COINCIDENCE: Moja ya ushahidi wa uwepo wa Mungu

Swali halikuwa kama unaamini, swali likikutaka uthibitishe kwamba yupo.

Viwili hivi ni tofauti.

Kama hujui tofauti kati ya kuamini na kuthibitisha, nitajuaje kama una basic requirements za kuweza kushiriki mjadala huu?
Okay.......nawewe mwenyewe ulishindwa kuthibitisha kama hayupo, kwa sababu ulieleza matatizo tu ya dunia hii. Je waweza thibitisha sasa kuwa hayupo?
 
Okay.......nawewe mwenyewe ulishindwa kuthibitisha kama hayupo, kwa sababu ulieleza matatizo tu ya dunia hii. Je waweza thibitisha sasa kuwa hayupo?

Ulilisoma na kulielewa jibu langu la swali lako kwangu kuhusu mimi kuthibitisha kwamba hayupo?

Kama umelielewa unaweza kulirudia kwa maneno yako hapa ili na mimi nielewe kwamba umeelewa?
 
Kwani ww unataka uthibitisho gani? Naww thibitisha hayupo, hatutaki utuorodheshee matatizo ya duniani....duniani kuna raha pia na taabu zipo.
 
Nimesoma mijadala ya watu pamoja na ya mleta uzi na nimegundua kwamba BINADAMU NDIO AMEMTENGENEZA / AMEMUUMBA MUNGU KUTOKANA NA KUSHINDWA KUPATA MAJAWABU YA VITU MBALIMBALI VILIVYOMZUNGUUKA.

Ni rahisi sana kusema umegundua hivyo hasa ukiwa wewe pia ni mmoja usiyeamini mungu. Ila watu wengi wameshindwa kuuelewa vizuri huu mjadala hata ambao wanaamini mungu.

Ngoja nikuulize kitu ambacho watu wengi wanaofuatilia huu mjadala wameshindwa kugundua.

Hivi wakati unausoma huu mjadala je,umeona kuwa wasioamini mungu kama kweli wapo hapa kwa ajili ya kuutafuta ukweli wa kwanini watu wanasema kuna Mungu? Au wapo hapa kwa ajiri ya kutetea kile wanachokiamini wao tu kuwa hakuna mungu?


Naamini utaweza kunijibu vizuri kwa sababu umefanya uchuguzi wa huu mjadala.
 
Ulilisoma na kulielewa jibu langu la swali lako kwangu kuhusu mimi kuthibitisha kwamba hayupo?

Kama umelielewa unaweza kulirudia kwa maneno yako hapa ili na mimi nielewe kwamba umeelewa?
Okay...rudia ile sentensi yako uliyoeleza kuwa kuna ubaya, vita n.k. kama sijakuelewa, nitakuelewa
 
Kwani ww unataka uthibitisho gani? Naww thibitisha hayupo, hatutaki utuorodheshee matatizo ya duniani....duniani kuna raha pia na taabu zipo.

Umelielewa jibu la swali lako hili nililokupa?

Inaonekana hujalielewa.

Unaweza kuthibitisha chochote ambacho hakipo kwamba hakipo?

Sijauliza kuhusu raha, nimeuliza kwa nini mungu kaumba ulimwengu ambao unawezekana kuwa na matatizo na tabu? Wakati aliweza kuumba ukimwengu ambao hauna wala hauwezekani kuwa na tabu?

Hujajibu swali hili, unajaribu kulizunguka tu.
 
Safi sana kwa swali zuri...naamini kaelewa na atakuja na majibu...
 
Kwa nini mungu mwenye uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote aumbe ulimwengu unaoruhusu ajali kutokea na viumbe wake kuumia vikali na hata kufa?

Wakati alikuwa na uwezo wote wa kuumba ulimwengu ambao ajali haiwezekani.

Hiyo ni will kama ambavyo wewe unawaza mambo yako yaliyomema ila kwa wengine wanaweza kuyaona mabaya. Kwahiyo issue ya ajali, majanga, vifo ni mapenzi ya Mungu wenda kwake anatafsiri sahihi nzuri na anapendezwa na kifo chetu baada ya kukosa utiii kwake.
 
 

The problem here its so diffucult to know about the will of ones above all God's will can't be known to people until when He decides to reveale it.
 
Napokuta mijadala kama hii humu huwa ninaipenda kweli kwa kuwa huwa ninaiangalia kwa jicho la kuwa neutral ili kuweza kuishughulisha akili kujua ukweli kuhusu mungu kwa mtazamo wa kibinadamu na huwa nakwenda mbali zaidi kujiuliza hivi kwanini mie ni mkristo au kwanini mie ni mkatoliki au mlutheri baadae napata jibu au babu yangu alikuwa hivyo au baba yangu then nakwenda mbali zaidi najiuliza tena kwanini sie waafrika tumechelewa kuzipokea hizi dini mpaka kuletewa na wakoloni kama karne moja na ushee ama mbili zilizopita

Haya yote tunayapata humu kwa kuwa tunayajadili kwa akili ya kibinadamu lakini tukienda kule kwenye imani ni utahubiriwa pasipo kutafakari kutokana na kwamba tumevipokea hivi vitu tangu tukiwa watoto wadogo mpaka tumekuwa hivyo fursa ya kuchallenge ili uweze kuelewa kwa undani zaidi tunakosa na hii ndio maana kutokana na utofauti wa kuelewa vitu ndio maana unakuta kuna maeneo watu wanatofautiana uelewa na kunakuwepo dini na madhebu kibao lakini mwisho wa siku wote wanahubiri uwepo wa mungu huku kila mmoja na mbinu yake.
 
Alipouumba, aliuumba kwa kuwezesha mabaya kufanyika au alikataza mabaya kuwezekana?

Ni sawa na kunilazimisha nikwambie Kikwete alifikiri nini hasa alipogombea urais.

Nachokijua ni kwamba ulimwengu ndiyo wa kwanza kuumbwa kabla ya binadamu, na kuna viumbe walikuwepo wakiishi kabla ya binadamu.

Na pia huu ulimwengu kuna wanaofanya maovu na wanaofanya mazuri.
 

Tafsiri ya maandiko kiebrania Adam means man kwa maana ya mwanaume kwa hiyo watu Wawili it means two sex ndivyo ilivyokuwa kwa viumbe wengine pia.
 
Last edited by a moderator:
Ni kweli ila humu jf kuna watu tofauti tofauti, usipokuwa makini unaweza ukawa sehemu mbaya kuliko uliyokuwa kwanza. Kila mtu anahubiri atakavyo, kuna wanaohubiri Mungu hayupo, kuna wanaofundisha watu uchawi ...kuna kila kila aina ya watu. Na kila mtu anahubiri kwa manufaa ya kikundi chao au nia yakupoteza umma ili uelekee gizani. Chamsingi ni kwamba, kama ubaya upo duniani jua kuna chanzo cha huo ubaya na pia kama wema upo pia kuna chanzo cha huo wema. Toka tumekuwa watoto twashuhudia miujiza mashuleni, maprofesa ( wachawi, waganga wa kienyeji) walikuwa wakiifanya, hii leo mtu akwambie hakuna miujiza au uchawi utamuuelewa? Kuna vitu vingi huwezi kuthibitisha ktk ulimwengu wa mwili bali ni mambo ya kiroho zaidi
 

Ndipo hapo ujue God at work mtamjua kwa njia mbalimbali ila lengo moja tu! Mungu huwezi mjua mpaka siku akijidhirisha kwako unachoweza fanya ni kumsikia tu katika masimlizi ya walio wahi kumwona kwa njia mbalimbali. Imani inajengwa na masilimlizi ya matendo ya Mungu.
 
Ameeen....! Halafu kwa kawaida binadamu anauwezo ambao limited kwa kila jambo. Mfano audible range ( 20HZ-20KHZ). Njee ya hapo either usisikie au masikio ya pasuke, na hata ktk kuona kuna range twaweza ona. Kwahiyo hata uwezo wa kufikiri...upo limited pia...Mwenyenzi- Mungu awabariki
 

Ushoga ni mpango wa mungu,hebu pinga tuone kabla sijathibitisha !
 

Mkuu wengi wasiyoamini mungu nao walitokewa na hali kama uliyonayo wewe sasa. Na umepoteza muda wako sana ktk umri uliyonao kuwa muumini wa hiyo imani uliyonayo kwa sababu tu et babu yako alikuwa imani hiyo.

Tumia akili vyema acha kuamini kibubusa kama ulivyo sasa. We Utafute ukweli maana hata hao wanaosema hakuna Mungu hawautafuti ukweli, hata ukitizama hoja zao utagundua hilo.
 

sasa hapo mjuaji si niwewe unaesema hayupo.ila anaesema yupo sio mjuaji maana kunavitu vingi havielewi ndomana anamueka nadharia mwenyenzi MUNGU..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…