Code zinaanza kufunguka

Code zinaanza kufunguka

Hakuna mtu anayeudharau uwezo wa watanzania, ni sisi wenyewe tunajidharau kwa kuendekeza tabia za ufisadi na wizi wa kila aina.
Sasa kweli unataka jambo kama hili nalo nirudie rudie kueleza kwa nini inaonekana hivyo hapa kwetu na huko kwingine kukawa ni tofauti?
Nimeeleza mara ngapi, jambo hili hili; na wewe unarudia rudia tu vile vile!

Hii haiwezi kuwa mbinu ya kunyamazisha mjadala, bali inakufanya uonekane kuwa mpuuzi tu.
Kwa hiyo kazi yangu kwako nimeimaliza.
 
Sasa kweli unataka jambo kama hili nalo nirudie rudie kueleza kwa nini inaonekana hivyo hapa kwetu na huko kwingine kukawa ni tofauti?
Nimeeleza mara ngapi, jambo hili hili; na wewe unarudia rudia tu vile vile!

Hii haiwezi kuwa mbinu ya kunyamazisha mjadala, bali inakufanya uonekane kuwa mpuuzi tu.
Kwa hiyo kazi yangu kwako nimeimaliza.
Mpuuzi ni wewe unayechukulia ni kitu kipya kwa mwekezaji wa kigeni kuja kufanya kazi nchini tena kwa mkataba ulioandikwa na wataalam kwa miezi kadhaa ya majadiliano.
 
Ngoja niseme hivi kama kumalizana na wewe: Wewe siyo hawa mapunguani wengi tunao waona humu JF; ila wewe ni fisadi anaye endeshwa tu na maslahi.
Siyo kwamba hujui unacho elezwa, unajuwa na pengine kujutia huko moyoni mwako kwamba laiti isinge kuwa maslahi ya genge, ungekuwa ni tofauti. Ungepigania maslahi ya waTanzania.
Kuna baadhi ya mabandiko yako humu ambayo yalionyesha haya ninayo elezea hapa

Hayo ya ujenzi wa shule na mengineyo yana tofauti gani na ninayo kueleza na kukumbusha hapa kila mara. Ujenge shule huku elimu inayo tolewa humo ni ya kuwawezesha waTanzania kuwa watawana..., elimu hiyo inayo manufaa gani?
Wachina hawatoi elimu ya kuwaandaa watu wao kuwa watumishi/watwana; elimu yao inawaandaa kuwa wamiliki na waendeshaji wa shughuli zao za maendeleo ya nchi yao. Hivyo hivyo na Korea Kusini, Vietnam, na kwingine kote wanakojua ni nini maana ya nchi kuwa na wajibu wa maendeleo yake.
Samia na hili genge lenu, fikra hizi hazimo kabisa akilini mwenu.

Ni hivi: tusizungushane bure. Wewe unajua ninacho zungumzia humu; na mimi kwa hakika kabisa najua unaelewa vyema ninayo andika na hata bila shaka unajutia kuwa huko kwenye upande unakolazimika kuwepo, kwa sababu tu ya maslahi, na ushikamano yenu na Samia kwa mambo mengineyo binafsi; kitamaduni na kiimani.

Sina sababu tena ya kuzungushana na wewe humu.
Dunia halisi haibembelezi mtu au nchi fulani, tuwekeze kwenye elimu za aina mbalimbali au tukubali kupelekeshwa na wageni wanaokuja kuwekeza kwetu, uchaguzi ni wetu kusuka au kunyoa.
 
Leo kauli ya mama yakuwapa mashavu wachina na kusema china kwa sasa ni super power na kupendekeza hata Watanganyika inabidi tuanze kujifunza kichina.

Ukiangalia kwa jicho la tatu utaona ni kama mama alikua anaendeleza battle na mabeberu na sasa hanawaambia kwamba hata kama wao wakizingua bado kuna mchina atampiga tagi.

Swali hapa ni la kujiuliza kumetokea kitu gani kati ya serikali ya mama na mabeberu, wote tunajua mabeberu hawana time na demokrasia yenu kama interest zao hamjazigusa, si unaona kwa Kagame wanajua michezo yote anayoicheza lakini wamekausha sababu wanajua Kagame sio tishio kwao wala kwa masilai yao bali Kagame ni tishio kwa waafrica wenzake.

Swali nalojiuliza mbona mwanzo mama aliendanao sawa tu na alikua royal tu sasa nini kimetokea?

Au kuna mzigo mkubwa anataka kummegea mchina? Au ni ile inshu ya kuwapa mbuga na bandari wale waarabu?

Soma Pia: Rais Samia: Kuna haja ya kuwa na Mchepuo wa Masomo ya Lugha ya Kichina


Najua kuna watu wanazijua code vizuri kuna battle ya chinichini Kati ya serikali ya mama na mabeberu, hata chadema wanajua hii kitu ndio mahana wamekubali kuicheza hii battle wakiwa upande wa pili sababu na wao wameona opportunity ya kumtingisha mother.

Ushaidi mwingine ni ukiona nyuzi nyingi kwenye mitandao au hapa JF za machawa wakiyasema vibaya mabeberu ujue kuna kitu hakipo sawa.

Swali ni kwamba mziki wa mabeberu mnauweza kuucheza ikiwa tu kuna kipindi bei ya sukari inawasumbua? au ndio tuwaache mpaka mtakapoanza kubeba malundo ya hela kwa ajili ya kununua mkate kama Zimbabwe.
"... alikuwa loyal" royal ni kitu kingine kabisa
 
Dunia halisi haibembelezi mtu au nchi fulani, tuwekeze kwenye elimu za aina mbalimbali au tukubali kupelekeshwa na wageni wanaokuja kuwekeza kwetu, uchaguzi ni wetu kusuka au kunyoa.
Haya maneno nenda kamwambie Samia, kwani ndiye sasa anayetupeleka waziwazi kabisa kwenye hali hiyo. unayo ieleza hapa.

Katika mambo yooote anayo yafanya kama kiongozi, hili la kuua moyo wa waTanzania kuamini kuwa na uwezo wa kujenga nchi yao ndilo la kwanza kabisa katika kumwondolea sifa za kuwa kiongozi wa nchi.
 
Mpuuzi ni wewe unayechukulia ni kitu kipya kwa mwekezaji wa kigeni kuja kufanya kazi nchini tena kwa mkataba ulioandikwa na wataalam kwa miezi kadhaa ya majadiliano.
Unaelewa kwamba hicho siyo ninacho pinga, na nimekwisha rudia mara elfu na zaidi humu.
Hakuna mahali popote ninapo pinga uwekezaji unaofuata taratibu na kuzingatia maslahi ya nchi. Wewe unapindisha ionekane napinga uwekezaji, bila kujali maelezo ninayo toa kwa sababu una tetea maslahi maalum katika uwekezaji huo. Hili ndilo limeteka akili yako.
 
Back
Top Bottom