Code zinaanza kufunguka

Code zinaanza kufunguka

Huduma za viwango zinatolewa muda huu na hakuna ule uswahili na upigaji uliozoeleka enzi zile tukiendesha TPA sisi wenyewe.
"Uswahili na upigaji" mnao nyinyi, toka kiongozi mkuu wa nchi hadi huko serikalini. Kwamba hakuna "Huduma za viwango" huko; ndiyo maana ingefaa hao DPW na wengine wawekwe huko huko mlipo nyinyi kwa sababu matatizo yote yana anzia huko huko.
 
Leo kauli ya mama yakuwapa mashavu wachina na kusema china kwa sasa ni super power na kupendekeza hata Watanganyika inabidi tuanze kujifunza kichina.

Ukiangalia kwa jicho la tatu utaona ni kama mama alikua anaendeleza battle na mabeberu na sasa hanawaambia kwamba hata kama wao wakizingua bado kuna mchina atampiga tagi.

Swali hapa ni la kujiuliza kumetokea kitu gani kati ya serikali ya mama na mabeberu, wote tunajua mabeberu hawana time na demokrasia yenu kama interest zao hamjazigusa, si unaona kwa Kagame wanajua michezo yote anayoicheza lakini wamekausha sababu wanajua Kagame sio tishio kwao wala kwa masilai yao bali Kagame ni tishio kwa waafrica wenzake.

Swali nalojiuliza mbona mwanzo mama aliendanao sawa tu na alikua royal tu sasa nini kimetokea?

Au kuna mzigo mkubwa anataka kummegea mchina? Au ni ile inshu ya kuwapa mbuga na bandari wale waarabu?

Soma Pia: Rais Samia: Kuna haja ya kuwa na Mchepuo wa Masomo ya Lugha ya Kichina

Najua kuna watu wanazijua code vizuri kuna battle ya chinichini Kati ya serikali ya mama na mabeberu, hata chadema wanajua hii kitu ndio mahana wamekubali kuicheza hii battle wakiwa upande wa pili sababu na wao wameona opportunity ya kumtingisha mother.

Ushaidi mwingine ni ukiona nyuzi nyingi kwenye mitandao au hapa JF za machawa wakiyasema vibaya mabeberu ujue kuna kitu hakipo sawa.

Swali ni kwamba mziki wa mabeberu mnauweza kuucheza ikiwa tu kuna kipindi bei ya sukari inawasumbua? au ndio tuwaache mpaka mtakapoanza kubeba malundo ya hela kwa ajili ya kununua mkate kama Zimbabwe.
sometimes ninyi vijana ukiwa home, mamako anatafuta chakula, ukiona anataniana na wababa jua yupo kazini anatafuta msosi ule, tulia. Nijuavyo, maza vyovyote atakavyofanya hawezi kugombana na mabeberu, ila anawalemba wachina ili waje wajenge TAZARA kama walivyoahidi na ili wamalizie kipande cha SGR tulichokwama kama walivyoahidi. Hapa juzi wachina waliahidi kukimalizia and at the same time WORLD BANK jana wamekuja kusema wana mpango kufadhili pesa kumalizia SGR. jiulize kwanini world bank wanakuja kusema hivyo baada ya mchina kusema atatufadhili? hivi wewe mamako akiwa anagonganisha wanaume si unatakiwa kufumba mdomo, anajua anachokifanya ili uishi. hapa tulipo, nchi yetu masikini sana, tunashindwa hata kumalizia hizo miradi, rais anaweza kuwa na madhaifu yake, ila akiwa anafanya vya maana tumuunge mkono. hayo yote ya mama na wababa ni mafumbo tu ili watu waelewe.
 
Tija ya TPA imeongezeka sana na hilo ndilo muhimu kuliko hizi siasa za sisi watanzania tuendeshe wenyewe.
Wewe na Samia nina hakika huu ndio uamini wenu kwamba Tanzania haiwezi kufanya chochote; ni lazima tufanyiwe kila kitu. 'Mentality' hii ndiyo inaua moyo wa waTanzania, wajione wao ni duni; wageuzwe kuwa watwana tu wa hao watu wengine.Uongozi wa namna hii ni balaa kwa nchi yoyote.
 
Usiitazame bandari kwa mtazamo wa kizamani itazame kwa mtazamo wa kisasa ikifanya biashara pana zaidi.

Itazame kama sehemu ya 'a logistic supply chain', DPW haishii tu kusimamia magati hapo TPA anapakia mzigo kule Rwanda na DRC halafu anauleta mpaka bandarini Dar na kuupakia melini kwenda huko ughaibuni.

Tazama biashara pana zaidi kuliko hiyo loading na offloading iliyozoeleka kufanyika hapo bandarini, usiitazame hii biashara kwa akili ya kimazoea.
 
"Uswahili na upigaji" mnao nyinyi, toka kiongozi mkuu wa nchi hadi huko serikalini. Kwamba hakuna "Huduma za viwango" huko; ndiyo maana ingefaa hao DPW na wengine wawekwe huko huko mlipo nyinyi kwa sababu matatizo yote yana anzia huko huko.
Pole sana na kilio chako chenye kufanana na cha samaki, macho yanapotelea ndani ya maji.
 
Nimetoa mfano hapo Airport Dar kuna kampuni ya Swissport miaka 30 sasa, nani amewahi kuhoji kwanini ipewe tenda wakati hizo kazi tunaweza kuzifanya wenyewe, hakuna mwenye kuja na hoja hizo kwani kinachoangaliwa na tija inayoletwa na hiyo kampuni.
Kwa bahati mbaya sana 'model' hii mnaikopi tu bila kujua maana yake ni nini.

Hao wajomba zenu; hivyo viinchi vyenye ukwasi mkubwa unaotokana na mali asili zao wao hawakufanya kama mnavyo fanya nyinyi hapa.

Vi-nchi hivyo havina watu wengi; kwa hiyo wanalazimika kuingiza watu toka nje kuja kuwafanyia kazi zote; kwa vile wanao utajiri unaotokana na mali asili zao walizozimudu vizuri na kuhakikisha zinawanufaisha wao zaidi.
Wao wametumia akili kuhakikisha utajiri wao ndio msingi wa kuzinufaisha nchi hizo; hawakuachia tu huo unao uita ubia ufanyike kiholela.

Kwa kutojua kwenu, hao hao wajomba zenu sasa wanahaha kutafuta mbadala wa jinsi ya kuendeleza neema za nchi zao baada ya hizo gesi na mafuta kupungua matumizi yake. Ndiyo maana wanatafuta nchi zenye viongozi wasio kuwa na dira wala uchungu wowote wa nchi wanazo ziongoza, kama hii yetu sasa hivi.
Badala ya waTanzania kwenda kujisalimisha kufanya kazi huko huko kwao, sasa wao ndio wanakuja hapa kuwafanya waTanzania watwana hapa hapa nyumbani kwao. Watakapo shika njia zote muhimu za uchumi; kwa mikataba ya namna hii ya miaka 30 na zaidi itakuwa endelevu, bila kikomo.
 
Usiitazame bandari kwa mtazamo wa kizamani itazame kwa mtazamo wa kisasa ikifanya biashara pana zaidi.

Itazame kama sehemu ya 'a logistic supply chain', DPW haishii tu kusimamia magati hapo TPA anapakia mzigo kule Rwanda na DRC halafu anauleta mpaka bandarini Dar na kuupakia melini kwenda huko ughaibuni.

Tazama biashara pana zaidi kuliko hiyo loading na offloading iliyozoeleka kufanyika hapo bandarini, usiitazame hii biashara kwa akili ya kimazoea.
"Biashara pana zaidi" ndio kitu gani. Sisi hatuwezi kuwa na mawazo ya hiyo biashara pana zaidi unayo izungumzia wewe?
Hata haieleweki unazungumzia kitu gani hapa.
 
Leo kauli ya mama yakuwapa mashavu wachina na kusema china kwa sasa ni super power na kupendekeza hata Watanganyika inabidi tuanze kujifunza kichina.

Ukiangalia kwa jicho la tatu utaona ni kama mama alikua anaendeleza battle na mabeberu na sasa hanawaambia kwamba hata kama wao wakizingua bado kuna mchina atampiga tagi.

Swali hapa ni la kujiuliza kumetokea kitu gani kati ya serikali ya mama na mabeberu, wote tunajua mabeberu hawana time na demokrasia yenu kama interest zao hamjazigusa, si unaona kwa Kagame wanajua michezo yote anayoicheza lakini wamekausha sababu wanajua Kagame sio tishio kwao wala kwa masilai yao bali Kagame ni tishio kwa waafrica wenzake.

Swali nalojiuliza mbona mwanzo mama aliendanao sawa tu na alikua royal tu sasa nini kimetokea?

Au kuna mzigo mkubwa anataka kummegea mchina? Au ni ile inshu ya kuwapa mbuga na bandari wale waarabu?

Soma Pia: Rais Samia: Kuna haja ya kuwa na Mchepuo wa Masomo ya Lugha ya Kichina

Najua kuna watu wanazijua code vizuri kuna battle ya chinichini Kati ya serikali ya mama na mabeberu, hata chadema wanajua hii kitu ndio mahana wamekubali kuicheza hii battle wakiwa upande wa pili sababu na wao wameona opportunity ya kumtingisha mother.

Ushaidi mwingine ni ukiona nyuzi nyingi kwenye mitandao au hapa JF za machawa wakiyasema vibaya mabeberu ujue kuna kitu hakipo sawa.

Swali ni kwamba mziki wa mabeberu mnauweza kuucheza ikiwa tu kuna kipindi bei ya sukari inawasumbua? au ndio tuwaache mpaka mtakapoanza kubeba malundo ya hela kwa ajili ya kununua mkate kama Zimbabwe.
Pale tutakapogundua kuwa wachina wanataka ubia waingie kwenye serikali hii, tutakuwa tumeshachelewa. Jamaa wana akiloi sana hawa.
 
"Biashara pana zaidi" ndio kitu gani. Sisi hatuwezi kuwa na mawazo ya hiyo biashara pana zaidi unayo izungumzia wewe?
Hata haieleweki unazungumzia kitu gani hapa.
DPW keshanunua madini mengi huko DRC na Rwanda akisaini mikataba na marais wao, pia ni mzoefu wa uendeshaji wa bandari kisasa.

Unaposema 'sisi' ukumbuke rekodi yetu mbaya na iliyojaa ufisadi mwingi ya uendeshaji wa TPA. Samia na serikali kuipata DPW imesaidia sana kupunguza wizi hapo TPA.

Kuna mnyororo mpana wa ufisadi ulikuwepo hapo TPA kwa muda mrefu, huo umekuwa ukikwamisha mchango wa bandari kwenye uchumi mkuu wa TZ. Ni lazima Samia apigwe vita kwa kuua mtandao huo wa wizi na kelele kutoka kila upande ni ushahidi wa ushindi wa vita dhidi ya ufisadi unaofanyika hapo mahali.
 
"Uswahili na upigaji" mnao nyinyi, toka kiongozi mkuu wa nchi hadi huko serikalini. Kwamba hakuna "Huduma za viwango" huko; ndiyo maana ingefaa hao DPW na wengine wawekwe huko huko mlipo nyinyi kwa sababu matatizo yote yana anzia huko huko.
DPW yupo hapo bandarini na tija ikiongezeka ataongezewa mkataba.
 
DPW keshanunua madini mengi huko DRC na Rwanda akisaini mikataba na marais wao, pia ni mzoefu wa uendeshaji wa bandari kisasa.
Unajiandikia tu humu huku hujui chochote.
DPW ni hiyo Bandari kavu tu hapo Kigali, hana zaidi ya hilo, lakini sasa unakuja na ulaghai wa kununua madini!
Unaposema 'sisi' ukumbuke rekodi yetu mbaya na iliyojaa ufisadi mwingi ya uendeshaji wa TPA. Samia na serikali kuipata DPW imesaidia sana kupunguza wizi hapo TPA
Hakuna asiyejua hiyo rekodi mbaya hapo bandarini; lakini hiyo haiwezi kuwa sababu ya kunadisha bandari kwa dola 250 milioni katika miaka mitano na baada ya hapo huyo aliye wahonga aendelee kuvuna miaka mingine 25 na zaidi

Kuwepo rekodi mbaya hapo bandarini ndio ulikuwa uchochoro wenu wa kufanya hujuma; badala ya kurekebisha rekodi hiyo mbaya?
Kuna mnyororo mpana wa ufisadi ulikuwepo hapo TPA kwa muda mrefu, huo umekuwa ukikwamisha mchango wa bandari kwenye uchumi mkuu wa TZ. Ni lazima Samia apigwe vita kwa kuua mtandao huo wa wizi na kelele kutoka kila upande ni ushahidi wa ushindi wa vita dhidi ya ufisadi unaofanyika hapo mahali.
Hiki ndicho kichaka mlicho kitumia kufanya ufisadi wenu hapo bandarini. Akina Erick Hamisi mkawaondoa kwa kukataa kuwa sehemu ya hujuma yenu; kwani mnadhani watu hawajui kilichokuwa kikitokea?

Bandari imetengenezwa kwa hela ya mkopo toka Benki ya dunia, iwe bora; mkaona muipige bei haraka haraka kwa kuwapa wajomba kwa njia zisizokuwa na uwazi, bila ya kushindanishwa na yeyote. Mama yako kahamishia kabisa ofisi Dubai!
Ulisha ona kiongozi gani anafanya ujinga wa namna hiyo!
 
DPW yupo hapo bandarini na tija ikiongezeka ataongezewa mkataba.
Iwe miaka mingapi 60?
Sidhani kuwa Samia atadumu hapo alipo muda wote huo. Akibahatika atakuwa kabakisha huo mwaka mmoja tu; na huyo DPW ikigundulika kuwa chanzo cha uhujumu anafungashiwa vilago tu. Sababu ya kumwondoa hapo haiwezi kukosekana. Miaka mitano tu, anafanyiwa tathmini ambayo itamwonyesha hakukidhi matakwa.
Ndio maana nyinyi pamoja na hao wajomba zenu mnahaha sana wakati huu, kuhakikisha mnamnunulia serikali Samia.
 
Unajiandikia tu humu huku hujui chochote.
DPW ni hiyo Bandari kavu tu hapo Kigali, hana zaidi ya hilo, lakini sasa unakuja na ulaghai wa kununua madini!
Hakuna asiyejua hiyo rekodi mbaya hapo bandarini; lakini hiyo haiwezi kuwa sababu ya kunadisha bandari kwa dola 250 milioni katika miaka mitano na baada ya hapo huyo aliye wahonga aendelee kuvuna miaka mingine 25 na zaidi

Kuwepo rekodi mbaya hapo bandarini ndio ulikuwa uchochoro wenu wa kufanya hujuma; badala ya kurekebisha rekodi hiyo mbaya?
Hiki ndicho kichaka mlicho kitumia kufanya ufisadi wenu hapo bandarini. Akina Erick Hamisi mkawaondoa kwa kukataa kuwa sehemu ya hujuma yenu; kwani mnadhani watu hawajui kilichokuwa kikitokea?

Bandari imetengenezwa kwa hela ya mkopo toka Benki ya dunia, iwe bora; mkaona muipige bei haraka haraka kwa kuwapa wajomba kwa njia zisizokuwa na uwazi, bila ya kushindanishwa na yeyote. Mama yako kahamishia kabisa ofisi Dubai!
Ulisha ona kiongozi gani anafanya ujinga wa namna hiyo!
Hujui lolote masikini ya Mungu. DPW yupo hapo TPA kaingia mkataba mzito na serikali na kinachofanyika ni cha maana kwa upande wa serikali ya Tanzania.
 
Iwe miaka mingapi 60?
Sidhani kuwa Samia atadumu hapo alipo muda wote huo. Akibahatika atakuwa kabakisha huo mwaka mmoja tu; na huyo DPW ikigundulika kuwa chanzo cha uhujumu anafungashiwa vilago tu. Sababu ya kumwondoa hapo haiwezi kukosekana. Miaka mitano tu, anafanyiwa tathmini ambayo itamwonyesha hakukidhi matakwa.
Ndio maana nyinyi pamoja na hao wajomba zenu mnahaha sana wakati huu, kuhakikisha mnamnunulia serikali Samia.
Umeandika upuuzi mtupu. Tanzania ya viwanda aliyoitamka hayati JPM wakati wa kampeni mwaka 2015 ndio hii kwa vitendo ipo kazini muda huu.

Na sio DPW peke yao kuna ubia mwingi unaendelea nchi nzima kwenye sekta ya viwanda, nyinyi wanaharakati bakini na kulialia kwenu.
 
Hujui lolote masikini ya Mungu. DPW yupo hapo TPA kaingia mkataba mzito na serikali na kinachofanyika ni cha maana kwa upande wa serikali ya Tanzania.
Sasa umebakiza mipasho kama hii, huna zaidi ya hapo.
Ufaidi huo ufisadi mnao ufanya sasa hivi kabla ya kiama chenu.
 
Na sio DPW peke yao kuna ubia mwingi unaendelea nchi nzima kwenye sekta ya viwanda, nyinyi wanaharakati bakini na kulialia kwenu.
"Ubia" gani unao fanyika kwenye viwanda. Umechanganyikiwa?
Umeandika upuuzi mtupu. Tanzania ya viwanda aliyoitamka hayati JPM wakati wa kampeni mwaka 2015 ndio hii kwa vitendo ipo kazini muda huu.
Umekwisha dhihirisha mara kadhaa tokea mwanzo jinsi akili yako ilivyo finyu. Huwezi kuelewa maana ya kinacho andikwa; badala yake unaishia kurudia yale yale yasiyo husika na mada.

Nani au ni wapi pameandikwa kuwa kujengwa viwanda Tanzania ni makosa?
Wakati huelewi kinacho jadiliwa, wewe unang'ang'ana tuu na maswala yasiyo husika katika mjadala; kwa sababu akili yote umewekeza kwenye ulaji na kuwawezesha wajomba kuhujumu taifa hili.
 
"Ubia" gani unao fanyika kwenye viwanda. Umechanganyikiwa?
Umekwisha dhihirisha mara kadhaa tokea mwanzo jinsi akili yako ilivyo finyu. Huwezi kuelewa maana ya kinacho andikwa; badala yake unaishia kurudia yale yale yasiyo husika na mada.

Nani au ni wapi pameandikwa kuwa kujengwa viwanda Tanzania ni makosa?
Wakati huelewi kinacho jadiliwa, wewe unang'ang'ana tuu na maswala yasiyo husika katika mjadala; kwa sababu akili yote umewekeza kwenye ulaji na kuwawezesha wajomba kuhujumu taifa hili.
DPW wapo bandarini mpaka mkataba wao utakapomalizika.

Viwanda vingi vinaanzishwa muda huu wewe huwezi kuvijua kwa sababu unabii wa majanga ni tatizo lako kuu kuliko mengine yote.

Akili finyu unayo wewe mwenye mawazo yale yale ya kuona kazi inafanywa na watu wengi, kuna teknolojia za kisasa zinaondoa nguvu kazi nyingi kwenye ajira muda huu, mitambo ya kisasa inafukuza watu makazini.

Ujerumani wamegundua teknolojia za kujenga nyumba bila ya uwepo wa mafundi kwenye site, ni mitambo tu ipo kazini, maana yake wote wanaosomea vyuoni masuala ya uhandisi wa majengo wanakwenda kukosa kazi siku teknolojia hizo zikifika hapa Tanzania.

Akija mwekezaji kwenye sekta ya uhandisi na mitambo yake ya kujenga, kina Kalamu wenye akili za kizamani watampinga kwa nguvu zote.

Dunia inakwenda kasi sana jitahidi uende nayo kwa kasi hiyo hiyo ili usibakie kuchekesha watu humu kwenye jamvi.
 
Sasa umebakiza mipasho kama hii, huna zaidi ya hapo.
Ufaidi huo ufisadi mnao ufanya sasa hivi kabla ya kiama chenu.
Nenda hazina kaulize mchango wa Bandari kwenye magawio ya serikali mwaka huu ni kiasi gani kimeongezeka.

Hakuna haja ya kuandikia mate, wino upo.
 
Back
Top Bottom