Uwepo wa ulimwengu unanifanya niamini kuwa mungu yupo ni kwa sababu kinyume na hivyo maana yake ni kwamba huu ulimwengu umetokea tu wenyewe.
Ni vigumu kusema kwamba huu ulimwengu umetokea tu wenyewe na mambo yakawa yanajiendesha yenyewe,kwa hivyo lazima kutakuwa na mwenyewe huu ulimwengu na ndiye mwenye kuhusika na yanayoenda humu ulimwenguni(kuchomaza jua na kuzama,mvua n.k). Mungu ndiye mwenye kusema(ktk vitabu) kuwa yeye ndiye aliyeumba huu ulimwengu.
Kuwepo vinginevyo kwa huu ulimwengu inamaana ya huu ulimwengu umetokea tu wenyewe,na kama nilivyosema inakuwa ngumu kuamini hivyo.
Tushaeleza sana kwamba ameumba hivi kwa sababu, na yote anaonesha uwezo wake,maana angetaka kufanya huu ulimwengu kutokuwa na maovu angefanya.
Umejiridhishaje kwamba fafanuzi zilizopo ni ulimwengu kuumbwa na mungu au kutokea wenyewe tu?
Unajuaje kwamba wewe fikra zako za kwamba ama ulimwengu umeumbwa na mungu ama kutokea wenyewe si fikra za kufuata kitu kama line ya reli inayoweza kwenda mbele na nyuma tu bila kujua kwamba kuna juu na chini?
Unajuaje kwamba hakuna fafanuzi nyingine zaidi, fafanuzi ambazo labda hata hatujapata elimu ya kuzielewa kwa sasa?
Na kama ulimwengu huu kwa jinsi ulivyo, in terms of order/intelligence, ni lazima uwe umeumbwa na mungu, then hilo linatueleza kwamba order/intelligence huwa haitikei tu, ni lazima ipangwe/iumbwe.
Kama ni hivyo, mungu aliyeumba ulimwengu yeye ana order/intelligence zaidi ya ulimwengu aliouumba.
Kama ni hivyo, ufafanuzi wako unazalisha swali lingine, ikiwa intelligence/order ninlazima oumbwe na haiwezi kutokea yenyewe (ndiyo maana unasema ulimwengu ni lazima uwe umeumbwa na mungu, na hauwezi kiwa umetokea wenyewe tu) je huyo mungu aliyeumba ulimwengu na mwenye intelligence na order kuliko ukimwengu naye kaumbwa na nani?
Maana kwa mujibu wa kanuni yako inayosema kwamba hakuna order/inyelligence inayoweza kutokea yenyewe tu, ni lazima iwe na muumba, hata mungu wako atahitaji muumba, na muumba wake atahitaji muumba, na muumba wake atahitaji muumba, ad infinitum, ad absurdum.
Unajikuta umemfanya mungu wako kuwa si mungu at all, bali ni a small cog in an infinite machine.
Unaona habari zako zinavyojichanganya na kujipinga zenyewe sasa?
Kwa jusema ulimwengu hauwezi kutokea wenyewr bula kuumbwa na mungu, undirectly umesema hakuna mungu.
Kwa maana mungu utakayemsema kauumba ulimwengu naye atahitaji mungu, na mungu wake atahitaji mungu, ad infinitum, ad absurdum, kama nilivyotaja hapo juu.
Habari ya mungu inajikanganya kwa mara nyingine tena.
Pia unasema ameuumba ulimwengu hivi kwa sababu, na angetaka kuuumba ukimwengu bula maovu angeumba.
Kusema hivi hakujibu swali langu.
Swali langu halikusema kwamba kaumba ilimwengu inaoruhusu maovu bila sababu, limeuliza kwa sababu gani?
Hujajibu swali.
Hujanipa sababu iliyomfanya mungu mwenye uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote aumbe ulimwebgu ambao inaruhusu maovu yasiyosemeja wakati alokuwa na uwezo wote wa kuumba ulimwengu ambao maovu hayawezekani.
Hujalijibu swali hili.
Nikikuuliza, kwa nini unatembea hivyo? Ukinijibu "kwa sababu", unakuwa hujajibu swali kimantiki.
Kwa sababu hujanipa sababu inayokufanya utembee hivyo.
Ndicho ulichofanya hapa.
Badala ya kunipa sababu iliyomfanya mungu aumbe ulimwengu unaoruhusu uovu, unaniambia kaumba ulimwengu hivyo jwa sababu.
Umekimbia swali, hujajibu swali,