Code zinaanza kufunguka

Labda ni kutaka kujaribu ubeberu wa China. India nayo inakuwa kwa kasi na kwa idadi ya watu imeshaipita China.
 
Anaweza kuwa rais mwenye mafanikio kuliko watano waliomtangulia, ukimchambua kwa haki lakini bila ya kwanza kumletea dharau za yeye kuwa mwanamke.

Samia anayo misingi ya marais watano waliomtangulia, anapita humo humo kwa akili iliyotulia.
Hayo ya 'mwanamke' unayaleta wewe, kwa sababu zako uzijuazo.
Mimi namwangalia Samia kwa yumbayumba yake toka ashike madaraka. Hiyo yumba yumba haionyeshi kiongozi anayejuwa anacho kifanya.
Mbaya zaidi, hana uwezo wa kueleza chochote anacho kiamini yeye.

Ishara muhimu ya kuonyesha hana misingi ni teuzi za kila wiki anazozifanya tokea aingie madarakani.

Ukisema Samia kau imarisha muungano kuliko au kuwashinda watangulizi wake, wewe utakuwa na sababu za kipekee sana kumhusu kiongozi huyu.

Ukisema Samia ni kiongozi anaye hangaishwa na hali duni za wananchi wa kawaida huko waliko, wewe utakuwa unazo sababu zako tofauti na za hao wanao hangaikia maisha yao huko vijijini.

Na nadhani baya zaidi linalomhusu Samia na uongozi wake ni kuwadharau raia anao waongoza. Kudhani kwamba hawa watu hawawezi kuleta maendeleo yao kwa juhudi zao. Yeye anacho fikiri wakati wote ni watu toka nje kuja kuleta maendeleo hapa.
Kiongozi anaua moyo wa uthubutu wa watu wake; nchi ya namna hiyo haiwezi hata miaka mia tano kuwa na maendeleo. Inazalisha watwana tu.

Samia ni mpita njia tu; ila kwa bahati mbaya sana, mpita njia ambaye atasababisha madhara makubwa kwa taifa hili kabla hajamaliza safari yake.
The sooner she is out of the way, the better for the nation.
 
Linapokuja swala la kibiashara hakuna beberu mbaya au mzuri likewise hakuna Mchina mzuri au mbaya. Shida inayotutafuna siku zote ni kuingia mikataba mibovu na corruption na hakuna wa kutusaidia kwa hayo isipokuwa sisi wenyewe. Mengine ni porojo tuu
 
Kila mwenye pumzi juu ya uso wa dunia ni mpita njia. Temporary home ni jina la wimbo wa Carrie Underwood, tupo hapa kwa muda mfupi tu.

Samia hana vishindo vya mbwembwe za wanasiasa kina JPM aliyetaka apigiwe makofi kwa kila alichoweza kufanya. Samia hana hiyo nguvu ya kutafuta sifa yeye mwenyewe. Pia hana makuu ana unyenyekevu hivyo hata akifanya kitu kikubwa sana ni vigumu kufahamu sisi watu wa kawaida.

Kivitendo anahangaishwa na hali duni za mwananchi wa kawaida, ndio maana miradi mingi iliyoanzishwa na JPM yeye anaimalizia muda huu huku akianzisha mingine mikubwa ya kilimo.

Angekuwa haguswi na shida za maskini hali ingekuwa ni tofauti na ukweli ulivyo huko mikoani.
 
Kila mwenye pumzi juu ya uso wa dunia ni mpita njia. Temporary home ni jina la wimbo wa Carrie Underwood, tupo hapa kwa muda mfupi tu.
Unajuwa wazi sikuwa na maana hiyo, sasa sijui hayo unayatoa wapi. Atakuwaje na "mbwembwe na vishindo" wakati uwezo wa kuongoza hana!
Unyenyekevu wa kuwaambia raia zake kutekwa, kuuawa ni "Drama"?

Kitu gani kikubwa kafanya na ikawa vigumu watu kufahamu? Wewe mwenyewe ulieleza humu JF kuwa baada ya sakata la bandari, kila kitu sasa itakuwa siri; na yeye kujitangaza kuwa 'Chura Kiziwi"; hizi ndiyo sifa za kiongozi? Mnaficha uchafu wenu ili watu wasijue kinachofanyika; huo ndio utawala bora?

Kiongozi aliye jaa hadaa na uongo kwa kila jambo, siyo wa kuaminika.
 
Tumuuliza Chura kiziwi amejipangaje? Nasikia ni YEYE kama To yeye hadi 2035
 
Akili ndogo tu...
Sera na diplomasia ya Tanzania kimataifa ilikuwa kutokufungamana na upande wowote!
Inashangaza kuona wakuu wa Dunia wapo UNGA... Yeye yupo Songea na Ruvuma anacheza bao na kusambaza ufuska!
 
Anaweza kuwa rais mwenye mafanikio kuliko watano waliomtangulia, ukimchambua kwa haki lakini bila ya kwanza kumletea dharau za yeye kuwa mwanamke.

Samia anayo misingi ya marais watano waliomtangulia, anapita humo humo kwa akili iliyotulia.
Mafanikio yasiyo na tija kwa wananchi ni upuuzi mtupu, Hali ya uchumi wa nchi ni ngumu sana kwa sasa, mafanikio pekee aliyonayo ni kukwapua mali zetu na kuwapa waarabu, kidogo na nyie vibaka mnapata pa kupitia.
 
Tusishangae Tanzania ikijiunga na BRICS! Wakati Marekani na West zinapoteza dominance ya dunia na dollar inavyozidi kupoteza thamani,si vibaya Mama akigeukia China.
Ingawa kwa Afrika huwezi kumkwepa Mamba ukamkimbilia Chui ukifikiri utakuwa salama!
Hata Mchina siyo mzuri.
 

Uwezo wa kuongoza wanaujua hao anaowaongoza ambao idadi yao ni milioni 64, haongozi nyumba kumi sio mwenyekiti wa serikali ya mtaa ni Rais wa Nchi nzima.

Kila kilichoachwa na Marehemu JPM anakimalizia muda huu, hakuna mradi aliyouacha hayati katika awamu ya tano usiokuja kumaliziwa ndani ya kipindi hiki cha awamu ya sita. Sio jukumu lake kutuwekea mkate na siagi mezani asubuhi kwa ajili ya kifungua kinywa anafanya masuala ya kisera zaidi na anayatekeleza ipasavyo.

Kuna mapinduzi ya kilimo yanaendelea muda huu katika mikoa inayozalisha chakula kwa wingi.

Kuna viwanda vinajengwa kwa kasi ya ajabu huko mikoani muda huu.

Sisi tunaozoea kulialia tukiwa hapa jijini Dar hatuwezi kuona makubwa yanayofanyika.
 
Kama hiyo Mchina anatutaka atulipie deni la taifa,otherwise aache utapeli wake.
 
Uwezo wa kuongoza wanaujua hao anaowaongoza ambao idadi yao ni milioni 64, haongozi nyumba kumi sio mwenyekiti wa serikali ya mtaa ni Rais wa Nchi nzima.
Na ni hao ndio wanaosema "hana uwezo wa kuaongoza"; lakini badala ya kuwaruhusu wamwonyeshe kuwa hana uwezo, badala yake kila njia zinatumika kulazimisha yeye kuendelea kuwepo kwenye uongozi bila ya ridhaa yao.
Wewe hili hulioni? Nimekwisha kueleza mara kadhaa sasa kuhusu hili: hicho "kipande cha mkate" kina manufaa gani kama uhai wenyewe upo mashakani?
Hiyo miradi unayo kimbilia kila mara, yeye hana lolote huko. Awepo, asiwepo, bado miradi inge endelea tu; tena pengine kwa ufanisi zaidi.
Kuna mapinduzi ya kilimo yanaendelea muda huu katika mikoa inayozalisha chakula kwa wingi.
Ni kama umezaliwa jana, kwamba hukumbuki haya maswala ya kilimo yanako tokea? Au unadhani watu wote hawajui/hawafuatilii yanayotokea hapa nchini miaka yote?

Kwa ufupi, Samia tokea aingie ni zero; na mbaya zaidi ni kuzidisha hali ya kunadisha nchi hovyo hovyo; kama alivyo fanya na Bandari; na sasa anaelekea kwenye Gesi na mali asili nyinginezo.
Kazi ya kuwageuza waTanzania kuwa watwana ndani ya nchi yao, hilo ndilo atapaswa kulijibu tokea sasa na kuendelea.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…