Code zinaanza kufunguka

Hamza ni AG wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, na anastahili kwa namna alivyowakimbiza kwenye suala zima la bandari.

Ulikuja na nia za kichawi za kutaka kuikatisha tamaa serikali iachane na uwekezaji lakini mkawa mnapungukiwa mengi kuhusu suala zima la huo uwekezaji.
 
Fursa zipo nyingi, viwanda kila kona vinajengwa nenda hapo mkoa wa Pwani utakutana na uzalishaji mali wa kila aina.

Viwanja vya ndege vinazidi kumaliziwa kwa kasi kubwa, vinaifungua Tanzania na kuifanya kuwa ni nchi inayoingilika na kutokeka kwa urahisi zaidi.

Pole sana kwa namna moyo wako unavyoumizwa na haya anayoyafanya Rais SSH.
 
Na bado mtajua hamjui! mabeberu kumbe ndio wamesanua mambo ya ugaidi wa serikali baada ya kuwatusi mabalozi wao! Mchina atabeba hadi figo zenu nyoko fisi maji mbadoo
 
EEEeeenHEEEE!
Hivi vyeo huko serikalini siku hizi navyo ni vya kujivunia? Watu wanapeana tu vyeo, hata kama uwezo hakuna!

Mambo ndani ya nchi hii yamefikia hapa yalipo fikia, hata ya kuwa na Rais, mkuu wa nchi asiye kuwa na sifa hata moja; kuna maajabu gani ya mtu kama huyo kubandika tu kila aina ya mtu mahali popote.

Hilo swala la bandari litakuwa ni aibu siku zote; hasa kutokana na uchafu ulio fanyika namna lilivyo shughulikiwa. Hakuna kitu hata kimoja cha kujivunia katika swala lile, lakini naona ndiyo imekuwa beji unayo tanguliza mbele kujivunia; huku ukijuwa huo ndio ulikuwa mwanzo wa anguko wa huyo unaye mnyonya damu kama kupe.

Kwani unadhani watu hawajui kwa nini Hamza amewekwa hapo alipo sasa; ili afanikishe mambo ya uchafu zaidi yanayo pangwa kufanyika katika mwendelezo wa uhujumu wa nchi hii.
Sasa mtu na akili zako timamu, na unajihesabu wewe ni mTanzania unaye penda nchi yako na raia wenzako, kuna kipi cha kujivunia katika uchafu kama huo!

Mnawaita waTanzania, "wezi, wavivu", n.k., halafu mnawaibia mali zao na kuwafanya watwana wenu na wajomba zenu?
 
Unaimba nyimbo ambazo hata 'tune' zake huzijui. Kwani hivyo viwanda kajenga Samia. Kabla ya yeye hapakujengwa viwanda nchi hii?
Kujengwa hivyo viwanda ndiyo iwe sababu ya kutusahaulisha hujuma zenu kwa waTanzania?

Hivyo viwanda ndiyo bei na thamani mliyo wawekea watanzania kuwapeleka kwenye utwana?
 
Pole sana mwanaharakati Kalamu.
 
Siasa za kijinga zinakuwa na wafuatiliaji wachache kwenye nchi ambayo watu wanajitambua na wanafukuzia fursa za kiuchumi.
 
"Fursa za kiuchumi" siyo kunadisha mali za watu unao waita wewe wajinga.
Hakuna anayenadisha mali za watanzania. Swissport wapo hapo uwanja wa ndege tangu 1995 nchi yetu imeuzwa kwa yoyote yule licha ya wao kufanya biashara hapa airport?.

Tupunguze huu wasiwasi na kujiona duni bila ya sababu zozote za msingi. Hakuna binadamu anayeweza kuishi kama kisiwa.
 
Huna sababu yoyote ya kuniita mwanaharakati, na wala sistahili kupewa pole yoyote. Ninayasema ninayo yaamini na kuyajuwa.
Hujui chochote unasumbuliwa na fikra za kijamaa za kudhani njia kuu za uchumi siku zote zinastahili zimilikiwe na umma, kuna mapinduzi ya kielimu yanaendelea duniani kila kukicha.
 
Hata huoni aibu kurudia yale yale ya miaka yote na kujibiwa.
Wewe, (huyo Hamza) kakaa hapo miaka mingapi?
Hao Swissport kazi hiyo ni peke yao wanaoweza kuifanya?

Ni kwamba wewe huelewi chochote ninacho kueleza humu. Utakuwa mTanzania wa akili gani kama huwezi kujuwa kuwa kazi kama hizo za Swissport zinaweza kufanywa na waTanzania? Hao wamekaa hapo miaka mingapi hadi leo; halafu unakuja hapa na kujivunia uongozi wa kijnga namna hii?

Hali ni hiyo hiyo, hata huko Bandarini. Kakaa hapo TICTS zaidi ya miaka 25; sasa mkaleta huyu mjomba wenu miaka zaidi ya 30; hivi hata huoni aibu kuzungumzia haya mambo kama huna akili kichwani?
 
Hujui chochote unasumbuliwa na fikra za kijamaa za kudhani njia kuu za uchumi siku zote zinastahili zimilikiwe na umma, kuna mapinduzi ya kielimu yanaendelea duniani kila kukicha.
Kama wewe unaona kuna ubaya wowote na ujamaa, mimi sioni hivyo. Na kama wewe unaona ubepari wa kuazima ndiyo sifa, mimi sioni hivyo.

Nilisha kueleza, hayo maswala ya ujamaa/ubepari, hizo ni fikra za kizamani sana. Hakuna nchi yoyote duniani ambayo imeshikilia mfumo mmoja wa ubepari au ujamaa.
 
Hujui chochote unasumbuliwa na fikra za kijamaa za kudhani njia kuu za uchumi siku zote zinastahili zimilikiwe na umma, kuna mapinduzi ya kielimu yanaendelea duniani kila kukicha.
'Actually' huu ni ujinga mkubwa sana. Ni wapi nilipo eleza kuhusu uchumi kumilikiwa na umma. Kwani hatuwezi kuwa na sekta binafsi hapa ya watu ambao sasa hivi mnafanya kila njia kuwageuza kuwa watwana?
 
Sijawahi kumpenda huyu mama yenu, kwa kweli sijaona alichofanya zaidi ya kututia kwenye hasara kubwa kwa kweli, naombeni msikilize hii clip mtaelewa.
 

Attachments

  • VID-20241001-WA0011.mp4
    14.7 MB
Hakuna binadamu anayeishi kama kisiwa. Muingereza aliyetutawala kamuajiri DP World kwenye sekta ya bandari.

Marekani kuna wahindi wengi tu kwenye sekta ya mawasiliano wenyewe wanaita outsourcing, ndio dunia ilivyo. Ile ya kujifungia mwenyewe ndani imeshapitwa na wakati.

Hamza yupo serikalini kuanzia mwaka 2014, mamlaka ya anga alianzia kama mwanasheria anayetetea haki za wasafiri akateuliwa kuwa mkurugenzi mkuu na sasa mwanasheria mkuu wa serikali.
 
"Fursa za kiuchumi" siyo kunadisha mali za watu unao waita wewe wajinga.
Hakuna anayenadisha, lengo la kumpatia DPW bandari aendeshe ni kuongeza tija kwenye hazina ya Taifa na hivi sasa imeongezeka sana.

SSH anafanyia kazi kwa vitendo yale maneno ya kebehi aliyoyasema Kagame kipindi kile cha JK, kwamba anao uwezo wa kuiendesha Tanzania kupitia bandari ya Dar peke yake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…