Code zinaanza kufunguka

Sidhani kuwa unafanya maksudi kupotosha; ni wazi huelewi ninacho sisitiza hapa. Upofu wa kujipatia fursa binafsi ndilo tatizo.
Ni wapi ulipo soma nimeandika kuwa Tanzania ijitenge kuwa kisiwa; haya wewe unayatoa wapi?

Kuna nchi gani imejitenga kuwa kisiwa katika dunia ya leo? Hata Korea Kaslkazini inawabidi washirikiane na China na sasa Urusi; lakini wewe kwa sababu zako unazo juwa mwenyewe, unanisakazia kuwa nagombea Tanzania ijitoe duniani, iwe kisiwa?

Hizo nchi zote zinazo sisitiza kufaidika wao katika ushirikiano na mataifa mengine wewe huzioni? Kwa nini nyinyi, wewe, Samia na genge lenu mnalazimisha Tanzania liwe shimo la takataka za dunia, mradi nyinyi mnufaike!

China wamefungua nchi; lakini hawakuwauza wachina wawe manamba; wewe hili hulijui? Hali ni hiyo hiyo na nchi zote; hata hiyo Marekani unayo kimbilia kuitolea mfano. Umemwona MMarekani akigeuzwa kuwa mtwana humo nchini mwao?

Mnatengeneza mazingira ya kupafanya Tanzania kuwa sehemu ya uchafu, wanakokwenda wajomba zenu, kama wanavyo fanya kwenye baadhi ya nchi kama Indonesia.
 
Hamza yupo serikalini kuanzia mwaka 2014, mamlaka ya anga alianzia kama mwanasheria anayetetea haki za wasafiri akateuliwa kuwa mkurugenzi mkuu na sasa mwanasheria mkuu wa serikali.
'Of course', watu wenye tabia za kinafiki mambo yao huwaendea vizuri wakati uongozi unapokuwa ni mbovu; wa kupenda kusifiwa hovyo hovyo na kujipendekeza; badala ya uwezo stahiki. Wewe hapo unaona ajabu kwa huyo Hamza kuwa kama alivyo?
Mtu huyo huyo, anamsifia Magufuli, kwamba ni mzalendo. Magufuli akiondoka na kuingia Samia na kufanya mambo kinyume kabisa na Magufuli katika baadhi ya mambo ya msingi, Samia anakuwa ndiye kiongozi bora. Utategemea nini kwa mtu kama huyo!
Vyeo vya kupewa, kwa vile umeandika jambo kumjibu Fatma Karume, hilo nalo ni jambo la kusifia kweli?
 
SSH anafanyia kazi kwa vitendo yale maneno ya kebehi aliyoyasema Kagame kipindi kile cha JK, kwamba anao uwezo wa kuiendesha Tanzania kupitia bandari ya Dar peke yake.
Angalia sasa unavyo jiaibisha. Sasa hapo unadhani Kagame atamsifia Samia kwa kuweza kuendesha bandari?
Sana sana huyo huyo Kagame atakuwa anawaona akili haziwatoshi. Mtashindwa vipi kuendesha bandari miaka nenda miaka rudi? Ni jambo gani sasa mtakalo weza kuliendesha wenyewe?

Narudia yale yale kukueleza, lakini akili yako imeganda kweli kweli kwa sababu unafaidika na uchafu unao nyonya toka kwa Samia.
 
Magufuli alikuwa na mawazo ya aina hii ya kwako akaishia kutukanwa na kusimangwa kuna watu walimuita mshamba kwa kukata kuwa na ukaribu na mataifa makubwa ya dunia hii.

Samia kaamua kuja kivingine bado msio na shukrani mnakuja na matusi ya kipumbavu kabisa.

Wewe huoni umuhimu wa uwekezaji, mamilioni ya vijana ambao muda huu wanapata ajira kwenye viwanda vinavyofunguliwa wakikusoma haya mawazo yako watakucheka na kuachana na fikra zako mazima.
 
Hakuna rais wa serikali ya CCM mwenye kuweza kuongozwa na hisia zake binafsi kwa asilimia 100, yapo, mengi ataendeleza yale ya mtangulizi wake.

Ilani ni ile ile na waandishi wake ni wale wale. Samia ndio Rais wetu wewe endelea tu kuishi na machungu moyoni mwako, umechagua kuishi hivyo na hakuna wa kukuingilia akilini mwako.

Hamza ni kichwa sana, huwezi kukubaliwa na marais zaidi ya wawili halafu kichwani mwako ukawa ni mtu tu wa kawaida.

Mkapa alisikitika siku alipokutana na Hamza wakari keshaondoka madarakani, akasema angetamani katika urais wake angefanya kazi na kijana kama Hamza.

Kikwete aliidhinisha apewe cheo kikubwa serikalini lakini Wasaidizi wa Mwakyembe pale wizara ya mawasiliano wakaficha barua aliyoagiza apewe cheo kikubwa, ndani ya makabati wakidhani wanamkomoa kumbe wanampiga chura teke na kumuongezea mwendo.

Hayati JPM alipomsikia katika mkutano mmoja wa serikali akaagiza apewe cheo cha ukurugenzi wa TCAA.
 
Mpuuzi wewe usiyetaka kuelewa kwamba biashara nzima ya DPW na serikali chanzo ni huko DRC ambapo Rais Tshisekedi alisaini na boss wa DPW mwaka 2017.

Biashara nzima ya DPW na Tanzania ni inaanzia kule DRC inakuja Rwanda halafu inakuja Tanzania. Kagame anafahamu kuwa bandari ya Dar inapoendeshwa kisasa hata wao wanafaidika kiuchumi.
 
Mchina hajawahi kuwa na huruma kwa ngozi nyeusi. Akikupa mkopo ujue utaulipa kwa riba kubwa na ukishindwa anajimilikisha chochote chenye thamani ili ajilipe.
 
Magufuli alikuwa na mawazo ya aina hii ya kwako akaishia kutukanwa na kusimangwa kuna watu walimuita mshamba kwa kukata kuwa na ukaribu na mataifa makubwa ya dunia hii.
Na huyo Samia akiwa mmoja wao wa hao waliokuwa wakimwita "mshamba"! Sasa hapo sijui kama unayaona maajabu hayo, au siyo? Na wewe ulimwita nani vile? Angalia sasa mnayo fanya; mafisadi wakubwa nyinyi hata chembe ya aibu hamna!
Wewe huoni umuhimu wa uwekezaji, mamilioni ya vijana ambao muda huu wanapata ajira kwenye viwanda vinavyofunguliwa wakikusoma haya mawazo yako watakucheka na kuachana na fikra zako mazima.
Hata ulazimishe mara ngapi kugeuza ninayo eleza kwa kujifanya huelewi haitakusaidia kitu. Uwekezaji wa Samia ni uvamizi wa mali za waTanzania; ni kuwafanya waTanzania kuwa watwana ndani ya nchi yao, ni uwekezaji wa kuifanya Tanzania kuwa tegemezi milele. Huo siyo uwekezaji ni zaidi ya uporaji. Ni kuua moyo wa taifa hili.
Ndiyo sababu Samia anastahili kuwekwa mbele za sheria kujibu mashataka ya uhaini juu ya taifa alilopewa jukumu la kuliongoza.
 
Haya uliyo andika hapa yalikuwa sahihi kabla ya Samia hajaenda kujificha kule kwa wajomba zake kwa wiki kadhaa akipanga njia za kulihujumu taifa hili.
Wiki ya kwanza tu baada ya kushika madaraka, akadakwa na 'genge' lililomharibu akili kabisa. Hii ni kwa sababu ya upungufu wake wa kuwa na msimamo na mawazo anayo yasimamia mwenyewe. Ile 'Royal Tour' unaikumbuka?
Hakuna Rais yeyote wa CCM aliye anza kwa ujinga wa aina ile. Ile haikuwa utekelezaji wa Ilani kama unavyo eleza wewe hapa Bila shaka utaeleza pia kwamba ni uendelezaji wa Ilani ya CCM kuua muungano kama anavyo fanya Samia tokea aingie serikalini! Mbali ya Kikwete, sijapata kumwona rais mwingine aliye fanya juhudi hiyo zaidi ya Samia..
Hamza ni kichwa sana, huwezi kukubaliwa na marais zaidi ya wawili halafu kichwani mwako ukawa ni mtu tu wa kawaida.
Sasa hivi ninamfahamu Hamza vizuri zaidi kadri unavyo zidi kumwelezea humu. Huyo ni uthibitisho sahihi wa tabia na desturi mnazo zionyesha humu nyote; akina Samia, Tlaatlaah; EeenHeee, na wewe mwenyewe; na wengi wengine nisio hitaji kuwataja.
Ni mila hatari za mtu kucheka/tabasamu huku akiwa na mzigo mzito moyoni mwake. Ukijisahau kidogo tu, anakumaliza.
Hivyo ndivyo mlivyo.
 
EEEEEeeeenHEEEEEee!
Imenibidi nicheke nilipokuwa nasoma wasifu huu juu ya Hamza!
Umesahau kuongezea habari za akina January Makamba hapo, ili kukamilisha sura sahihi inayo mhusu huyu Hamza.

Na sasa ndiye Mwanasheria Mkuu wa Serikali! EEEeeeenHEEEEE!
 
Wacha upumbavu wako. Zungumzia Tanzania hapa na jinsi mnavyo inajisi nchi hii. Hayo ya huko Kongo waachie wakongo wenyewe.
Kwa hiyo unataka kuhamishia yanayo wasumbua wakongo yaje pia hapa Tanzania?

Na hata huoni aibu kusema uongo: Tshisekedi atasaini mkataba 2017 vipi na hao DPW?
 
Ameshajua kua CIA wamesha m write off kwenye kinyang'anyiro kijacho!!

jk hakulopoka Kwa bahati mbaya"labda mambo yaharibike sana"!!
 
Mkuu Kalamu hii ni dunia isiyo na huruma na isiyosubiri mimi na wewe tuamke tupate akili ili tuweze kwenda sambamba na ushindani uliopo.

Uwekezaji unafanyika ulimwengu mzima, na serikali zinazoukubali ufanyike haziongozwi na wajinga, huongozwa na wasomi wenye kujua wanafanya nini.

JPM alikuwa na akili kama za kwako, watu humu wakamuita mshamba leo kaja Samia mwenye akili tofauti watu bado wanakuja na ukosoaji mwingi tu, dawa yenye kufaa ni Samia kuendelea kufanya kile anachokiamini kwa faida ya Tanzania inayofunguka kiuchumi.
 
Samia alikuta Tanzania ina ndege 11 za abiria katika kipindi cha miaka mitatu kanunua ndege tano, moja ya mizigo na nne za abiria.

Kazi ya hizo ndege haina tofauti na royal tour, kuutanganza utalii na kurahisisha ufikaji na uondokaji wa hao watalii.

Hamza ni mtaalam wa sheria mbobezi kwenye zile za kimataifa, mikataba mingi iliyoandikwa na kusainiwa katika awamu ya tano na ya sita ni kazi ya Hamza pamoja na wanasheria wengine.

Kusema Samia alidakwa ndani ya wiki ya kwanza, ni kuendekeza majungu na stori za vijiweni. Hakuna aliyemdaka.
 
Mpumbavu ni wewe usiyeweza kukubali ukweli kwamba Biashara ya bandari ni muendelezo wa Logistic supply chain kwa maana ya biashara inayoanzia DRC ikaishia hapa Tanzania.

Mpumbavu ni wewe ambaye pengine hufahamu kuwa Tshisekedi baada tu ya kuapa kuwa rais wa DRC alifanya ziara rasmi hapa nchini na akatembelea bandari ya Dar mahali ambapo DPW alikuja kufanya uwekezaji wake.

Hii ni biashara kubwa yenye kuhusisha mataifa matatu, nenda kawaambie hao waliokutuma kwamba mipango yao kupitia wewe wakala wao ilishashindwa kitambo tu.
 
Mkuu Kalamu hii ni dunia isiyo na huruma na isiyosubiri mimi na wewe tuamke tupate akili ili tuweze kwenda sambamba na ushindani uliopo.
Mstari huu upo sahihi kabisa, ndiyo maana nakataa ujinga anao fanya Samia. Hao anaowagawia mali zetu hawaji hapa kutufanyia fadhira; wanakuja hapa kuneemeka juu ya migongo ya waTanzania. Hawapo hapa kuwasaidia waTanzania kwa chochote. Ndiyo maana namwona Samia kuwa kiongozi wa hovyo, kwa sababu hajui anacho fanya.

Lengo kuu la uwekezaji toka nje liwe ni kutuwezesha sisi waTanzania kuendesha shughuli hizo katika muda mfupi iwezekanavyo, na siyo kutufanya sisi tuwe watwana tu wa kuwategemea hao wawekezaji. Bandari miaka 50 tunawapa wageni, bila ya kuweka mikakati ya kujua kuifanya kazi hiyo sisi wenyewe? Mfano wako wa Swissport... na kwingine, kila mahala unapoweza kutazama.
Huwezi kupata maendeleo kwa njia hiyo. Miaka yote utakuwa ni tegemezi tu wa watu wengine hata katika maswala rahisi kabisa.
 
Upumbavu ulio nao ni kwamba unashikilia jmambo tofauti kabisa na unayo ambiwa.
Nani kakwambia hapendi ufanisi wa bandari? Ni wapi ulipo soma nikisema bandari ya Dar es Salaam haitakiwi kuwa na ufanisi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…