Leo kauli ya mama yakuwapa mashavu wachina na kusema china kwa sasa ni super power na kupendekeza hata Watanganyika inabidi tuanze kujifunza kichina.
Ukiangalia kwa jicho la tatu utaona ni kama mama alikua anaendeleza battle na mabeberu na sasa hanawaambia kwamba hata kama wao wakizingua bado kuna mchina atampiga tagi.
Swali hapa ni la kujiuliza kumetokea kitu gani kati ya serikali ya mama na mabeberu, wote tunajua mabeberu hawana time na demokrasia yenu kama interest zao hamjazigusa, si unaona kwa Kagame wanajua michezo yote anayoicheza lakini wamekausha sababu wanajua Kagame sio tishio kwao wala kwa masilai yao bali Kagame ni tishio kwa waafrica wenzake.
Swali nalojiuliza mbona mwanzo mama aliendanao sawa tu na alikua royal tu sasa nini kimetokea?
Au kuna mzigo mkubwa anataka kummegea mchina? Au ni ile inshu ya kuwapa mbuga na bandari wale waarabu?
Soma Pia: Rais Samia: Kuna haja ya kuwa na Mchepuo wa Masomo ya Lugha ya Kichina
Najua kuna watu wanazijua code vizuri kuna battle ya chinichini Kati ya serikali ya mama na mabeberu, hata chadema wanajua hii kitu ndio mahana wamekubali kuicheza hii battle wakiwa upande wa pili sababu na wao wameona opportunity ya kumtingisha mother.
Ushaidi mwingine ni ukiona nyuzi nyingi kwenye mitandao au hapa JF za machawa wakiyasema vibaya mabeberu ujue kuna kitu hakipo sawa.
Swali ni kwamba mziki wa mabeberu mnauweza kuucheza ikiwa tu kuna kipindi bei ya sukari inawasumbua? au ndio tuwaache mpaka mtakapoanza kubeba malundo ya hela kwa ajili ya kununua mkate kama Zimbabwe.