COINCIDENCE: Moja ya ushahidi wa uwepo wa Mungu


Haya maswali yako ya kiboya yanakusaidia nini?
 

Unataka kueleweka kweli kwa hoja kuwa, Sheria haijitoshelezi kwa kuwa inahitaji uwepo wake? Embu tuambie, unawezaje kututofautishia kati ya Sheria na Uwepo wa Sheri, ili tujue unachongea ni nini hasa. Tafadhali.

Sheria haina inachohitaji, ila tu yenyewe inatosha. Huku ndio kujitosheleza. Je, KUJITOSHELEZA KWA SHERIA NI MAPUNGUFU?

Maswali yako haya;
a) Kwanini Mungu awe Sheria, hapa ni sawa na kuhoji kwanini Mungu ni Mungu!
b) Je bila sheria angeweza kuwepo? Hapo ni sawa na kuuliza Je, bila Mungu mwenyewe, Mungu angeweza kuwepo! Ili nikujibu, jibu hili kwanza, tuoneshe MPAKA KATI YA MUNGU NA UWEPO WA MUNGU!
c) Je, sheria inajihitaji yenyewe ili iwepo? Onesha kwanza ni wapi mpaka wa Sheria na Uwepo wa Sheria? Unawezeje kutenganisha Uwepo wa Mungu na Mungu?
d) Je, bila sheria hiyo sheria isingekuwepo? Unauliza bila Mungu je Mungu asingekuwepo? Tutenganishie kwanza Uwepo wa Mungu na Mungu? Ni wapi tunaweza kuona Uwepo wa Mungu bila Mungu mwenyewe?
Hujui unachohoji, unarudiarudia swali moja mara kenda.
e) Na hiyo sheria ilitoka wapi? Sheria ni Asili.
Mungu wetu yu tayari kutushindia vitani. Anaita sasa!
 

Yote hayo kaka kayataka mwanadamu, Mungu alipoiumba dunia, aliumba kila kitu ikiwemo kifo na akaviona ni vyema, kifo kilikuwepo EDEN na akakiona ni chema kwakuwa alitegemea mwanadamu atatii sheria zake za kutogisa wala kula matunda ya mti huo, sasa walipokaidi amri hio mabaya yote yakawakuta, chuki, njaa taabu misuko suko yote hayo yalitokana na ukaid wa mwanadamu, kwahio kabla hujahojo upendo wa Mungu ni bora u hoji ukaidi wa Mwanadamu. Mungu ni pendo na anafanya kila kitu kwa malengo yake hakuna wa ku question the work of God never on earth or heaven above.
 

Mungu katokeaje? Kwa nini mungu iwe lazima awepo?

Hujajibu hili swali, ukisema ni asili hujajibu kwa sababu hujaeleza kwa nini ni lazima awepo, na awepo huyu tu.
 

Kwa nini mungu aumbe kifo wakati alikuwa na uwezo wa kuumba ulimwengu ambao kifo hakiwezekani?

Baba gani anaweza kumpa mwanawe mchanga vikimbe viwili, kimoja kikiwa na maziwa na kingine chenye sumu iki tu mtoto mchanga achague?

Mtoto akichagua sumu na kufa, utasema baba ana mapenzi na mtoto?
 

Kwanini unadhani suala la kumuokoa huyo jamaa ni suala la Mungu?

Una uhakika kabisa kwamba huyo jamaa alimuomba Mungu sahihi kama inavyohitajika hadi umuwekee doubt Mungu?

Una uhakika alimuomba Mungu wa kweli?

Maswali ni mengi sana lakini kufikia hitimisho kwa namna hii ni hatari sana!
 

Adam hajawah kuwa mtoto mchanga aliumbwa na akil zote ndo maana akapewa bustan aitawale, na vitabu vinasema walikuwa na makutano na Mungu jion jua lilipopungu (mwanzo 3:8) sasa alifanya kusudi kabisa kujaribu tunda la mema na mabaya. Yale yalikuwa madharau na jeuri kwa hio hakukuwa na jinsi lazima Mungu angetimiza neno lake ya kuwa ukila utakufa hakika ( mwanzo 2:17) ilikuwa lazima adamu afe na kupoteza ukuu wake dunian kutokana na jeur yake. Hapo Mungu alionesha msimamo wake tuu juu ya neno lake. Mungu ni mwema na pia ni pendo.
 

Aliumbwa na akili kama za mungu?

Kama hakuumbwa na akiki kama za mungu, kwa nini mungu kambania?

Ina maana mungu ana choyo?
 
Aliumbwa na akili kama za mungu?

Kama hakuumbwa na akiki kama za mungu, kwa nini mungu kambania?

Ina maana mungu ana choyo?

Mungu na binadamu kamwe hawezi kufanana uwezo wa robot na mwanadamu je unaweza ukawa sawa?! Kumbuka Mungu alituumba tufanye usharika na yy na kumuabudu tuu. Ukitaka kufanana na Mungu yatakukuta ya Lucifa
 

Jibu ni jepesi sana juu ya swali lako maarufu la ajali n.k.
M/mungu tunaemuamini sisi alishatwambia hapa duniani ni mapito tu, na ni mtihani kwa watu wote wenye akili na waliomini uwepo wake watafaulu mtihani huu na mwisho wataenda kuishi maisha ya mile na mile(huko hakuna ajali wala janga lolote ni raha tu, kama unavyotaka wewe) ..
Maana yake nikua hayo maisha ya bila ajali na majanga yeyote havipatikani hapa duniani ni hukooo kwenye maisha ya kesho baada ya kifo..
Hapa ni mshike mshike tu, sasa kwa wenye akili ndo tushafahamu kua hapa si pa milele kwahyo lolote lawezekana juu ya ajali na majanga mengine, ili iwe fundisho kwa wanao baki.
hukumu ya hao waliopatwa na majanga anaijua yeye mwenye muumba, sio mimi na wewe kwahyo usikimbilie kusema pengine wao kupatwa na majanga hao watu ndio hawajapendelewa na mungu, no mind you maisha yakweli hayapo hapa duniani..

Kiranga elewa kua kupenda dunia ni maradhi yanayozidi hata ugonjwa wa ukimwi.. (fikiri nje ya box, utaelewa sana)
 

Unajibu katika context ya mabaya kuwa mtihani.

Kwa nini mungu mwenye uwezo wote, ujuzi wote, upendo wote na uwepo pote ahitaji kuwapa mtihani viumbe wake?

Najua kwa nini walimu na Baraza la Mitihani wanatoa mitihani. Kwa sababu wanataka kujua wanafunzi wameelewa nini. Walimu na Baraza la Mitihani hawajui kila kitu, na wanahitaji mitihani iki kujua wanafunzi wanahua nini.

Huyu mungu ambaye yeye ndiye mtia wa neema zote, zikiwemo neema za akili ya kumjua na ya kutomjua, kwa nini ahitaji kuwapa mitihani viumbe wake mwenyewe?

Hususan kama mitihani yenyewe inahusisha mabaya wakati ambapo angeweza kufanya vyovyote anavyotaka na kufikia lengo lile lile bila kutumia mabaya?

Mungu alishindwa kuumba ulimwengu ambao hauna mabaya na ambao ungempa vyote alivyotaka kuvipata kama anavyovipata sasa?
 

Kiongozi, nasikia yule bibie "k" kakuweka kwenye Ignore List
 

I thought nilikwambia ufikiri nje ya kiboks!

Any way isiwe tabu, twenda na hii... Mfano kuna watu toka wazaliwe hawajawah kukumbwa na majanga yeyote kwa maana ya ajali, tsunami n.k..
Je unafikiri hao watakua wanalindwa na nani?
Ni kiunganisha dots naanza kuelewa kua wewe utautambua uwepo wa mungu baada ya kuona watu/binaadamu wanaishi bila kukumbana na hayo majanga, sasa nipe jibu kua hao ambao wameishi bila ya hayo majanga ni viumbe/binadamu wanaoepushwa na nani if not God himself!?
 

Sijauliza swali kuhusu wasiokumbwa na majanga.

Nimeukiza kuhusu majanga, imekuwaje yanawezekana kurokea katika ulomwengu ulioumbwa na mungu mwenye uwezo wote, ujuzi wote, upendo wote na uwepo pote?

Ina maana mungu alipokuwa anaumba ulimwengu aliweza kuuumba ulimwengu ambao majanga hayawezekani lakini hakutaka tu?

Au alitaka kuumba ulimwengu ambao hauna majanga ila hakuweza?

Hujajibu swali hili.

Ulichofanya imelikwepa na kuongelea kitu tofauti.

Ulichoulizwa hujajibu, ulichojibu hujaulizwa.
 

Wewe ulikutana na mungu wapi akakwambia kua kwake ili ionekane dunia ni ya haki lazima isiwe na ajali, na mangonjwa n.k?
Pingine context ya HAKI kwa mungu mwenyewe ndo hivi alivyoiumba!
Sisi ni viumbe tulio ndani ya uumbaji wake..

Pia kuna malaika ambao wameumbiwa maisha unayoyasema wewe, huko kwao hamna ajali wala harufu ya tsunami, sasa kama ameweza kuwaumba malaika hivyo vipi ashindwe kwetu?.. Hapana ajashindwa ispokua kuna somo ndani yake..
#toka nje ya kiboksi plz
 

Wewe ulikutana na mungu wapi akakwambia kua kwake ili ionekane dunia ni ya haki lazima isiwe na ajali, na mangonjwa n.k?
Pingine context ya HAKI kwa mungu mwenyewe ndo hivi alivyoiumba!
Sisi ni viumbe tulio ndani ya uumbaji wake..

Pia kuna malaika ambao wameumbiwa maisha unayoyasema wewe, huko kwao hamna ajali wala harufu ya tsunami, sasa kama ameweza kuwaumba malaika hivyo vipi ashindwe kwetu?.. Hapana ajashindwa ispokua kuna somo ndani yake..
#toka nje ya kiboksi plz
 

Sijaonana na mungu ila characteristic yake anayodaiwa kuwa nayo ya upendo wote inamtaka azuie kuumba ulimwengu ambao una mabaya, na ulimwengu huu tunaona una mabaya mengi.

Hujatoa jibu kwa nini iwe hivyo.

Na kama kuna malaika wameumbwa na kipewa maisha yasiyo mabaya, kwa nino binadamu hajaumbwa na kupewa maisha hayo?

Hata baba anayempa zawadi mtoto mmoja na kumnyima mwingine ataonekana hana haki, sembuse mungu?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…