COINCIDENCE: Moja ya ushahidi wa uwepo wa Mungu


Kama suala la. Accident ni God's plan…. Sasa hebu tafakari unadhani ajali zinazotokea Afrika ni Sawa na Ajali zinazotokea Ulaya au Amerika?? Kama jibu ni hapana ina maana Mungu anapenda sana watu wafe kutoka Afrika?? Na jibu hapana unadhani suala la Accident linauhusiano na mungu….
Hebu tuangalie nfabo huu….. Je kabla ya ndege, pikipiki, gari au hata meli kuwepo, ajali zilikuwa katika wakati gani….
 
Kama ni chenga umeikubali kirahisi sana kiasi cha kuhoji uhodari wako.

Chenga ambazo mwenye kuzipinga hasogei mbele anazunguka hapohapo tu,basi ni bora kumuachia azipige maana hazina maana yeyote.
 
Kwani kama hayupo wewe unakosa nini?
Sasa tuamie kwenye upande wako!
Na je, nini mwanzo au asili yako? Kama si mungu?

hakosi chochote, hata akiwa hajui chanzo cha asili ya mwanadam sio ndio kwamba jibu lake ni mungu, kwa kifupi bado hatuna majibu ya asili ya chanzo cha mwanadam yaliyo na uhakika 100%, ndo mana wanasayansi wanaendelea kuchunguza ila kama ww unasema asili ya mwanadam ni mungu basi unatakiwa ulete ushahidi, we are open to learn new idea about the origin of human being.
 

Ushaidi gani ambao unauhitaji kuthibitisha kwamba mungu yupo. tofauti na huo.

je? wewe ukiambiwa uthibitishe kwamba tanganyika imewahi kuwa kuloni la mwingereza utaniambia kitu gani? acha kubisha kitu ambacho kipo wazi.
 
Hujathibitisha kwamba mungu yupo.

Ni wapi humu niliposema nataka kuthibitisha uwepo wa Mungu?Hizo njia unazotaka kupita mie ndiyo njia zangu. Turudi tulichokuwa tukikijadili mwanzo.

Halafu ajabu ni kwamba haujawahi kuthibisha kuwa hakuna Mungu,unachokifanya wewe ni kueleza hisia zako ambazo zinakufanya uamini kuwa hakuna Mungu.
 
Kwani kama hayupo wewe unakosa nini?
Sasa tuamie kwenye upande wako!
Na je, nini mwanzo au asili yako? Kama si mungu?

Swali si kwamba nakosa au napata nini kama mungu yupo, swali ni mungu yupo au hayupo.

Mimi kutokujua mwanzo na asili yangu kikamilifu si uthibitisho kwamba asili yangu ni mungu kama vile mimi kutokujua square root ya mbili ni nini kwa ukamilifu si uthibitisho kwamba square root ya mbili ni nane.

Kinachotakiwa ni wewe unioneshe, kama unasema mungu yupo, ni vipi unaweza kuthibitisha kwamba mungu yupo?

Hili hujafanya bado.
 

Kama huna nia ya kuthibitisha kwamba mungu yupo basi unapiga ramli za ganga ongo tu hapa.
 
Kama huna nia ya kuthibitisha kwamba mungu yupo basi unapiga ramli za ganga ongo tu hapa.

Kwa sababu hatukuwa tukijadili kuhusu uthibitisho wa mungu,we umelileta hili ili kupiga chenga tulichokuwa tukikijadili.

Na wewe ni lini uliwahi kuthibitisha kutokuwepo kwa mungu?
 
Kwa sababu hatukuwa tukijadili kuhusu uthibitisho wa mungu,we umelileta hili ili kupiga chenga tulichokuwa tukikijadili.

Na wewe ni lini uliwahi kuthibitisha kutokuwepo kwa mungu?

Kichwa cha thread kinasema "coincidence-moja-ya-ushahidi-wa-uwepo-wa-mungu". Kama unaona mada haizungumzii habari za uwepo wa mungu, wewe ndiye unayetuondoa kwenye mada.

Hakuna kisichokuwepo ambacho kinaweza kuthibitishwa kwamba hakipo.

Kwa sababu hakipo. Visivyokuwepo havithibitishiki kutokuwepo. Kwa sababu uthibitisho unaendana kwa kanuni na vilivyopo, si vilivyopo.

Kama unapinga, unaweza kunipa mfano wa kitu chochote ambacho hakipo na kimethibitishwa kwamba hakipo.
 
Hujathibitisha kwamba mungu yupo.
That is an old line which died because of lack of evidence and for self refutation. If you have the ability to refute the existence of God with evidence and ready to be defeated intellectually. Let us debate.

God Hater, you are a non theists, isn't it? If non theism were fallible, then per your belief you would be a chemically determined animal with no free-will to choose anything - including your thoughts expressed here. Your non theism cuts it's own throat. In fact, there will be no good or evil in you since morals exists because of God.

If you are ready to debate, why do you believe no God exists when you have no evidence or arguments to justify that belief?
 
Where is your refutation of no God?
 

Mkuu muda mwengine huwa unafurahisha sana.

Kutokuwepo kwa kitu ni hali ya kukosa sifa za kuwepo kitu hicho.
Vitu vyote unavyokubali kuwa vipo basi vina sifa za kuonesha kuwepo kwake. Na ndiyo maana huwa unasema kuwa kama "mungu yupo mbona dunia ina maovu,wakati angeweza kuumba dunia isiyo na maovu".

Hayo huwa ni maneno yako wewe ambayo kwako ni uthibitisho wa kukufanya useme hakuna mungu.
Kwa maana kwamba kakukosekana hizo sifa ndiyo unasema kuwa hakuna mungu.

Sasa leo unapokuja kusema kisichokuwepo hakithibitishibiki unanifanya nikushangae na kukumbuka ule msemo wa kwamba ukiwa muongo usiwe unasahau.
 

Tatizo hujasoma Anselm, hujamsikia Russell, hujui emanant criticism ni nini wala hujui tofauti kati ya logical consistency na the garden variety of non sequitor.

Halafu unataka kubishana na mimi.

Kwa kujua hilo, nimerahisisha sana mjadala kwa kukupa challenge ndogo tu.

Nimeandika "Kama unapinga, unaweza kunipa mfano wa kitu chochote ambacho hakipo na kimethibitishwa kwamba hakipo.".

Hujanipa mfano huu.

Unawaa waa tu kama mbayuwayu aliyepotea njia na kukumbwa na dhoruba asiloweza kulihimili.
 

Mtu mwenye kupenda sana kukariri mambo basi lazima aone namchanganya tunapojadiliana.
Tatizo lako mambo uliyoyakariri hayakufanyi kuwa na upeo mkubwa wa kufikiri kama unavyodhani.

Kila mtu ana watu wake katika mambo yake hivyo sina haja ya kujua nani aliyesema,nachokiangalia ni kipi kilichosemwa.

Huo mfano wako nimekujibu kwa kirefu ila kwa sababu kukariri kumekuathiri ukaona nimekuchanganya.

Unaposema "kisichokuwepo hakithibitishiki". Hoja inayoibuka ni kwamba je,kipi kinachofanya tuseme hiki hakipo na kile kipo?

Kwahiyo kabla ya kukurupuka na kusema kisichokuwepo hakithibitishiki, kwanza tufahamishane kuwa ni kigezo gani kimetumika kusema hicho kitu hakipo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…