Sidhani kuwa unafanya maksudi kupotosha; ni wazi huelewi ninacho sisitiza hapa. Upofu wa kujipatia fursa binafsi ndilo tatizo.Hakuna binadamu anayeishi kama kisiwa. Muingereza aliyetutawala kamuajiri DP World kwenye sekta ya bandari.
Marekani kuna wahindi wengi tu kwenye sekta ya mawasiliano wenyewe wanaita outsourcing, ndio dunia ilivyo. Ile ya kujifungia mwenyewe ndani imeshapitwa na wakati.
Hamza yupo serikalini kuanzia mwaka 2014, mamlaka ya anga alianzia kama mwanasheria anayetetea haki za wasafiri akateuliwa kuwa mkurugenzi mkuu na sasa mwanasheria mkuu wa serikali.
Ni wapi ulipo soma nimeandika kuwa Tanzania ijitenge kuwa kisiwa; haya wewe unayatoa wapi?
Kuna nchi gani imejitenga kuwa kisiwa katika dunia ya leo? Hata Korea Kaslkazini inawabidi washirikiane na China na sasa Urusi; lakini wewe kwa sababu zako unazo juwa mwenyewe, unanisakazia kuwa nagombea Tanzania ijitoe duniani, iwe kisiwa?
Hizo nchi zote zinazo sisitiza kufaidika wao katika ushirikiano na mataifa mengine wewe huzioni? Kwa nini nyinyi, wewe, Samia na genge lenu mnalazimisha Tanzania liwe shimo la takataka za dunia, mradi nyinyi mnufaike!
China wamefungua nchi; lakini hawakuwauza wachina wawe manamba; wewe hili hulijui? Hali ni hiyo hiyo na nchi zote; hata hiyo Marekani unayo kimbilia kuitolea mfano. Umemwona MMarekani akigeuzwa kuwa mtwana humo nchini mwao?
Mnatengeneza mazingira ya kupafanya Tanzania kuwa sehemu ya uchafu, wanakokwenda wajomba zenu, kama wanavyo fanya kwenye baadhi ya nchi kama Indonesia.