COINCIDENCE: Moja ya ushahidi wa uwepo wa Mungu

COINCIDENCE: Moja ya ushahidi wa uwepo wa Mungu

Nimekua nikijaribu kutafuta details ndogo ndogo kujaribu kuja na hitimisho langu kuwa kweli Mungu yupo.

Moja ya ushahidi wa uwepo wa Mungu ni hili la Coincidence.

Kutokana na kukosa maana sahihi ya neno coincidence nitatumia neno lingine linalofanana kwa maana na hili , ili kuweza kuwapa kuelewa kusudio la bandiko hili.

Neno coincidence linalandana kwa maana na neno, accident, luck , fate.

Accident = Ajali, luck = bahati , fate = majaliwa.

Matokeo ya hayo niliyoyataja hapo juu ni kutokana na nguvu za ziada zilizo nje ya uwezo wa mwanadamu.

Mfano; AJALI;

Umeamkaka asubuhi unachukua gari yako kufika barabarani unagonga mtu anakufa!

Kama ungekuua na uwezo wa kugundua kama siku hiyo ungegonga mtu akafa, ungeweza kuchukua maamuzi sahihi ili ajali hiyo isitikee, lakini kwakua jambo hilo lipo nje ya uwezo wako huwezi kulizuia au kuliahirisha.

Bahati:

Imetokea ajali wakafa abiria wengine lakini kwa "bahati" wewe pekee ndie uliyepona. mazingira ya ajali yanaonesha kwamba ilistahili abiria wote wasiwe hai lakini kwa ajabu la wengi wewe pekee umepona. Tunaita hiyo ni "bahati"

Majaliwa;

Unapangilia kuwa daktari lakini , jitihada zako zote hazipelekei wewe kuwa daktari na badala yake unaishia kua mwanasheria. hapa uanasheria unaonekana kua ndio yalikua majaliwa yako, na udaktari ulikua unalazimisha tu.

Tukiangalia tafsiri ya neno majaliwa au fate katika lugha ya kingereza mtu ataona kwamba ili majaliwa yawepo basi kuna kuwa na nguvu za ziada zinazopelekea hayo kuwepo, tuangalie;

FATE:

(i) The supposed force, principle, or power that predetermines events:

(ii) The inevitable events predestined by this force

(iii) A final result or consequence; an outcome.

(iv) An unfavorable outcome in life.

Uchanganuzi huo unaonesha kwamba neno MAJALIWA au fate, ni zao la nguvu zinazotabiri matukio.

Nguvu hizo ni zipi?? Nguvu hizo zinatoka wapi?? nguvu hizo zinazuilika??

Mfano: je unaweza tambua siku yako ya kufa?? je unajua nani anayechukua roho yako?? je unaweza zuia kifo?? Hilo ni jambo gumu kidogo, tujaribu mfano mwepesi kidogo.

Je umeshiriki kwa asilimia ngapi katika kutengeneza matukio katika maisha yako, au kuyazuia au hata kuweza kuyabadilisha??

jibu ni hakuna.

Kwahiyo kama kwa kiasi kikubwa hukuweza kuzuia mengi ya matukio katika maisha yako au kuyabadili, hapo tunapata jibu kwamba lazima kutakua na nguvu ya ziada iliyopelekea jambo hilo kutokea.

Sayansi haibishi kwamba hakuna nguvu bila kuwa na chanzo hizo, hakuna ubishi kwamba nguvu zinzzopelekea kutokea kwa hayo mambo zina chanzo chake.

Kuna weza tokea ubishi wa hicho chanzo cha hizo nguvu, lakini kwa imani yangu naamini kwamba chanzo cha nguvu hizo ni MUNGU.

Kufupisha maelezo, jambo lililopelekea mimi kuandika mada hii ndefu, ni hili dogo tu.

" kuna jirani yangu ninaishi nae mtaa mmoja, tunakuja nyumbani nyakati tofauti, tunalala nyakati tofauti, na tunaamka nyakati tofauti, lakini kila asubuhi lazima tukutane barabarani muda ule ule"

Hii ina maanisha nini??

Kama tunatofautiana muda wa kurudi nyumbani, muda wa kulala, muda wa kuamka, inakuwaje lazima kila siku muda ule ule tukutane barabarani??

Is this fate?? accident?? Luck?? au tunapanga tukutane muda huo???

I rest my case with a conclusion kwamba , Mungu yupo na yeye ndie hupanga maisha yetu. Our life is planned hata kabla hatujazaliwa.

Kama suala la. Accident ni God's plan…. Sasa hebu tafakari unadhani ajali zinazotokea Afrika ni Sawa na Ajali zinazotokea Ulaya au Amerika?? Kama jibu ni hapana ina maana Mungu anapenda sana watu wafe kutoka Afrika?? Na jibu hapana unadhani suala la Accident linauhusiano na mungu….
Hebu tuangalie nfabo huu….. Je kabla ya ndege, pikipiki, gari au hata meli kuwepo, ajali zilikuwa katika wakati gani….
 
Kama ni chenga umeikubali kirahisi sana kiasi cha kuhoji uhodari wako.

Chenga ambazo mwenye kuzipinga hasogei mbele anazunguka hapohapo tu,basi ni bora kumuachia azipige maana hazina maana yeyote.
 
Kwani kama hayupo wewe unakosa nini?
Sasa tuamie kwenye upande wako!
Na je, nini mwanzo au asili yako? Kama si mungu?

hakosi chochote, hata akiwa hajui chanzo cha asili ya mwanadam sio ndio kwamba jibu lake ni mungu, kwa kifupi bado hatuna majibu ya asili ya chanzo cha mwanadam yaliyo na uhakika 100%, ndo mana wanasayansi wanaendelea kuchunguza ila kama ww unasema asili ya mwanadam ni mungu basi unatakiwa ulete ushahidi, we are open to learn new idea about the origin of human being.
 
Ushaidi gani ambao unauhitaji kuthibitisha kwamba mungu yupo. tofauti na huo.

je? wewe ukiambiwa uthibitishe kwamba tanganyika imewahi kuwa kuloni la mwingereza utaniambia kitu gani? acha kubisha kitu ambacho kipo wazi.
 
Hujathibitisha kwamba mungu yupo.

Ni wapi humu niliposema nataka kuthibitisha uwepo wa Mungu?Hizo njia unazotaka kupita mie ndiyo njia zangu. Turudi tulichokuwa tukikijadili mwanzo.

Halafu ajabu ni kwamba haujawahi kuthibisha kuwa hakuna Mungu,unachokifanya wewe ni kueleza hisia zako ambazo zinakufanya uamini kuwa hakuna Mungu.
 
Kwani kama hayupo wewe unakosa nini?
Sasa tuamie kwenye upande wako!
Na je, nini mwanzo au asili yako? Kama si mungu?

Swali si kwamba nakosa au napata nini kama mungu yupo, swali ni mungu yupo au hayupo.

Mimi kutokujua mwanzo na asili yangu kikamilifu si uthibitisho kwamba asili yangu ni mungu kama vile mimi kutokujua square root ya mbili ni nini kwa ukamilifu si uthibitisho kwamba square root ya mbili ni nane.

Kinachotakiwa ni wewe unioneshe, kama unasema mungu yupo, ni vipi unaweza kuthibitisha kwamba mungu yupo?

Hili hujafanya bado.
 
Ni wapi humu niliposema nataka kuthibitisha uwepo wa Mungu?Hizo njia unazotaka kupita mie ndiyo njia zangu. Turudi tulichokuwa tukikijadili mwanzo.

Halafu ajabu ni kwamba haujawahi kuthibisha kuwa hakuna Mungu,unachokifanya wewe ni kueleza hisia zako ambazo zinakufanya uamini kuwa hakuna Mungu.

Kama huna nia ya kuthibitisha kwamba mungu yupo basi unapiga ramli za ganga ongo tu hapa.
 
Kama huna nia ya kuthibitisha kwamba mungu yupo basi unapiga ramli za ganga ongo tu hapa.

Kwa sababu hatukuwa tukijadili kuhusu uthibitisho wa mungu,we umelileta hili ili kupiga chenga tulichokuwa tukikijadili.

Na wewe ni lini uliwahi kuthibitisha kutokuwepo kwa mungu?
 
Kwa sababu hatukuwa tukijadili kuhusu uthibitisho wa mungu,we umelileta hili ili kupiga chenga tulichokuwa tukikijadili.

Na wewe ni lini uliwahi kuthibitisha kutokuwepo kwa mungu?

Kichwa cha thread kinasema "coincidence-moja-ya-ushahidi-wa-uwepo-wa-mungu". Kama unaona mada haizungumzii habari za uwepo wa mungu, wewe ndiye unayetuondoa kwenye mada.

Hakuna kisichokuwepo ambacho kinaweza kuthibitishwa kwamba hakipo.

Kwa sababu hakipo. Visivyokuwepo havithibitishiki kutokuwepo. Kwa sababu uthibitisho unaendana kwa kanuni na vilivyopo, si vilivyopo.

Kama unapinga, unaweza kunipa mfano wa kitu chochote ambacho hakipo na kimethibitishwa kwamba hakipo.
 
Hujathibitisha kwamba mungu yupo.
That is an old line which died because of lack of evidence and for self refutation. If you have the ability to refute the existence of God with evidence and ready to be defeated intellectually. Let us debate.

God Hater, you are a non theists, isn't it? If non theism were fallible, then per your belief you would be a chemically determined animal with no free-will to choose anything - including your thoughts expressed here. Your non theism cuts it's own throat. In fact, there will be no good or evil in you since morals exists because of God.

If you are ready to debate, why do you believe no God exists when you have no evidence or arguments to justify that belief?
 
Kichwa cha thread kinasema "coincidence-moja-ya-ushahidi-wa-uwepo-wa-mungu". Kama unaona mada haizungumzii habari za uwepo wa mungu, wewe ndiye unayetuondoa kwenye mada.

Hakuna kisichokuwepo ambacho kinaweza kuthibitishwa kwamba hakipo.

Kwa sababu hakipo. Visivyokuwepo havithibitishiki kutokuwepo. Kwa sababu uthibitisho unaendana kwa kanuni na vilivyopo, si vilivyopo.

Kama unapinga, unaweza kunipa mfano wa kitu chochote ambacho hakipo na kimethibitishwa kwamba hakipo.
Where is your refutation of no God?
 
Mkuu muda mwengine huwa unafurahisha sana.

Kutokuwepo kwa kitu ni hali ya kukosa sifa za kuwepo kitu hicho.
Vitu vyote unavyokubali kuwa vipo basi vina sifa za kuonesha kuwepo kwake. Na ndiyo maana huwa unasema kuwa kama "mungu yupo mbona dunia ina maovu,wakati angeweza kuumba dunia isiyo na maovu".

Hayo huwa ni maneno yako wewe ambayo kwako ni uthibitisho wa kukufanya useme hakuna mungu.
Kwa maana kwamba kakukosekana hizo sifa ndiyo unasema kuwa hakuna mungu.

Sasa leo unapokuja kusema kisichokuwepo hakithibitishibiki unanifanya nikushangae na kukumbuka ule msemo wa kwamba ukiwa muongo usiwe unasahau.
 
Tatizo hujasoma Anselm, hujamsikia Russell, hujui emanant criticism ni nini wala hujui tofauti kati ya logical consistency na the garden variety of non sequitor.

Halafu unataka kubishana na mimi.

Kwa kujua hilo, nimerahisisha sana mjadala kwa kukupa challenge ndogo tu.

Nimeandika "Kama unapinga, unaweza kunipa mfano wa kitu chochote ambacho hakipo na kimethibitishwa kwamba hakipo.".

Hujanipa mfano huu.

Unawaa waa tu kama mbayuwayu aliyepotea njia na kukumbwa na dhoruba asiloweza kulihimili.
 
Mtu mwenye kupenda sana kukariri mambo basi lazima aone namchanganya tunapojadiliana.
Tatizo lako mambo uliyoyakariri hayakufanyi kuwa na upeo mkubwa wa kufikiri kama unavyodhani.

Kila mtu ana watu wake katika mambo yake hivyo sina haja ya kujua nani aliyesema,nachokiangalia ni kipi kilichosemwa.

Huo mfano wako nimekujibu kwa kirefu ila kwa sababu kukariri kumekuathiri ukaona nimekuchanganya.

Unaposema "kisichokuwepo hakithibitishiki". Hoja inayoibuka ni kwamba je,kipi kinachofanya tuseme hiki hakipo na kile kipo?

Kwahiyo kabla ya kukurupuka na kusema kisichokuwepo hakithibitishiki, kwanza tufahamishane kuwa ni kigezo gani kimetumika kusema hicho kitu hakipo.
 
Back
Top Bottom