Inawezekana umeshamuona pasipo kujua coz matendo Yake yanaonesha wazi juu ya uwepo wake
Mungu yupo jamaa kadadavua vilivyo juu ya uwepo wa Mungu
mwambie kiranga huyo anataka kututoa imani.mwezi huu....
Sijaelewa msomi. Kwa sababu haiwezekani nitake uthibitisho wa jambo fulani, sasa mtu atakaponiambia "nimethibitisha kitu ndotoni, kwa sababu nimeota ni uthibitisho wangu". Si tu kwamba atakuwa bado hajathibitisha bali pia atakuwa ameongea utumbo kabisa.
Sasa labda msomi unieleza, inapotokea mtu anaambiwa athibitishe jambo fulani halafu huyo anayeambiwa athibitishe anasema kwamba "nimethibitisha kitu ndotoni" je,kweli kauli hiyo ni uthibitisho(siulizi kwamba ni uthibitisho sahihi au si sahihi) kwa maana kwamba inafaa kuitwa ni uthibitisho?
Halafu haujanijibu swali hili:
Hivi uthibitisho hauwi wa ukweli kama hakijatumika kipimo cha
mwenyekutaka huo uthibitisho au uthibitisho unaweza ukawa wa ukweli ila usikubaliwe kwa sababu kipimo cha mtaka huo uthibitisho hakipo?
nijothemaster umetisha mkuu kwa hayo maswali ulompa....yani anaamini kabisa kuwa dunia ni mviringo wakati wala hajawahi kupanda chombo chochote cha angani ili akathibitishe hilo
anaamini kabisa kama baba na mama yake kweli ndo wazaz wake kwa kuambiwa tu...hajawahi kuthibitisha hilo
anaamini moyo wake unadunda na kusukuma damu hata hajawahi kuuona
anaamini kabisa kuwa akiumwa ugonjwa fulani na daktari akamwambia hvo na kumpa dawa anaitumia dawa ile na anapona...kaambiwa tu hajathibitisha kabisaa
afadhali hata wanaosema hawana uhakika na uwepo wa Mungu huku wanaendelea na research zao kujua ukweli kuliko kiranga anahitimisha kwa hoja dhaifu na sababu zile zile za mfumo wa kuuliza maswali yaleyale kila siku... Kiranga jipange asee
Hata swali hujalielewa mpaka sasa. Sijauliza kwa nini ulimwengu una maovu. Nimeuliza kwa nini mungu mwenye uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote akaamua kuumba ulimwengu ambao unaruhusu maovu wakati alikuwa na uwezo wa kuumba ulimwengu ambao hauruhusu maovu.
Maswali mawili haya ni tofauti, na kama huelewi tofauti yake, sitegemei kwamba utaweza kujibu swali langu.
Hujajibu swali. Kama unamuelewa mungu unatakiwa ujue reasoning yake.Kama huwezi kujibu huelewi reasoning.Kama huelewi reasoning ya mungu humuelewi idea ya mungu huyo, kama huelewi idea ya mungu huyo unaweza kufikiri yupo wakati hayupo, katungwa tu na watu.
Nilichohoji ni sababu zilizomfanya mungu kuumba ulimwengu ambao unawezekana kuwa na mabaya na matatizo wakati ana uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote wa kuumba ulimwengu ambao hauna matatizo.
Hujajibu swali hili.
Jibu la kutupa mitihani linapwaya, kwa sababu mungu anayejua yote, kuweza yote na mwenye upendo wote hahitaji kutupa mitihani ya kutuua na kututesa ili kuweza kufanya chochote anachotaka.
Kwa nini mungu kaumba ulimwengu ambao binadamu anaumia na kuteseka sana kwa maovu, tena wengine watoto wadogo ambao hata hawana hatia, wakati alikuwa na uwezo wa kuumba ulimwengu ambao hauna mabaya?
Huyu mungu hana huruma? Mbona mnasema ni mwingi wa huruma?
Sasa vile vitoto vinavyokufa kwa mafuriko Shinyanga (tumeona picha zinatisha) hakuvihurumia alipoumba ulimwengu ambao mafuriko yanaweza kutokea na kuua vitoto masikini?
Kwa nini mungu hakuumba ulimwengu ambao mafuriko hayawezi kutokea wakati alikuwa na upendo wote, ujuzi wote na uwezo wote kwa mujibu wenu?
Hujanipa sababu zinazoeleweka kimantiki.
"wakati alikuwa na uwezo wa kuumba ulimwengu ambao hauruhusu maovu."
Ndiyo vilevile tu,ameumba ulimwengu ambao unaruhusu maovu kwa sababa ya kutufanyia mtihani kwetu.
kwanini Rais Jose
Mujica ni tajiri halafu aamue kuishi maisha sawa na raia wengine,kwanini atake maisha ya
usawa wakati yeye uwezo anao?
Kuna anayemlazimisha kuishi maisha ya kawaida na usawa?
Kwa nini ahitaji maovu ili kutupa mtihani?
Mungu alishindwa kuumba ulimwengu ambao hauna maovu lakini una mtihani katika mazuri tu?
Mujica ametoa sababu zake, nimezielezea hapo juu. Nimekuuliza sababu za mungu ni zipi? Hujazielezea.
Unaeleza habari ya mtihani, mtihani si sababu ya ulimwengu kuwa na maovu, kwani mungu alishindwa kuuma ulimwengu ambao una mtihani ila hauna maovu?
Kwa nini mungu ahitaji kutupa mtihani at all?
Kwa nini unaogopa kutokwa na imani ambayo huwezi hata kuitetea kwa kuielezea kimantiki?
Unatakiwa uwe na uwezo ama wa kuitetea imani yako, au kuiacha kwa sababu haiteteeki.
Habari yako ya kukataa ukweli kwa sababu unaogopa ukweli utakutoa katika imani yako ya uongo ndiyo habari ya "cognitive dissonance" niliyoiongelea katika post #678 .
cc: bona
kwanini Rais Jose Mujica ni tajiri halafu aamue kuishi
maisha sawa na raia wengine,kwanini atake maisha ya
usawa wakati yeye uwezo anao?
Kuna anayemlazimisha kuishi maisha ya kawaida na usawa?
inaweza kua ww ndo unatatizo lakutoelewa comment za wenzanko...swala la imani si nshaeleza hapo, na hata ww tukiangalia unaimani nyingi tu..tena kwavitu visivyo namajibu...jaribu kufikiri japo kidogo ujiulize vizur...
umethibitishiwa,umeoneshwa,umefafanuliwa..lkn huoni..jarbu kufikiri kdogo ikibi uzirudie coment kabsa labda utaelewa vzur..
swali lako linajibiwa unauliza tena linajibiwa unauliza,.huelewi au makusudi....
Nakujibu swali lako, natumaini na wewe utajibu swali langu.
Rais Mujica ameamua kuishi maisha kama ya raia wa kawaida kwa sababu anaamini katika usawa wa binadamu na hataki viongozi kuishi maisha tofauti sana na wanaowaongoza, hiyo ndiyo sababu yake, nimekupatia jibu, swali lako lilitaka sababu ya kwa nini rais Mujica anaishi maisha sawa na raia wengine.
Umeuliza swali, umepewa jibu.
Sasa zamu yangu.
Kwa nini mungu mwenye uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote kaamua kuumba ulimwengu ambao mabaya yanawezekana wakati alikuwa na uwezo wa kuumba ulimwengu ambao mabaya hayawezekani?
Hujajibu swali kimantiki.
Kama nilivyoeleza kwamba sababu ni ili iwe mtihani kwetu kwa atakayefaulu basi amemuandalia makazi yake na kwa atakaye feli pia amemuandalia makazi yake. Kwahiyo utaona haya maisha hapa ulimwenguni ni kama safari tu.
Kwa hiyo mungu alishindwa kuumba ulimwengu ambao hauna mabaya lakini una mtihani?
Na kwa nini mungu muweza yote, mjuzi wa yote na mwenye upendo wote ahitaji mtihani?
Huko mbinguni kuna ukosefu wa sehemu za kukaa watu useme mungu hawezi kuwapeleka wote ahitaji mtihani kuwachuja?
Huyo mungu hajui yote useme kwamba anahitaji mtihani ili kuwajua watu?
Mtihani gani upo kwa mtoto wa mwaka mmoja anayefariki kwa mafuriko Shinyanga? Huyo mtoto kapata mtihani gani hapo? Atafaulu au kushindwa kivipi?
Maswali yako yanauliza kwanini aamue hivi na kwanini asiamue vile. Sioni kama upo sahihi kuniuliza maswali ya aina hiyo.
Ni sawa na kuuliza kwanini Rais Jose Mujica aamue kuishi maisha ya usawa kwa kuwa rais lakini anaishi maisha ambayo hayaendani na cheo chake. Kwanini asingejitenga tu na kuishi maisha yake pekee?yani mbali kabisa na kuishi na watu ambapo kusingekuwa na suala la usawa.
Hakuna anayemlazimisha kuishi hivyo.
Nini kinamfanya aamini maisha ya usawa ndiyo sahihi?
Sijui kama umenielewa maana yangu hapo.
Swali langu linatokana na tabia za msingi kabisa mnazosema huyu mungu anazo.
Ambazo no kiweza kufanya vyote, kujua yote na kuwa na upendo wote.
Nilitegemea mungu mwenye uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote aumbe ulimwengu ambao mtoto mchanga wa mwaka mmoja hawezi jufa katika mafuriko.
Kwa sababu hata kama unaweka habari ya mtihani, huyu mtoto mchanga hakuna anachotahiniwa, kwani hajaanza hata kuujua ulimwengu.
Hapo tunaona jibu la mtihano ni la uongo.
Sasa kwa nini mungu mqenye uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote kaumba ulimwengu huu ambao mtoto mdigo kama huyo anaweza kufariki katika a natural disaster wakati mungu angeweza kuumba ulimwengu ambao watoto wachanga hawawezi kufa katika hali mbaya kama hiyo?
Kwa nini mungu kaumba ulimwengu ambao mabaya yanawezekana wakati alikuwa na uwezo, ujuzi na upendo wote wa kuumba ulimwengu ambao manaya hayawezekani?
Hujajibu swali hili kimantiki.
Swali ni sahihi. Kwa sababu ulimqengu tunaouona unapingana na tabia za msingi kabisa za huyo mungu mnayesema yupo. Tabia za kiweza yote, kujua yote na kuwa na upendo wote. Sasa nikiangalia maovu ya dunia nashangaa, imekuwaje mungu huyu akaumba ulimwengu ambao mabaya yanawezekana?
Ina maana alitaka kuumba ulimwengu ambao mabaya hayawezekani akashindwa?
Kama alitaka ila kashindwa, ni kqeli anaweza yote?
Au hakushindwa kuumba ulimwengu usiowezekana kuwa na mabaya ila hakutaka tu?
Kama hakushindwa kuumba ulimqengu b usiowezekana kuwa na mabaya, ila hakutaka tu, ni kweli kwamba anatupenda na ana upendo wote?
Kiranga unarudia sana maswali jaribu kuuliza swali moja moja ili lijibiwe hadi lieleweke.
Nilishaeleza kwamba Mungu hakuyafanya haya maisha kuwa ya raha kiasi usipigwe hata na kijiwe kama utakavyo au ufikiriavyo. Na ndiyo maana nikasema maisha ya ulimwengu ni kama safari. Na tabu zote tunazoziona iwe umasikini, maradhi,ulemavu, n.k
Yote hiyo ni mitihani ktk hii safari kupima imani yako,maana mungu anataka tumuabudu na kufuata yale aliyotuamlisha. Hivyo endapo utaweza kushinda majanga hayo kwa kuendelea kumuabudu na kufuata maamlisho yake na makatazo yake basi tutakuwa tumefaulu mtihani na tutaenda makazi aliyotuandalia na watakao fanya kinyume na hivyo hao ndiyo waliyofeli na watapelekwa ktk makazi waliyoandaliwa.
Hivyo haya maisha ni kama safari.
Na mwisho wa hii safari yetu ni kifo na kila mtu lazima afe. Na kila mtu amepangiwa ni jinsi gani atafu,kwahiyo hao watoto hawana tatizo ila kila mtu amepangiwa kifo chake.
Lakini kuna matatizo ambayo tunayapata kwa kufanya mambo aliyoyakataza,ni kama kununua bidhaa mfano simu halafu ukapewa maelekezo kwamba usiitie maji,ila wewe ukafanya kama ulivyoambiwa usifanye.
Halafu pia sifa za mungu zipo nyingi hata kuumba pia ni sifa yake, sasa isije ikawa kutokuzijui sifa zake ndiyo maana hatuelewani.
Thread hii imejikita katika kutoa ushahidi zaidi ya imani.
Kama unafikiri thread hii inaongelea imani umepotea njia.
Nilishasema hapo mwanzo kwamba imani unaruhusiwa kuwa nayo yoyote, hata ukisema unaamini mungu ni funza aliyeko kwenye kidole cha babu yako, unaruhusiwa na kutetewa na katiba ya Tanzania na "Universal Declaration of Human Rights" ya mwaka 1948.
Ukisema mungu huyo yupo as a matter of fact, hapo ndipo unaanza kuulizwa ushahidi na uthibitisho.
Ushaelewa tofauti sasa? Inaonekana hujaweza kutofautisha matters of fact from matters of faith.
Hujathibitisha kwamba mungu yupo. Kama umethibitisha nipe link hapa.
basi thread yako ndo imepotea njia..kwasababu kile unachowaza ww na thread yako ilivo vipo tofauti....
sababu vithibitisho vya mwenyezi MUNGU kuepo vipo wazi kabisa,tukikueleza ww sasa ndo unaanza kwenda nje ya thread...
nilikwambia mwanzo kule, mwenyezi MUNGU ni MWANZO na MWISHO kama mimi na ww hatujui mwanzo wala mwisho nini hasa tunaishi hapa duniani kama sio kwa imani na matumaini...
kwama tu wewe huzijui dakika mbili mbele nini hasa kinakupa kiburi kuzifikia kama sio imani tu,huo ndo uthibitisho wa MUNGU kuepo..
hakuna kitu wala mtu hapa duniani aliye mfanya binadamu awe na imani,hata hao UN unaosema walikuta watu wanaimani tayar..kilicho wekwa ni uhuru tu wakuamini,kama vile kiranga haanini MUNGU yupo....
kila mmoja anaimani kwa jambo fulani,..kwasababu hamna mtu anayeweza weza kuumba basi yupo aliyeumba huo ni uthibitisho wa MUNGU kuepo..ndomana hatuamini huyo funza,wala sanamu wala binadamu hapa duniani lkn tuna amini kuna MUNGU muumbaji...
hivo jaribu kuilewa thread yako vithibitisho vipo ila nikazi yako kuviamini au usiviamini..kama unaweza kumbingana na hivo vithibitisho tunavyo kupa basi anzisha thread nyingine manake hii thread tutakua tushajibu..ndomana nasema ww ndo unatoka nje ya thread...
Akhasante..