhasama ndani ya jamii ya waTanzania, hapo patakosekana chuki vipi!
 
Muingereza anazo bandari mbili zinaendeshwa na DPW, sisi tumetawaliwa na muingereza
Ni mara ngapi umerudia rudia haya maneno humu, nami kukueleza kwamba Mwingereza hategemei bandari moja kama tulivyo sisi; na kwamba Mwingereza hakushindwa kuendesha bandari hizo kwa kuwa hana ujuzi kama tulivyo sisi; lakini kwa vile akili imelala huwezi kutambua hilo.
Kwani Mwingereza akifanya na sisi ni lazima tufanye, tena bila ya kuelewa kwa nini Mwingereza anafanya hivyo? Ni 'mentality' hii ndiyo inayonifanya nikudharau sana wewe na huyo mama yako.
Hukuanza leo kuwadharau waTanzania kwa kuwaita wavivu, wezi na mambo mengine ya kipuuzi kabisa, kwa vile tu nyinyi mnajichukulia kuwa mnayo asili ya huko kwingine.
Ni akili hii inayo wafanya nyinyi muwe maadui wakubwa wa waTanzania, kwa sababu kila mnalo fanya ni kuwadidimiza badala ya kuwafanya wawe watu wanao amini kuwa wana uwezo mkubwawa kufanya kila wanalofanya watu wengine kote duniani.

Badala ya kufanya kazi ya kuwaongoza hawa waTanzania wajenge uwezo wao huo, nyinyi mnageuka na kufanya kila njia ya kuwafanya wajione hawana uwezo ili muendelee kuwafanya watwana wenu na hao mnaowagawia maliasili zetu wakati huu.
, huu ni uongozi wa namna gani huu! Unaipeleka nchi wapi?

Ninaamini mtakomeshwa tu.
Unapo elezwa kwamba tatizo si huko kuwekeza toka nje; akili yako imedumaa haiwezi kamwe kubadilika. Umepewa mifano chungu nzima hapa kukuonyesha ujinga wa mnayo fanya. TICTS wamekaa Bandarini miaka zaidi ya 25; mlipoona hamuwezi kupata hongo za kutosha kutoka kwao, mka waondoa, mkaleta mjomba katika njia za kiovu kabisa; naye atakaa hapo zaidi ya miaka 30, wakati huo Tanzania bado ipo na misukule yake isiyoweza kujifunza chochote katika muda wote huo; kwa sababu akina Samia dira yao iliwaonyesha waTanzania hawana uwezo wa kufanya chochote!
Swissport hivyo hivyo. Mapori yetu, hata kupanda misitu tu, mnaona waTanzania hawawezi
 
Hizi nadharia ni za humu humu JF uhalisia wa ufanisi wa mtanzania ni mbovu siku zote.

Mtanzania mwizi anapopewa ofisi, mvivu anapopewa kuendesha taasisi, anapenda mno majungu na fitina.

Mtanzania anataka afanye kazi yenye thamani ya shilingi milioni moja lakini anataka mshahara wa milioni tano, hana uhalisia wa mipango yake na hicho anachoweza kukipata kutokana na kazi yake.

TPA ulijaa wizi na kila aina ya ufisadi na kila anayetaka kuwekeza anapigwa vita na hao hao mafisadi wenye kula bila kuvuja jasho.

Swissport yupo hapo Airport kwa miaka 30 kuna ubaya gani DPW akiendesha bandari yetu kwa mkataba wa miaka 10 mpaka 15?.

TUmechezea elimu matokeo yake tunaishia kulialia kwa kuchanganyikiwa kwetu, dunia hii sio lelemama ukilemaa umeachwa hapo hapo na wanaokuzunguka wanazidi kupiga hatua za kimaendeleo.
 
Hizi nadharia ni za humu humu JF uhalisia wa ufanisi wa mtanzania ni mbovu siku zote.

Mtanzania mwizi anapopewa ofisi, mvivu anapopewa kuendesha taasisi, anapenda mno majungu na fitina.

Mtanzania anataka afanye kazi yenye thamani ya shilingi milioni moja lakini anataka mshahara wa milioni tano, hana uhalisia wa mipango yake na hicho anachoweza kukipata kutokana na kazi yake.

TPA ulijaa wizi na kila aina ya ufisadi na kila anayetaka kuwekeza anapigwa vita na hao hao mafisadi wenye kula bila kuvuja jasho.

Swissport yupo hapo Airport kwa miaka 30 kuna ubaya gani DPW akiendesha bandari yetu kwa mkataba wa miaka 10 mpaka 15?.

TUmechezea elimu matokeo yake tunaishia kulialia kwa kuchanganyikiwa kwetu, dunia hii sio lelemama ukilemaa umeachwa hapo hapo na wanaokuzunguka wanazidi kupiga hatua za kimaendeleo.
 
TPA kuna waendeshaji wawili, DPW na Adani wameingiza mabilioni ya pesa na wanaongeza ufanisi kila kukicha.

Tanzania imekuwa ikiangamazwa miaka na miaka kabla hata Samia hajaingia kwenye siasa za vyama, wanaoiangamiza baadhi yao ni hao hao wanaoupinga uwekezaji wa DPW na Adani, wamo humo serikalini.

Kujifanya mzalendo sana sio kigezo cha kuwa mkweli kwa taifa lako.

Ufisadi upo na ushahidi ni reports zinazotolewa na wakaguzi wakuu wa serikali kuanzia zile za Ludovick Utoh mpaka hizi za Kichere, kila siku zinajaa uchafu wa taasisi zetu.

Wanaoziongoza hizo taasisi zenye kutoa taarifa chafu ndio hawa wanaopinga uwekezaji wa DPW na Adani, ni unafiki mtupu.
 
Hizi nadharia ni za humu humu JF uhalisia wa ufanisi wa mtanzania ni mbovu siku zote.
Haya sasa; nyinyi msio waTanzania ndio mtakao waletea waTanzania ufanisi au kwenu kuwaweka kuwa watwana zenu ndilo suluhisho?
Unaendelea kuonyesha ni kiasi gani ulivyo na akili mbovu kabisa. Na ni hivyo hivyo alivyo na Samia mwenyewe.

Enzi hii unaweza wewe kujiona kuwa ni bora zaidi ya binaadam mwingine, kweli?
Mtanzania mwizi anapopewa ofisi, mvivu anapopewa kuendesha taasisi, anapenda mno majungu na fitina.
Na ulivyo mpuuzi kabisa; hata hujui kwamba nyinyi haya mnayo fanya hapa ndio wizi mkubwa.
Nitajie nchi yoyote hapa duniani ambayo watu wake siyo wezi? Huko kwa wajomba zenu hakuna wizi. Siyo wavivu wa kupindukia wale; tena watu duni kabisa?
Sasa mtu kama wewe huelewi kwamba kila nchi ina sheria na taratibu za kubana yote hayo ya wizi. Badala ya kuongoza nchi iondokane na tabia hizo, Samia sasa ndiyo anatuletea majizi ya kila aina. Kawapata vikaragosi, akina Hamza Johari na akina Kafulila wa kutekeleza maovu hayo. Sasa wanaimba waTanzania ni wezi , wavivu!

Nenda China ukaibe kama utasalimika; lakini wachina wanapo kuja hapa wanaiba!
 
Tatizo lako huelewi unacho zungumzia. Msukumo wa kuwaibia waTanzania ndio ulio kujaa kichwani kiasi kwamba huwezi kuelewa jambo jingine lolote.

Maandishi yako hapa yanaonyesha wazi kabisa ulivyo na upungufu wa uelewa wa mambo..

Kwa maana yako ni kwamba waTanzania watakuwa ni watu wa kufanyiwa tu kazi na watu wengine kwa sababu hawana uwezo wa kufanya chochote, na wizi ndiyo sifa yao milele.
Watu wa aina yako tutawakomesha tu, muda si mwingi unaokuja.
 
Hakuna lolote la maana unalo andika sasa hivi bali kurudia yale yale uliyo kwisha andika mara nyingi tu humu bila ya kujibu hoja husika.

Ufisadi upo Tanzania peke yake? Mbona huko kwingine nchi hizo zinapambana na ufisadi wa wananchi wake na kufanikisha nchi hizo kupata maendeleo. Na hata hao wawekezaji mnaotuimbia hapa kila siku, wanajuwa wanapokwenda kuwekeza katika nchi hizo ufisadi wanauweka pembeni. Hapa kwetu mnawatafuta nyinyi wenyewe kwa nia ya ufisadi; kwa nini wasifanye ufisadi huo.
Ufisadi mnafanya nyinyi viongozi halafu mnawasingizia waTanzania?
 
Namna tunavyoendesha bandari ni ushahidi wa uendeshaji wetu mbovu wa mashirika yote yaliyobinafsishwa wakati wa hayati Mkapa.

Tuna ufundi mwingi wa maongezi imarefu kama haya ya Kalamu, ukweli ni kwamba kikazi tupo dhaifu sana.

Samia kafanya la maana sana kuleta waendeshaji wawili hapo TPA ili pato la bandari liongezeke pia ufanisi uongezeke.

Mnaopenda kukariri maisha imekula kwenu. Pato la bandari linalokwenda hazina limeongezeka kwa muda wote hao waendeshaji wapya wakifanya kazi hapo TPA. Kwa miezi ya karibuni bandari yetu ndio bora kwa shughuli za upakuaji na upakiaji wa mizigo katika afrika ya mashariki. haya huwezi kuyaona kwa sababu akili yako imekaa kupokea habari mbaya tu.

Pole sana Kalamu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…