Kujua ni ndoto ambayo mpaka sasa inafukuziwa.
Strictly speaking, hakuna yeyote anayejua chochote.
Ila kuna misingi ya kuviondoa vile ambavyo si tu havijulikani, bali pia haviyumkiniki. Kama vile kuwapo kwa mungu.
Mkuu maelezo yako hayajajibu maswali niliyokuuliza.
Mungu katokeaje? Kwa nini mungu iwe lazima awepo?
Hujajibu hili swali, ukisema ni asili hujajibu kwa sababu hujaeleza kwa nini ni lazima awepo, na awepo huyu tu.
Upande gani wa maswali yako haujajibiwa?
Maana inawezekana tatizo so kwamba hujajibuwa, tatizo uelewa wako mdogo jibu hulioni hata likiwekwa chini ya pua yako.
God is Nature. Utakapopata chanzo cha Asili, haitobaki kuwa Asili tena.
Umetoa wapi hoja ya kuwa Uwepo wa Mungu ni wa lazima? Uwepo wa Mungu si swala la Ulazima wala Kutokuwa lazima! Ulazima au laa, havina mahusiano na Uwepo wala Ukuu wa Mungu!
Usiwe mzuri wa kukwepa maswali, laiti ungekuwa unajibu maswali yangu, ungeeleweka. Jibu haya;
1. JE, KUJITOSHELEZA NI MAPUNGUFU?
2. Unawezaje kututenganishia Uwepo wa Mungu na Mungu, kufikia hatua ya wewe kudai Mungu anahitaji uwepo wake? Ni kwa namna gani tunaweza kumuona Mungu bila uwepo wake, au Uwepo wake bila Mungu! Usiwe unakurupuka!
Anaita sasa!
Ni kweli yawezekana upeo wangu ni mdogo ndiyo maana nimeshindwa kuona majibu katika maelezo yako,lakini pia yaweza kuwa wewe ndiyo ukawa na upeo mdogo na ndiyo ukaona maelezo yako yamejibu maswali yangu kumbe sivyo.
Sasa hebu chambua maelezo yako uliyotoa ili tuone kama yamejibu kwa njia gani maswali yangu niliyokuuliza.
Sijaonana na mungu ila characteristic yake anayodaiwa kuwa nayo ya upendo wote inamtaka azuie kuumba ulimwengu ambao una mabaya, na ulimwengu huu tunaona una mabaya mengi.
Hujatoa jibu kwa nini iwe hivyo.
Na kama kuna malaika wameumbwa na kipewa maisha yasiyo mabaya, kwa nino binadamu hajaumbwa na kupewa maisha hayo?
Hata baba anayempa zawadi mtoto mmoja na kumnyima mwingine ataonekana hana haki, sembuse mungu?
Mungu yupo na atakuwepo, ukikubali ukakataa haisaidiii. NI BORA UAMINI YUPO UENDE UKAMKOSA KULIKO UAMINI HAYUPO UMKUTE, UTAUMBUKA SIO KIDOGO.
Hii hatakiwi kua kauli ya alie amini..
Ukiamini amini 1 kwa 1,sio habari za ukimkuta sijui uspomkuta...
Anaetaka aamini kua yupo asie taka na siamini mungu hana hasara juu ya watu hao wawili kati ya anae amin na asie amini..
Mwenye hasara na faida ni mimi na wewe..
Over
Maswali gani?
Kiranga unajua sana mpaka hujui kitu..
Unasema hujawah kumuona mungu, unchojua ni characteristics zake!
How comes ujue sifa zake wakati huamini uwepo wake?
Kisichokuwepo kina sifa gani?
Tulikuwa tunajadili kauli yako ya kusema hautaki kuamini unataka jua,nikakwambia unieleze kujua ni nini na kuamini ni nini.
Unafahamu tofauti ya kusema "characteristics zake anazodaiwa kuwa nazo" na kisema "najua characteristics zake"?
Unaonekana hufahamu.
Na kama hufahamu tofauti ya hayo mawili, kwa nini nifikiri uko qualified kuendelea na huu mjadala?
Huyu jamaa hana majibu, yeye kazi yake ni kuuliza tu. ukimubana anakimbilia kwenye theory za math.
Kama anadaiwa kua nazo na wewe umeamua kuzitumia hizo anazodaiwa, wakati wewe binafsi huzikubali na huzitambui..
Nani hayuko qualified kuendelea na huu mjadala!
Kama ambavyo nimekua nikisema, unapenda kugeuza maelezo wakati wa kutoa majibu(naona sasa unataka tofauti ya maneno na sio issue ya uwepo wa mungu)
By the way hatujadili mada kwa kuangalia qualifications za mtu, bali tunaangalia content ya hoja zake,
Naweza nikawa siko na sifa za kujadili huu mjadala, wewe sifa hizo unazo? Anazipima nani? Au wewe mwenyewe?
Tulikuwa tunajadili kauli yako ya kusema hautaki kuamini unataka jua,nikakwambia unieleze kujua ni nini na kuamini ni nini.
hivi ni mungu ndio aliyemuumba mwanadamu au mwanadamu ndio aliyemuumba mungu?..kama mungu ndio aliyemuumba mwanadamu iweje sasa mungu huyo awe tofautitofauti?nasema hivyo kwasababu kuna wanaoamini sanamu kama mungu wao,wengine ng'ombe ndio mungu wao,kuna mtu huko kenya anajiita mungu na watu wanamuabudu kama mungu wao na maisha yanaenda..historia inaonyesha wazee wetu wazamani walikuwa ni polytheists(waliamini mungu zaidi ya mmoja)ndio sasa ikaja hiyo tunayoambiwa mungu ni mmoja tu...na sisi tukaamini kuwa ni mmoja.what i have realised is that,man created god and started to fear the only god he has created...yes,unachonga kinyago unaanza kukiogopa kinyago kilekile ulichokichonga..
Mkuu Joto Hasira,
Hapa hata mimi ''mtu wa imani kutokana na kuzaliwa ktk familia iliyo ktk ''imani'' inanifanya kujiuliza maswali kibao kama unavyosema kuna Miungu kadhaa kama wote tunavyofahamu ingawa wana-imani wanadai Mungu yupo mmoja tu.
Halafu mwanazuoni Pierre Whalon hapo juu anasema atomi ya hydrogen haiko moja wala atom zingine , maana yake kuwa Mungu siyo mmoja na kama kuna Miungu kibao basi hakuna Mungu, ....If God also exists, then God would be just another fact of the universe, relative to other existents and included in that fundamental dependency of relation.
In other words, God could not be God
Naomba msaada wa ''watu wa imani'' baada ya kusoma nukuu hapo juu waje kuokoa jahazi la Imani